Jenerali Mabeyo amuaga Rais Mwinyi. Ajiandaa kustaafu June 2022

Jenerali Mabeyo amuaga Rais Mwinyi. Ajiandaa kustaafu June 2022

Hivi Zanzibar iliwahi kutoa CDF, maana ni jambo la Muungano. Ila sio lazima atoke visiwani
 
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo leo amefika Ikulu ya Zanzibar kwaajili ya kumuaga Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi ikiwa ni maandalizi ya kustaafu mwishoni mwa mwezi huu.

Jenerali Mabeyo 65, amelitumikia jeshi kwa miaka 42 sasa na muda wake wa utumishi unaenda ukingoni mwezi huu.

Jenerali Mabeyo amehudumu nafasi ya Mkuu wa Majeshi kwa miaka 6 sasa baada ya kuteuliwa mwaka 2016 na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, hayati John Pombe Magufuli.

Katika uongozi wake kama CDF, alishuhudia kukabidhiwa kwa madaraka kwa Rais wa kwanza mwanamke, Samia Suluhu Hassan baada ya kifo cha mtangulizi wake.

Daima utumishi wake uliotukuka utaendelea kukumbukwa ndani ya JWTZ na Nchi kwa ujumla. Nikutakie maandalizi mema ya kustaafu Jenerali Mabeyo

View attachment 2252170
PUMZIKA MZEE MABEYO NCHI UMEILINDA MUNGU AKUPE MAISHA MAREFU

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Akitoka zake hapo anasubiria kupewa Uenyekiti wa bodi wa taasisi yoyote ya kiserikali,atakula mema ya nchi hadi vitukuu vyake,tunaoteseka ni sisi waswahili wa uku uswahilini,maisha ni kupanga na kuchagua
 
Mayalla, unataka military career progression ifanyike kisiasa?

History ya jeshi ambayo haina hata ten generals ni fupi sana kuifanyia desktop analysis. Unahitaji kupata composition ya jeshi by:
[emoji828]️Soldier’s URT part of origin (whether Tanganyika or Zanzibar)
[emoji828]️Soldier’s region of origin
[emoji828]️Soldier’s tribe
[emoji828]️Soldier’s religion

Let’s assume, for the sake of it, kwamba jeshi letu (linalokadiriwa kuwa na active personnel 27,000) lina askari 25,000 kutoka Tanganyika na askari 2,000 kutoka Zanzibar. Unataka pool ya askari 25,000 na pool ya askari 2,000 ziwe na equal probabilities za kuzalisha an army general? That would be pure politics!

Dimensions zingine (mkoa, kabila na dini) nazo zinakuwa affected na composition ya jeshi in a similar fashion, more or less!
 
Anakaa ofisini miaka sita anatunzwa hadi afe, halafu nesI aliyetumika miaka 45 anaambulia kiko kotoo
Ili huyo nesi aweze kufanya kazi kwa amani ni lazima alindwe na huyo mwanajeshi. Tunasahau kuwa huko mipakani kuna wanajeshi wanaosimama usiku kucha wakiwa na bunduki mkononi ili sisi huku Dar na mikoa mingine tuweze kukoroma.
 
..na kuna manesi wanaosimama usiku kucha ktk kuwauguza wenza, watoto, na wazazi, wa askari wanaolinda mipaka.

..bila manesi, askari walioko mipakani ingebidi wawe ktk hekaheka za kuuguza wapendwa wao, na wakati huohuo wabebe jukumu la kulinda mipaka.
 
Mayalla, unataka military career progression ifanyike kisiasa?

History ya jeshi ambayo haina hata ten generals ni fupi sana kuifanyia desktop analysis. Unahitaji kupata composition ya jeshi by:
[emoji828]️Soldier’s URT part of origin (whether Tanganyika or Zanzibar)
[emoji828]️Soldier’s region of origin
[emoji828]️Soldier’s tribe
[emoji828]️Soldier’s religion

Let’s assume, for the sake of it, kwamba jeshi letu (linalokadiriwa kuwa na active personnel 27,000) lina askari 25,000 kutoka Tanganyika na askari 2,000 kutoka Zanzibar. Unataka pool ya askari 25,000 na pool ya askari 2,000 ziwe na equal probabilities za kuzalisha an army general? That would be pure politics!

Dimensions zingine (mkoa, kabila na dini) nazo zinakuwa affected na composition ya jeshi in a similar fashion, more or less!
Mkuu Pulchra Animo , sio kufanya appointment ya CDF mpya kisiasa, only kufanya uteuzi with more consideration, kama watu wa upande ule pia wapo wenye kukidhi sifa na vigezo, wapewe, kwa hoja ya uwezekano, siku zote waliokuwepo ilia hawakuwahi kupewa kwa marginalisation only ambao ni ubaguzi!.

Mfano reli ya TAZARA, kwa vile ipo Tanzania, then it's statutory DG wa TAZARA, lazima atoke Zambia, Deputy ndio Mtanzania. Hivyo hata Mtanzania awe mzuri vipi, hawezi kuwa DG wa TAZARA.

The same applies to BOT, Gavana wa BOT atatoka Tanzania Bara, na deputy Governor atatoka Zanzibar, lakini kwa miaka mingi hiyo nafasi haikuwa na mtu kwa marginalisation tuu kuwa hakuna Mzanzibari mwenye sifa na vigezo, vya Ph.D ya Uchumi, hadi alipopatikana Juma Reli, kitu ambacho sii kweli. Mwaka 1999, kulikuwa ni binti mmoja wa Kizanzibari, ana Ph.D ya Uchumi alikuwa na head one of department za Citi Bank, pale New York. Kuna Mzanzibari mwingine ana Ph.D ya Uchumi, siku nyingi, ni lecture pale IFM.

Tanzania ni nchi ya JMT, kwenye nafasi za uongozi, Watanzania wa pande zote, dini zote, rangi zote au jinsia zote wapewe fursa sawa bila kubaguliwa. Hata Samia kuwa rais wa JMT, ni kwa kudra tuu za Mwenyeenzi Mungu, vinginevyo mfumo dume ungeendelea kuwabagua wanawake kuwa nchi hii bado haina mwanamke mwenye sifa na vigezo vyote vya kuwa rais wa JMT. Ubaguzi kama huu upo sekta nyingi, tuu, hivyo swali langu hili kumhusu CDF ni valid
tena now ndio more valid kwasababu soon the position of CDF will fall vacant.
P
 
..na kuna manesi wanaosimama usiku kucha ktk kuwauguza wenza, watoto, na wazazi, wa askari wanaolinda mipaka.

..bila manesi, askari walioko mipakani ingebidi wawe ktk hekaheka za kuuguza wapendwa wao, na wakati huohuo wabebe jukumu la kulinda mipaka.
Ongea hivyo ukiwa unaishi mijini, wanajeshi ndio waliopigana na maharamia waliotaka kuleta ugaidi kule Rufiji na Mkuranga wakati huo sisi wa Dar tukiwa usingizini usiku.

Naweza kukuelewa unapoongea hivi kwani ni nchi yenye amani na siku zote kuna rabsha ndogo ndogo tu.
 
..ongea hivyo ukiwa hujaugua au kuuguliwa.

..pia mbona magaidi waliokuwa wakiteka na kutesa wapinzani walikuwa hawakamatwi wakati tuna jeshi linalojitambua?

..pia ilikuwaje magaidi wakaingia ktk eneo la serikali na kujaribu kumuua mbunge huku tukidai tuna jeshi imara?

..kwanini kulitokea mlipuko wa bomu ktk ofisi za mwanasheria mwanaharakati karibu kabisa na makao makuu ya jeshi na wahusika hawakukamatwa?

NB.

..unakumbuka sakata la gesi Mtwara na mikoa ya kusini? Unakumbuka vikosi gani vilishiriki kupiga na kuumiza wananchi wale?

..magaidi wa mkiru tunawalaani vikali na kwa nguvu zote. lakini tukiwa wakweli tutabaini kwamba ni matokeo ya utawala mbaya na sera mbovu za Ccm kwa mikoa ya kusini.
 
..ongea hivyo ukiwa hujaugua au kuuguliwa.

..pia mbona magaidi waliokuwa wakiteka na kutesa wapinzani walikuwa hawakamatwi wakati tuna jeshi linalojitambua?

..pia ilikuwaje magaidi wakaingia ktk eneo la serikali na kujaribu kumuua mbunge huku tukidai tuna jeshi imara?

..kwanini kulitokea mlipuko wa bomu ktk ofisi za mwanasheria mwanaharakati karibu kabisa na makao makuu ya jeshi na wahusika hawakukamatwa?

.
Suala la mbunge ni moja tu na hakuna mwenye uhakika hizo CCTV cameras kama kweli ziliondolewa, ni suala lenye siasa nyingi.

Wanajeshi wanalinda nchi hii miaka na miaka, kazi yao ni ngumu ingawa kwetu inaonekana ni nyepesi.
 
..magaidi wameingia eneo la serikali wakajaribu kuua mbunge. Na wameondoka bila kuguswa.

..magaidi wamelipua ofisi za mwanasheria karibu na makao makuu ya jeshi. Na hawakukabiliwa na askari yeyote.

..tungekuwa na jeshi imara hayo yasingetokea.

..nchi hii inalindwa na MUNGU.
 
Back
Top Bottom