TANZIA Jecha Salim Jecha afariki dunia akipatiwa matibabu hospitali ya Jeshi Lugalo

TANZIA Jecha Salim Jecha afariki dunia akipatiwa matibabu hospitali ya Jeshi Lugalo

Unamlaumu tu bure, yeye binafsi asingeweza kufanya vile bila kushurutishwa/kuagizwa na wenye nchi.
Mtu yeyote anaponiambia habari za kushurutishwa au kuagizwa kutenda mambo kinyume na sheria za nchi huwa namuuliza kama anamfahamu Prof. Mussa Assad.

Kwa mtu muadilifu( ambao kwa Tanzania ya leo ni watu wachache sana) ni bora umtoe uhai wake lakini sio kumtoa kwenye misingi yake ya uadilifu.

Tusitetee wahuni kwa mwavuli wa kushurutishwa au kuagizwa.

 
Kwa maamuzi yake ya kipumbavu na ubinafsi alisababisha watu kupoteza maisha na wengine kuhama nchi kuwa wakimbizi, watetezi wake wanasema bila yeye nchi ingerudi kwa extremist ambao wangeirudisha nchi kwa sultani
 
Umenisaidia sana! Nilikuwa najiuliza sababu ya wabara kucheza Ngoma ya wazanzibari ikawa sielewi kumbe Kuna kugawana faida ikiwa muungano utavunjika!!! Any way nadhani muungano huu ni kwaajili ya kulinda maslahi ya chama tawala upande wa bara na pia znz.
Leo la muungano lilikuwa ni hatari ya visiwa vya zenj kuwa islamic state.Ndo maana Tanganyika wakaogopa na ikabidi waungane na Zanzibar. Sasa kwa sasa ili muungano uendelee kuwepo inabidi chama tawala (Afro Shiraz + TANU) kiendelee kubaki madarakani.
 
Unaandika upumbavu halafu unasema eti "wabillaahil tawfiyq.??!!"
Unataja jina la Allaah baada ya kuandika maneno ya jeuri na uadui kwa muislamu mwenzio aliyekufa au wewe ni kafiri?!
Wewe muislamu kweli kuendeleza maneno ya visasi na marehemu.
Kama wewe siyo mtoto una uhakika hujawahifanya dhambi hapa duniani ? Sisi sote ni watenda dhambi, na sisi sote tunahitaji msamaha wa mola wetu.
Sera ya uislamu kwa waislamu wenzetu waliotangulia ni kusema:
ربنا اغفر لنا ولإخواننا الذين سبقونا بالإيمان ولا تجعل في قلوبنا غلا للذين آمنوا ربنا إنك رووف رحيم.
Kaka,alichowafanyiwa Wanzanzibar ni dhulma lakini
Na huyo Mungu anachukua dhulma na atalipwa Kwa ubaya wake

Wala usimlaumu Huyu kaka aliyeandika Jecha aliringia kibri Cha madaraka na pumzi ,Leo amekufa akakutane na mola wake na dhulma aliyoifanya ikalipwe vzr
Yaani kumuombea maghfra Jecha labda kwanza arudishe Kila alichokifanya kwanza ndo asamehewe...

Na huwezi mtoa mtu ktk uislam Kwa hiloo unless kama ni mushriki huyo mtu
 
Punguza maswali ya kijinga. Ingekuwa hivyo, mtume angekuwa hai mpaka Leo. Watu wanaongelea ujinga alioufanya huyo Jecha Zanzibar. Watu wameshakabidhiwa vyeti vya ushindi yeye anaamka na kufuta matokeo. Very stupid
Hapana yule baba hapana kiukweli wengi tumefarijika na Hili la yeye kupumzika Kwa amani ...dhulma alofanya daahhh
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) aliyefuta uchaguzi 2015 na kupata umaarufu mkubwa, Jecha Salim Jecha leo amefariki Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam na mwili wake utapelekwa Zanzibar kwa maziko.

Jecha Salim Jecha alipata umaarufu mwaka 2015 baada ya kufuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar. Zaidi soma Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Aprili 17, 2018 Salim Jecha Salim aling'atuka rasmi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) baada ya kuhudumu katika nafasi hiyo kuanzia Mei 4, 2013. Zaidi soma Hatimaye 'mtemi' Jecha Salim Jecha ang'atuka

Mwaka 2020, Jecha Salim Jecha alichukua fomu ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM), jambo ambalo lilizua utata ukizingatia mwaka 2015 alikuwa ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar yenye dhamana ya kusimamia chaguzi zote kisiwani humo. Zaidi soma Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC), Jecha Salim Jecha achukua fomu ya urais Zanzibar

Mola amsamehe makosa yake alipoteleza.

View attachment 2691725
Picha maarufu ya Jecha Salim Jecha enzi za uhai wake​
Kwanini hakupelekwa DP World!,ohhh sorry nilimaanisha Dubai,
 
Back
Top Bottom