Jenerali Mabeyo amuaga Rais Mwinyi. Ajiandaa kustaafu June 2022

Alipaswa awe amestaafu mwaka 2017!! Hakukuwa na ulazima wa yeye kuendelea na kazi baada ya kufikisha miaka 60 hapo june 2017.
 
Ana mabinti huyu mzee? Nataka nipate hiyo mbegu. Muungwana sana huyu jamaa.
 
Anakaa ofisini miaka sita anatunzwa hadi afe, halafu nesI aliyetumika miaka 45 anaambulia kiko kotoo
Maisha ni uchaguzi, Nesi angechagua kuwa Mjeda labda naye bahati ingempata
 
Umenena vyema kabisa, nchi hii tunalindwa na Mungu tu..sidhani kama dhana na malengo ya kuanzishwa JWTZ yanatekelezwa kikamilifu, ni kama JWTZ imeungana na wanasiasa kuweka matabaka kwenye Jamii ya watz..sabab hata jina tu kuitwa JWTZ ilikuwa na maana JW kuwa watetezi wa wananchi bila kujali adui anatoka nje ya mipaka ya nchi au ndani ya mipaka ya nchi, ni Bahati mbaya sana hapa kwetu..kwa sasa maadui wa wananchi wamo humu humu ndani, lkn hatujawahi kusikia JW wanatutetea dhidi ya ukandamizwaji haki na uhuru wa wananchi, demokrasia nk, JW nao wamekuwa wanafanya kazi km ya polisi..kulinda watawala, nidhamu pia imeshuka..mimi ningependa kuona JW wanasimama na wananchi 100% wasikubali hongo ya vyeo baada ya kustaafu au hata nyongeza ya mishahara kwao tofauti na watumishi wengine, ningependa kuona JW wakiweka kambi za muda sehemu zote karibu na boarder post zetu..namanga, tunduma, sirari nk hii habari ya kukamata wahabeshi na wasomali katikati ya nchi isingekuwepo tena sasa ndio imezidi..ningependa kuona JW wanakuwa na program za kuweka kambi za kutembea, mobile camping vijijini na kushiriki kazi za maendeleo kuonyesha kwa vitendo wao ni jeshi la wananchi kweli..
Ndio maana tunataka katiba mpya ili JW irudi kwa wananchi kwa vitendo..Mungu yupo ipo siku!
 
..tukiweza kubadilisha Maraisi bila vurugu.

..tukiweza kubadilisha majority bungeni bila vurugu.

..kwangu mimi hizo ndizo "LITMUS TEST" za demokrasia yetu kuwa imekomaa.

Kuwa na mapenzi na chama fulani cha kisiasa ni kitu kimoja na kuwa na mpango wa baadaye wa kugombea nafasi ya kisiasa kwa ticket ya chama hicho ni kitu kingine.

Kumzuia retired soldier au judge/magistrate kugombea nafasi ya kisiasa hakusaidii chochote. Wapo wenye mapenzi na chama fulani cha kisiasa na wako tayari kukipendelea ingawa hawana mpango wowote wa baadaye wao kugombea nafasi za kisiasa kwa ticket ya chama hicho. Kama ni shida hao bado wataendelea kuwa shida, kwa sababu ya mapenzi waliyonayo kwa chama!
 
kweli umehudumia taifa kwa kiwango Cha kutukuka nenda tu kajipumzikie huko mashambani ukalime na kufuga mifugo Ila nikikuangalia usoni nabaki natoa machozi.
 
Mkuu hata ingekuwa wewe lazima hali hiyo ikukute, unapaswa kuelewa mzazi na mlezi ni watu wawili tofauti kabisa!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…