TANZIA Jecha Salim Jecha afariki dunia akipatiwa matibabu hospitali ya Jeshi Lugalo

TANZIA Jecha Salim Jecha afariki dunia akipatiwa matibabu hospitali ya Jeshi Lugalo

Hata wewe hapo una madhambi na bado unaishi!! Kifo na madhambi anayoyapenda mtu havina uhusiano wowote .
Wabaya wanakufa na wazuri wanakufa.
Kwahiyo kufurahia kifo Cha mtu wakati wewe hujui utakufa lini ni upumbavu uliopitiliza.
Acha afe tu mimi hainihusu kama wangekuwa wanafufuka ningeomba afe tena, una la zaidi.
 
Hata hawa wa mkataba wa kihuni wajitafakari sana sana na waangalie mitandao ya kijamii kuhusu Jecha ili wajifunze mapema.
 
Hata hawa wa mkataba wa kihuni wajitafakari sana sana na waangalie mitandao ya kijamii kuhusu Jecha ili wajifunze mapema.
Sisi wanamitandao ya kijamii tunamuombea jecha dua njema kabisa kwa sababu kila alipoteleza kibinadamu ilikuwa ni kwa shinikizo la nyie watanganyika.
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) aliyefuta uchaguzi 2015 na kupata umaarufu mkubwa, Jecha Salim Jecha leo amefariki Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam na mwili wake utapelekwa Zanzibar kwa maziko.

Jecha Salim Jecha alipata umaarufu mwaka 2015 baada ya kufuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar. Zaidi soma Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Aprili 17, 2018 Salim Jecha Salim aling'atuka rasmi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) baada ya kuhudumu katika nafasi hiyo kuanzia Mei 4, 2013. Zaidi soma Hatimaye 'mtemi' Jecha Salim Jecha ang'atuka

Mwaka 2020, Jecha Salim Jecha alichukua fomu ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM), jambo ambalo lilizua utata ukizingatia mwaka 2015 alikuwa ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar yenye dhamana ya kusimamia chaguzi zote kisiwani humo. Zaidi soma Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC), Jecha Salim Jecha achukua fomu ya urais Zanzibar

Mola amsamehe makosa yake alipoteleza.

View attachment 2691725
Picha maarufu ya Jecha Salim Jecha enzi za uhai wake​
MHSRIEP
 
Back
Top Bottom