Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo leo amefika Ikulu ya Zanzibar kwaajili ya kumuaga Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi ikiwa ni maandalizi ya kustaafu mwishoni mwa mwezi huu.
Jenerali Mabeyo 65, amelitumikia jeshi kwa miaka 42 sasa na muda wake wa utumishi unaenda ukingoni mwezi huu.
Jenerali Mabeyo amehudumu nafasi ya Mkuu wa Majeshi kwa miaka 6 sasa baada ya kuteuliwa mwaka 2016 na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, hayati John Pombe Magufuli.
Katika uongozi wake kama CDF, alishuhudia kukabidhiwa kwa madaraka kwa Rais wa kwanza mwanamke, Samia Suluhu Hassan baada ya kifo cha mtangulizi wake.
Daima utumishi wake uliotukuka utaendelea kukumbukwa ndani ya JWTZ na Nchi kwa ujumla. Nikutakie maandalizi mema ya kustaafu Jenerali Mabeyo
View attachment 2252170