Kama ni kweli Muhoozi kasema hivyo msiwe na Hofu kwani Mwezi Mmoja uliopita Rais Museveni ( Baba yake Mzazi ) aliwaita Marafiki zake Wawili ( Wazee Wawili wa Kitanzania ) sasa ni Wastaafu ila walikuwa wakihidimu Taasisi ya Ikulu na Nyeti Awamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na katika Mazungumzo yao Mzee ( Rais ) Museveni aliwaomba Wazee hawa Wamuite Muhoozi huku Tanzania waongee nae na Wamkanye juu ya haya ayafanyo kwani hata Baba yake ( Rais ) Museveni yanamkwaza pia.
Kuhusu huyu Mtoto wa Rais Museveni aitwae Muhoozi Kainerugaba kutaka au kutamani kuja kuwa Rais wa Uganda GENTAMYCINE nawahakikishia kuwa hatokuja kuwa Rais kwani Baba yake halitaki hilo na anasema Uganda si Himaya ya Kifalme bali ni Taifa linaloheshimu Utu na Misingi Kisiasa na Kidemokrasia.
Mmoja wa hawa Wazee Wawili ( ambao ni Marafiki wakubwa na wa karibu na Rais Museveni waliolelewa vyema na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na hata Muhoozi anawajua kwani walimlea pamoja na Dada yake Natasha walipokuwa wakiishi Upanga Ghorofani jirani na Muhimbil Hospital ) anategemea kwenda nchini Uganda ambapo licha ya kuonana na Rais Museveni ila pia ana appointment ya Kukutana na huyu Kijana Mtoto wa Rais Muhoozi ili kwa Niaba ya Mzee Mwenzake atakayemuacha Dar es Salaam ( Tanzania ) ampe 'Vipande' vyake hivyo huenda akaanza Kubadilika.
Hata hivyo pamoja na Rais Museveni ( Baba yake Mzazi ) leo Kukerwa na akifanyacho Mwanae Muhoozi MImi kama GENTAMYCINE nampa lawana nyingi Rais Museveni hasa kwa Kumpandisha Vyeo vya Kijeshi haraka haraka, kumpa Madaraka hasa Kikosi chake cha Ulinzi SFC ( zamani PPU ), kumruhusu aunde Jeshi lake binafsi la Kumtii ( ndani ya Jeshi Mama ) la UPDF na hivi karibuni Kumteua kama Mkuu wa Kikosi cha Ardhini.
Vitu vyote hivi Rais Museveni alivyomfanyia Mwanae huyu ( Muhoozi ) automatically vilimpa Jeuri na Kiburi Mwanae kiasi cha kuona na kudhani kuwa baada ya Baba yake Mzazi ( Rais Museveni ) Kung'atuka Madarakani anayefaa kuwa Rais ajaye wa Uganda ni Yeye tu Muhoozi.
Nina mengi juu ya hili, hawa ( Rais Museveni na Mwanae Muhoozi) nchi ya Uganda, Siasa zake, machache ila ya Muhimu kuhusuTaasisi zake za UPDF na ile ya CMI na kinachotokea sasa, ila kwa sasa naomba niishie tu hapa tafadhali.