Jenerali Mabeyo amuaga Rais Mwinyi. Ajiandaa kustaafu June 2022

Jenerali Mabeyo amuaga Rais Mwinyi. Ajiandaa kustaafu June 2022

Asante kwa utumishi wako.

Na kila la heri katika mambo yako Mengine.
 
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo leo amefika Ikulu ya Zanzibar kwaajili ya kumuaga Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi ikiwa ni maandalizi ya kustaafu mwishoni mwa mwezi huu.

Jenerali Mabeyo 65, amelitumikia jeshi kwa miaka 42 sasa na muda wake wa utumishi unaenda ukingoni mwezi huu.

Jenerali Mabeyo amehudumu nafasi ya Mkuu wa Majeshi kwa miaka 6 sasa baada ya kuteuliwa mwaka 2016 na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, hayati John Pombe Magufuli.

Katika uongozi wake kama CDF, alishuhudia kukabidhiwa kwa madaraka kwa Rais wa kwanza mwanamke, Samia Suluhu Hassan baada ya kifo cha mtangulizi wake.

Daima utumishi wake uliotukuka utaendelea kukumbukwa ndani ya JWTZ na Nchi kwa ujumla. Nikutakie maandalizi mema ya kustaafu Jenerali Mabeyo

Jenerali Mabeyo unaondoka ila umetuachia Rais wa Ajabu ambaye hajawahi kuonekana​

 
Tunamshukuru kwa utumishi wake uliotukuka na kudumisha nidhamu ya Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ..
 

Jenerali Mabeyo ikiwezekana malizia utumishi wako na Huyo mama amalize Muda wake.​

 
Moja ya Wakuu wa jeshi niliyetokea kumu 'admaya' sana. CDF Mabeyo tutakuheshimu na kukuenzi daima kwa mchango wako katika jeshi,kanisa,jamii na taifa kiujumla.Vitabu vyako ulivyoandika ni kumbukumbu njema sana.Salute Soldier [emoji870]
Naomba vitabu vyake nivione
 
Mteuwaji asisahau kuwa Wakristo ( tena wa Katoliki ) ndiyo huwa CDF ( japo katika Madhehebu mengine ) anaweza Kuokoteza okoteza lakini asiwekwe hapo wa Dini yake Mteuwaji.

Najua kuna mtakaonishangaa na Kunishambulia ila GENTAMYCINE nasisitiza ni lazima CDF aje ( kwa sababu ambazo ni za Ndani kabisa ) awe ni Mkristo kutoka Dhehebu lenye Nguvu na Ushawishi Tanzania na Duniani la Katoliki.

Ukikereka na nilichokiandika Koroga Sumu ya Panya unywe na Ukishainywa jipige Kofi la Kutukuka na jiite Popoma.
Mkuu GENTAMYCINE hujawahi kukwama na comment zako za kiwaki [emoji28][emoji28][emoji706][emoji706][emoji706]
 
Thank you for your service General

Ukaongeze muda wa ibada na kutubu pia kucheza na wajukuu sasa, sio kuanza kukuona majukwaani kuangaika kugombea nafasi za kisiasa
 
Back
Top Bottom