TANZIA Jenerali Tumainiel Kiwelu afariki Dunia, kuzikwa Mbezi Loius Dar

Kuna nyingine ya Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ( Poti wangu kabisa kutoka Mkoani Mara ) Jenerali George Mwita Waitara ila kwa leo naomba nisitiririke wala kuserereka nayo Kwanza.
 
Huyu Tumainieli kiwelu ndie aliyekua mkuu wa mkoa wa Iringa aliyemuua Mwamwindi?
Kha, mkuu umepuyanga Sana. Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Iringa aliuawa na siyo alimuua Mwamwindi. Mwamwindi alipomuua mkuu wa mkoa Dr. Kleruu alishtakiwa na kupatikana na hatia a kahukumiwa kifo na akanyongwa.Hivyo wahusika wa tukio hilo wote walishakuwa Kama mwendazake toka miaka hiyo ya 70.
 
Nimekuwa naona majina mengi ya uchagani na upareni yana eithaer anzia na el au kumalizikia na el je eli katika majina hayo humaanisha nini
Tumainiel
Eliatosha
Sifael
Happiel
Elbariki
Eliona
Elikunda
Baniel
 
Nimekuwa naona majina mengi ya uchagani na upareni yana eithaer anzia na el au kumalizikia na el je eli katika majina hayo humaanisha nini
Tumainiel
Eliatosha
Sifael
Happiel
Elbariki
Eliona
Elikunda
Baniel
Eli = mungu wa kimila
 
RIP Jenerali Kiwelu, utumishi wako ulikuwa uliotukuka. Umepigana vita iliyo njema, imani umeilinda.
 
Pumzika kwa amani kamanda, wewe na Luteni Generali Silas Mayunga (Mti Mkavu) mnakukukwa sana na watanzania hasa hasa kwenye ile vita ya Kagera ya kumtokomeza / Kumchakaza nduli Iddi Amini dada. Vikosi vyenu mlivyokuwa mkiviongoza vilifanya maajabu makubwa!!
 
Mwinyi Kweli anatakiwa a Edit hicho kitabbu chake

Kabla kwenda kumkabili Raisi hakuwa peke yake walienda kwenye landrover na viongozi wengine wa juu JESHINI ila kiongozi akiwa yeye KIWELU na walienda sababu ya hasira waliyokuwa nayo

Walimwita waziri wa Fedha wakati huo Profesa Kighoma Malima awaeleze sababu ya mishahara kuchelewa na maslahi duni Jeshini ,wakati huo ukusanyaji kodi ulikuwa chini mifisadi ilikuwa kibao serikali ilkuwa hela haina!!

Profesa Malima ,Profesa wa uchumi akaanza kusema ngoja niwaeleweshe kichumi tatizo liko wapi tatizo kodi ndogo!!! Kiwelu akasimama akasema wewe karani wa wizara ya fedha kamwambie bosi wako atuachie nchi atupe masaa hata matatu tu tutakusanya kodi .UMESIKIA WEWE KIKARANI CHA WIZARA YA FEDHA

Profesa Malima akakimbia anahema akamwambia Mwinyi wanataka kupindua nchi.Hawajakaa muda KIWELU AKAINGIA IKULU NA TEAM YAKE WANA MIHASIRA KIBAO WAKAONGEA wakamaliza

Walipotoka mishahara ikapanda na maslahi kuboreshwa na kila askari mwenye kuanzia nyota wakakopeshwa magari ya kutembelea pick up kwa bei nafuu na wakaanzishiwa maduka yao ya kununua vitu ambayo ni duty free hayana kodi .Magufuli ndiye alikuja kuyafunga baada ya kuona yanatumika kama uchochoro wa kukwepa kodi vitu vinaenda kwenye hayo maduka halafu vinashushwa maduka binafsi

Baada ya sakata lile Mwinyi alimuondoa uwaziri wa Fedha Profesa Kigoma Malima na kumuweka Jakaya KIkwete mwanajeshi mwenzao kuwa waziri wa fedha!!! mambo yakatulia
 
Juma Nkangaa ndie juma ikangaa au?
Acha ubwege wewe, mwenyewe katika maandishi yako umetofautisha halafu unauliza swali? nakusalimu kwa jina la jamuhuri ya muungano wa Tanzania, itikiaaaaa.
 
Huyu mzee kwanini wanamzika Dar? kwa nini asipelekwe kwao Moshi? Maana serikali inaweza kugharimia.

Anyway, maybe ni wish yake azikwe Dar. But I find it strange.

Nafsi yake ipumzike alipoandaliwa na mola wake.
 

Pole sana Ndugu,jamaa na marafiki pamoja na jeshi la wananchi kwa kupoteza mtu mashuhuri nchini.
 
Huyu Tumainieli Kiwelu ndie aliyekua mkuu wa mkoa wa Iringa aliyemuua Mwamwindi?
Soma hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…