TANZIA Jecha Salim Jecha afariki dunia akipatiwa matibabu hospitali ya Jeshi Lugalo

TANZIA Jecha Salim Jecha afariki dunia akipatiwa matibabu hospitali ya Jeshi Lugalo

Ee Mungu usimsamehe kosa hata moja huyu mfuta matokeo ya uchaguzi sukuma jehanam anakostahili hana maana kabisa Jesha
 
Afande Kumbulu kama bado uko hapo Mortuary Lugalo Hospital tafadhali uoshe huo Mwili vizuri kama ulivyouosha Kiuweledi wa Marehemu Kapteni John Komba ulipoletwa hapo.
 
Maisha ya Duniani ni mafupi, tutende wema hapa Duniani
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) aliyefuta uchaguzi 2015 na kupata umaarufu mkubwa, Jecha Salim Jecha leo amefariki Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam na mwili wake utapelekwa Zanzibar kwa maziko.

Jecha Salim Jecha alipata umaarufu mwaka 2015 baada ya kufuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar. Zaidi soma Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Aprili 17, 2018 Salim Jecha Salim aling'atuka rasmi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) baada ya kuhudumu katika nafasi hiyo kuanzia Mei 4, 2013. Zaidi soma Hatimaye 'mtemi' Jecha Salim Jecha ang'atuka

Mwaka 2020, Jecha Salim Jecha alichukua fomu ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM), jambo ambalo lilizua utata ukizingatia mwaka 2015 alikuwa ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar yenye dhamana ya kusimamia chaguzi zote kisiwani humo. Zaidi soma Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC), Jecha Salim Jecha achukua fomu ya urais Zanzibar

Mola amsamehe makosa yake alipoteleza.

View attachment 2691725
Picha maarufu ya Jecha Salim Jecha enzi za uhai wake​

---
Rais Samia ahani msiba wa Marehemu Jecha Salum Jecha

View attachment 2693134
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wanafamilia wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Marehemu Jecha Salum Jecha mara baada ya kuwasili katika Kijiji cha Mkwajuni Uyagu Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa ajili ya kutoa pole.​
Huyu jamaa kumbe alifariki mbona hamkusema
 
Hakupenda yeye kufuta matokeo. Kiongozi wa CCM kipindi kile ndiye aliye shinikiza. Si ajabu Jecha alikua MTU wa kupenda haki Sana, Ila pressure from above. Ndio maana alikosa amani Sana wakati akitangaza.
Yeye na huyo kiongozi wawekwe chumba kimoja wafurahiye waliyoyafanya huku wanaungua matumbo!
 
Jecha alinichekesha sana alipochukua form ya kugombea urais wa Zanzibar kupitia ccm yake. Inaonekana Jecha alishamset mrithi wake pale ZEC amtangaze kuwa ameshinda ila maccm bila kukumbuka fadhila kwa mema aliyowatendea wakamkata mapema kwa roho mbaya zao.

Rest easy Jecha. Natumaini unapewa malipo ya staiki yako huko uliko.
 
Jecha alinichekesha sana alipochukua form ya kugombea urais wa Zanzibar kupitia ccm yake. Inaonekana Jecha alishamset mrithi wake pale ZEC amtangaze kuwa ameshinda ila maccm bila kukumbuka fadhila kwa mema aliyowatendea wakamkata mapema kwa roho mbaya zao.

Rest easy Jecha. Natumaini unapewa malipo ya staiki yako huko uliko.
Noma sana
 
Back
Top Bottom