TANZIA Jecha Salim Jecha afariki dunia akipatiwa matibabu hospitali ya Jeshi Lugalo

Sasa uso kwa uso na maalim Seif!
Yes mkuu Maalim Seif ni legend wa siasa hapa nchini, naamini familia yake itatembea kifua mbele maana msingi uliowekwa na mpendwa wao ulijengwa kwa ukweli, uungwana,push back na hakua mnafiki, ila kitendo cha kuingia kwenye serikali ya umoja na ccm,sikukielewa ila sasa alikua yupo right
 
Jina lako na unachokizungumza wala haviendani pole sana
 
Habari kutoka znz ni kuwa aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha amefariki dunia katika hospital ya Lugalo jijini Dar es salaam.chanzo Radio One
Yaana mtu afariki Dar es salaam halafu useme habari imetoka Zanzibar kweli?!
 
Wakati aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha akizikwa jana katika Kiiji cha Mkwajuni, Mkoa wa Kaskazini Unguja, wadau wa siasa wamemueleza jinsi alivyoacha historia.

Jecha, aliyepata umaarufu baada ya kufuta Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 visiwani Zanzibar, alifariki dunia jana katika Hospitali ya Rufaa ya Jeshi Lugalo, Dar es Salaam. Akizungumza jana Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Hamad Masoud Hamad alisema Jecha atakumbukwa na historia kwa kile alichokifanya hata kama hakufanya kwa ridhaa yake, lakini kwa kuwa yeye ndiye alichukua uamuzi huo.

"Kwanza tumUombee Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema, amsamehe makosa yake, duniani mapito yapo mengi tunafanyiwa, lakini mwisho wa yote yanaisha," alisema

Rais Samia Suluhu Hassan alituma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia kifo hicho, akiwaombea moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Mchambuzi wa siasa kisiwani Zanzibar, Makame Haji alisema Jecha ametangulia mbele ya haki, lakini alikuwa mzalendo wa kweli katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kwa sababu alijitoa na alikuwa yupo tayari kupoteza maisha yake kwa ajili ya Serikali yake.

Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Juma Duni Haii alisema yeye na Jecha walitoka kijiji kimoja cha Kibeni na walianza kusoma elimu va msingi darasa moja.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk Muhammed Dimwa alisema chama kimepokea kwa masikitiko msiba huku kikisitisha ziara ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar aliyokuwa akiendelea nayo kisiwani Pemba.

"Huu ni msiba mzito, tumepokea kwa masikitiko makubwa." alisema


WANAJAMVI TUTAMKUMBUKA JECHA KWA LIPI?
 
Wakati aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha akizikwa,Watanzania tutamkumbuka kwa lipi?
Tutamkumbuka kwa kunajisi uchaguzi Zanzibar 2015
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wanafamilia wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Marehemu Jecha Salum Jecha mara baada ya kuwasili katika Kijiji cha Mkwajuni Uyagu Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa ajili ya kutoa pole.

 
Kwa jinsi alivyo mpindulia mezaa maalim Seif Sharif Hamad.🤔
 
Tutamkumbuka Kwa dhulma ya wazenji
 
Wewe mpk lini?
Au Bado upo Sana
Samia atakapofuta mkataba wa kuuza Bandari zetu nami nitamfuata Jecha!! Kumbuka kasema ameziba masikio kwani hana $$$$ alizokula waarabu wanazodai warudishiwe!!
 
Samia atakapofuta mkataba wa kuuza Bandari zetu nami nitamfuata Jecha!! Kumbuka kasema ameziba masikio kwani hana $$$$ alizokula waarabu wanazodai warudishiwe!!
Mi sio mwanasiasa Mkuu
Na sinaga time na siasa
Unanionea tu
 
R.I.P Jecha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…