Mnapenda ku catch feelings kwenye vitu vidogo.
Mchambuzi anaongea kupitia takwimu na sio kuridhisha upande eti kwasababu ni timu ya nyumbani au namna gani.
Hapo umem attack kupitia tittle tu ya uzi lakini naimani hujasikiliza sababu za msingi kwanini yeye ameona hivyo.
Huwa nashangazwa sana sometimes unakuta matokeo yamekuja kinyume na wachambuzi walivyobashiri basi kila mtu anaanza kuwarudia kuwatukana.
Hiyo sio fair na ukitaka kuona jaribu kufatilia tu hata hapo studioni wanakuwa wachambuzi wenyewe kwa wenyewe wanatofautiana maono.
Lakini angalia namna wanavyo argue kisomi kukosoa maoni ya mchambuzi mwezake kwa kutoa sababu za mashiko kuonesha namna gani mwezake hayupo sahihi.
Huwezi kukuta wanatukanana kwa hiki kiwango ambacho sisi mashabiki tumekuwa tukiwafanyia.
Mkuu,
Unataka tudadavue uhalali wa hoja ya huyo Mchambuzi? Ungepaswa kutiririka ni kwa namna gani yeye anaona Yanga akifungwa 3 bila huko kwa Madiba.
Mimi naanza kwa kukuletea matokeo ya Marumo Gallants awapo katika ardhi ya nyumbani kwa mechi zote 6 kisha matokeo ya Yanga akiwa ardhi ya ugenini, kisha tupime logic ya Mchambuzi wako.
Mpaka sasa Marumo Gallants kacheza mechi 6 nyumbani;
1.Mtoano
Vs ASSM ELGECO PLUS 1-0
Vs AL AHLI TRIPOLI 3-0
2.Makundi
Vs AL ALKHADAR 4-1
Vs USM ALGER 2-0
Vs SAINT ELOI LUPOPO 3-2
3. Robo Fainali
Vs Pyramids 1-0
Katika hizo mechi sita, ambazo kashinda magoli zaidi ya 3 (kwa scenario ya mchambuzi) ni mechi 3 sawa na 50%. Na katika hizo ambayo katoka na clean sheet ni ni moja tu dhidi ya Al Ahli Tripoli. Nasemea clean sheet kwa sababu hii ni knock out. Mwenzako kupata goli moja tu ni milestone. Akishinda 3-1, Yanga anapita.
Hivyo, katika mechi zake 6, iliyozaa uhakika ya kutoboa kwa goli 3-0 ambayo kasema Leah ni moja ambayo ni sawa na 17%.
Turudi kwa Wenzetu Utopolo kwa Matokeo ya Ugenini. Mind you, tunapaswa kuvitupilia mbali factors zingine na turudi kupima uhalali wa hoja za Leah kwa matokeo ya uwanjani kwa timu zote mbili.
Yanga mpaka sasa katika kombe la Shirikisho kacheza mechi tano;
1. Knock out
Vs Club Africain 0-1
2.Group Stage
Vs Monastir 2-0
Vs AS Bamako 1-1
Vs Tp Mazembe 0-1
3.Robo fainali
Vs Rivers United 0-2
Katika mechi tano, Yanga kashinda mechi 3 ambayo ni sawa na 60% na kutoka droo moja na kushindwa moja. Hivyo, Yanga anaonekana kuwa na rekodi nzuri ugenini. Na katika mechi zote sita, hakuna mechi ambayo kafungwa zaidi ya goli mbili. Hivyo, hiyo 3 ya Leah hakuna. Katika mechi tano, Yanga kafunga katika mechi nne, sawa na asilimia 80.
Sasa hoja yake ya kusema Yanga atafungwa goli 3-0 anaipata wapi? Uwezekano wa kushinda 3 anao, ila si bila. Matokeo sawa yana namna yake, lakini kwa data tu, mchambuzi huwezi kukurupuka na kusema atafungwa kiasi kadhaa cha magoli.
Uwezekano wa Marumo Gallants kushinda upo kama ilivyo nature ya mpira. Lakini si kwa kiwango cha kuaminishwa na Leah.
Twende mdogo mdogo.