Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yes mkuu Maalim Seif ni legend wa siasa hapa nchini, naamini familia yake itatembea kifua mbele maana msingi uliowekwa na mpendwa wao ulijengwa kwa ukweli, uungwana,push back na hakua mnafiki, ila kitendo cha kuingia kwenye serikali ya umoja na ccm,sikukielewa ila sasa alikua yupo rightSasa uso kwa uso na maalim Seif!
Jamani tumefanya nn sisi watu wa munguIla nyieee....
Japo ni ukweli...
Jina lako na unachokizungumza wala haviendani pole sanaHao waliopoteza maisha kama ni watoto wadogo kweli ni tatizo.
Ama kama watu wazima ni mihemuko Yao ya kisiasa na ushabiki usiokuwa na maana.
Any way kwenye ushabiki hata kwenye mpira watu wanakufaga!! Mimi siwezi kupoteza maisha kwaajili ya kumshabikia Zito,Mbowe au Lipumba huo ni ulimbukeni. Hawa wanasiasa Huwa wanatafuta riziki zao kwenye siasa lakini hapohapo wanawafanya walalahoi ndio ngazi na madaraja ya kuwafikisha kwenye shine zao! SIWAPENDI WANASIASA.
Yaana mtu afariki Dar es salaam halafu useme habari imetoka Zanzibar kweli?!Habari kutoka znz ni kuwa aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha amefariki dunia katika hospital ya Lugalo jijini Dar es salaam.chanzo Radio One
Tutamkumbuka kwa kunajisi uchaguzi Zanzibar 2015Wakati aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha akizikwa,Watanzania tutamkumbuka kwa lipi?
Kwa jinsi alivyo mpindulia mezaa maalim Seif Sharif Hamad.🤔Wakati aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha akizikwa jana katika Kiiji cha Mkwajuni, Mkoa wa Kaskazini Unguja, wadau wa siasa wamemueleza jinsi alivyoacha historia.
Jecha, aliyepata umaarufu baada ya kufuta Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 visiwani Zanzibar, alifariki dunia jana katika Hospitali ya Rufaa ya Jeshi Lugalo, Dar es Salaam. Akizungumza jana Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Hamad Masoud Hamad alisema Jecha atakumbukwa na historia kwa kile alichokifanya hata kama hakufanya kwa ridhaa yake, lakini kwa kuwa yeye ndiye alichukua uamuzi huo.
"Kwanza tumUombee Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema, amsamehe makosa yake, duniani mapito yapo mengi tunafanyiwa, lakini mwisho wa yote yanaisha," alisema
Rais Samia Suluhu Hassan alituma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia kifo hicho, akiwaombea moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Mchambuzi wa siasa kisiwani Zanzibar, Makame Haji alisema Jecha ametangulia mbele ya haki, lakini alikuwa mzalendo wa kweli katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kwa sababu alijitoa na alikuwa yupo tayari kupoteza maisha yake kwa ajili ya Serikali yake.
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Juma Duni Haii alisema yeye na Jecha walitoka kijiji kimoja cha Kibeni na walianza kusoma elimu va msingi darasa moja.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk Muhammed Dimwa alisema chama kimepokea kwa masikitiko msiba huku kikisitisha ziara ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar aliyokuwa akiendelea nayo kisiwani Pemba.
"Huu ni msiba mzito, tumepokea kwa masikitiko makubwa." alisema
WANAJAMVI TUTAMKUMBUKA JECHA KWA LIPI?
Tutamkumbuka Kwa dhulma ya wazenjiWakati aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha akizikwa jana katika Kiiji cha Mkwajuni, Mkoa wa Kaskazini Unguja, wadau wa siasa wamemueleza jinsi alivyoacha historia.
Jecha, aliyepata umaarufu baada ya kufuta Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 visiwani Zanzibar, alifariki dunia jana katika Hospitali ya Rufaa ya Jeshi Lugalo, Dar es Salaam. Akizungumza jana Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Hamad Masoud Hamad alisema Jecha atakumbukwa na historia kwa kile alichokifanya hata kama hakufanya kwa ridhaa yake, lakini kwa kuwa yeye ndiye alichukua uamuzi huo.
"Kwanza tumUombee Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema, amsamehe makosa yake, duniani mapito yapo mengi tunafanyiwa, lakini mwisho wa yote yanaisha," alisema
Rais Samia Suluhu Hassan alituma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia kifo hicho, akiwaombea moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Mchambuzi wa siasa kisiwani Zanzibar, Makame Haji alisema Jecha ametangulia mbele ya haki, lakini alikuwa mzalendo wa kweli katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kwa sababu alijitoa na alikuwa yupo tayari kupoteza maisha yake kwa ajili ya Serikali yake.
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Juma Duni Haii alisema yeye na Jecha walitoka kijiji kimoja cha Kibeni na walianza kusoma elimu va msingi darasa moja.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk Muhammed Dimwa alisema chama kimepokea kwa masikitiko msiba huku kikisitisha ziara ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar aliyokuwa akiendelea nayo kisiwani Pemba.
"Huu ni msiba mzito, tumepokea kwa masikitiko makubwa." alisema
WANAJAMVI TUTAMKUMBUKA JECHA KWA LIPI?
We classmate wa Jecha mwenzio ndio katangulia hivyo nawe anza kutia maji!!Rest Easy Class mate
Wewe mpk lini?We classmate wa Jecha mwenzio ndio katangulia hivyo nawe anza kutia maji!!
Samia atakapofuta mkataba wa kuuza Bandari zetu nami nitamfuata Jecha!! Kumbuka kasema ameziba masikio kwani hana $$$$ alizokula waarabu wanazodai warudishiwe!!Wewe mpk lini?
Au Bado upo Sana
Mi sio mwanasiasa MkuuSamia atakapofuta mkataba wa kuuza Bandari zetu nami nitamfuata Jecha!! Kumbuka kasema ameziba masikio kwani hana $$$$ alizokula waarabu wanazodai warudishiwe!!
Ameshindwa kabisa kufuta kifo jamani
R.I.P JechaAliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) aliyefuta uchaguzi 2015 na kupata umaarufu mkubwa, Jecha Salim Jecha leo amefariki Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam na mwili wake utapelekwa Zanzibar kwa maziko.
Jecha Salim Jecha alipata umaarufu mwaka 2015 baada ya kufuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar. Zaidi soma Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu
Aprili 17, 2018 Salim Jecha Salim aling'atuka rasmi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) baada ya kuhudumu katika nafasi hiyo kuanzia Mei 4, 2013. Zaidi soma Hatimaye 'mtemi' Jecha Salim Jecha ang'atuka
Mwaka 2020, Jecha Salim Jecha alichukua fomu ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM), jambo ambalo lilizua utata ukizingatia mwaka 2015 alikuwa ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar yenye dhamana ya kusimamia chaguzi zote kisiwani humo. Zaidi soma Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC), Jecha Salim Jecha achukua fomu ya urais Zanzibar
Mola amsamehe makosa yake alipoteleza.
View attachment 2691725
Picha maarufu ya Jecha Salim Jecha enzi za uhai wake
---
Rais Samia ahani msiba wa Marehemu Jecha Salum Jecha
View attachment 2693134
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wanafamilia wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Marehemu Jecha Salum Jecha mara baada ya kuwasili katika Kijiji cha Mkwajuni Uyagu Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa ajili ya kutoa pole.