TANZIA Jenerali Tumainiel Kiwelu afariki Dunia, kuzikwa Mbezi Loius Dar

Katika wanajeshi waliondolewa jeshini miaka hiyo na kupewa vyeo vya kisiasa ni huyu, kwanza alikiwa anakubarika sana jeshini, halafu alikuwa mtata. Kama si mazengwe huyu angekuja kuwa mkuu wa majeshi
 
Poleni sana wanafamilia, JWTZ na Watanzania kumpoteza Gen. Kiwelu.
Naomba kukumbushwa, mpaka anastaafu ukuu wa mkoa wa Kagera, mtajwa alikuwa na rank ya Maj. Gen. (Mstaafu); ni lini alipandishwa rank na kuwa full Gen. mwenye kumbukumbu naomba mnitujuze.
Maombi na sala zangu faraja ya Mungu alie juu na iwe juu ya wote ambao smiba huu unatuhusu.
Bwana haya mambo ya Kijeshi hata sijui yanakwendaje kama umestaafu lkn najua bado kuna Jenerali Sarakikya na ana nguvu tu na ndio waliokuwa wamebaki na Jeneral Tumainieli Kiwelu na wana NYOTA 4
4 star general ambaye hakuwahi kuwa Mkuu wa Majeshi!
All in all utumishi wake jeshini ulitukuka!
 
Huyu Tumainieli kiwelu ndie aliyekua mkuu wa mkoa wa Iringa aliyemuua Mwamwindi?
Acha kuchanga habari Kiwelu hajawahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa na ni Mwamwindi ndiye Aliyemuua Mkuu wa Mkoa Wilbert Kleruu ndio Alikuwa mkuu wa Mkoa wa Iringa
 
Jenerali Tumainiel Kiwelu amefariki tarehe 18 Mei 2021 na atazikwa shambani kwake Mbezi Luis Dar es salaam tarehe 22 May 2021

Bwana ametoa Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe.

View attachment 1792046

View attachment 1792059
Mungu Ampe Pumziko la Milele Nilimfahamu akiwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na Ndiye Aliyeujenga UWANJA WA NELSON MANDELA SUMBAWANGA
 
Jenerali Tumainiel Kiwelu amefariki tarehe 18 Mei 2021 na atazikwa shambani kwake Mbezi Luis Dar es salaam tarehe 22 May 2021

Bwana ametoa Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe.

View attachment 1792046

View attachment 1792059
Huenda kidogo sasa Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi akapumua ( na nashangaa katika Kitabu chake hajazungumzia Mkwara aliopigwa na Marehemu ) wakati alipokuwa Rais wa Tanzania 1985 hadi 1995 kwani Marehemu alikuwa ni Shupavu, Makini, Asiyeogopa kama Haki na Sheria vyote viko upande wake na mwenye Kujiamini kama ilivyo Sifa Mama ya Mwanamedani ( Mwanajeshi ) yoyote yule duniani.

Ni kwamba Kipindi hicho cha Awamu ya Pili ( ya Rais Mwinyi ) Mishahara kwa Wanajeshi ilikuwa inachelewa sana Kulipwa hadi kupelekea Wanajeshi kuanza ' Kujisevia ' Bidhaa Madukani kwa Ubabe na wengine hata Kujiingiza katika Uratibu wa Uhalifu ili tu waweze Kujikimu.

Hali ilipozidi kuwa mbaya ( na hapa naiongelea 1985 hadi 1995 ) Marehemu huyu Afande Kiwelu alienda moja kwa moja kuonana na Rais Mwinyi ambapo alimweleza kuwa anampa Masaa machache tu awe ameshawalipa Mishahara yao Wanajeshi vinginevyo ' wanamtimbia ' mazima mazima pale Ikulu hali iliyomfanya Rais Mwinyi ' aufyate ' na Kuwatafutia Mishahara yao alikokujua na kuwapa mara moja ambapo Heshima ya Marehemu ndani ya Jeshi ( JWTZ ) iliongezeka maradufu na kuwa Mmoja wa Makamanda waliopendwa zaidi na Wanajeshi Kipindi chake cha Utendaji.

Na ni Juhudi hizi hizi za Marehemu Afande Kiwelu ndiyo zilisababisha tokea Siku hiyo Awamu zote za Marais mpaka sasa ( leo ) watacheza na Mishahara ya Kada zingine zote kwa Kuwacheleweshea ila siyo kwa Wanajeshi ( JWTZ ) na nahisi Rais Mstaafu Mzee Mwinyi alihakikisha kila Rais anayechukuwa nchi basi anapewa Angalizo hilo ndiyo maana tokea Awamu yake hadi sasa sijasikia Upuuzi huo ukijitokeza tena.

Mwambieni Rais Mstaafu Mzee Mwinyi akifanyie ' editing ' Kitabu chake alichokizindua hivi karibuni na aliweke hili Tukio kwani lina Umuhimu sana kwa Watu kujua na wale ambao Kipindi hicho mlikuwa bado katika Zipu za Baba zenu na wale walioko pia Zipuni kwa sasa ili wakizaliwa wakutane nayo.

Kwani ni Jambo ( Tukio ) ambalo lilitokea ( lilimtokea ) Mzee wa Watu achilia mbali na lile la ' Kuwambwa ' Kwake Makofi akiwahutubia Waislamu alipowagusia Kutumia Condoms pale Wakitiana ( Wakitinduana ) ili Kujiepusha na Maambukizi ya UKIMWI ambao miaka hiyo ulikuwa umepamba sana Moto na ' Unawafyeka ' mno Watanzania.
 
Makamanda wa vita ya Kagela hawa RIP Mzee Kihwelu
 
Sasa naelewa kwa nini alikuja kuondolewa jeshini wakaona heri wampe vyeo vya kisiasa ili ajifunze nidhamu ya kiraia pia.

Rais ni Jemedari Mkuu unapaswa kumtii hata alipokuwa anadai mishahara alipaswa kutumia busara kama sio nidhamu ya juu ya kijeshi sio kumtishia Rais.

Hii kwa watu waliowahi kupitia majeshi watakubaliana kwamba ilibidi kumtoa pale maana siku nyingine atakuwa na madai mengine atakosa nidhamu kwa kiongozi then ikageuka ugaini, tena ana bahati Mwinyi alikuwa mtu poa Yani angekuwa Nyerere angemtandika kesi ya uhaini . Rais hatishiwi hata kama unahisi unaweza kufanya hayo.

Naelewa ndio maana walimpandisha vyeo baada ya kustaafu kigoma alikokuwa Major General then mpaka full four star General amebaki na sarakikya nae alipigwa Pini sababu hizi hizi.

Huwezi kuwa kiongozi halafu unaendeshwa na askari wa chini kiasi unamkosea heshima mkuu wa nchi.

By the way alikuwa shupavu sana rip to the best General who never became a general 🤷
 
..R.I.P Tumainieli Kiwelu.

..Watz watakukumbuka jinsi ulivyoongoza kwa ushupavu na weledi mkubwa OPERATION CHAKAZA.

..Umeacha rekodi ya kuwa Mtanzania pekee aliyeaminiwa kutumikia ktk nafasi ya Mnadhimu Mkuu wa JWTZ mara mbili.

NB.

..Operation Chakaza ndio mapigano yaliyoyaondoa majeshi ya uvamizi ya Uganda toka ktk ardhi ya Tanzania.
 
Poleni sana wanafamilia, JWTZ na Watanzania kumpoteza Gen. Kiwelu.

Naomba kukumbushwa, mpaka anastaafu ukuu wa mkoa wa Kagera, mtajwa alikuwa na rank ya Maj. Gen. (Mstaafu); ni lini alipandishwa rank na kuwa full Gen. mwenye kumbukumbu naomba mnitujuze.

Maombi na sala zangu faraja ya Mungu alie juu na iwe juu ya wote ambao smiba huu unatuhusu.

..alipandishwa cheo toka Brigadier kuwa Major General wakati wa vita vya Kagera.

..baada ya vita vya Kagera aliteuliwa na Rais Nyerere kuwa Mkuu wa mkoa wa Tanga, akahamishiwa Rukwa, na baadae Tabora.

..alipandishwa kuwa Lieutenant General na kuteuliwa na Raisi Mwinyi kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jwtz.

..Raisi Mkapa alimpandisha cheo kuwa General na kumteua kuwa Balozi wa Tanzania Ufaransa.

..Baadae uteuzi wa kwenda ubalozini ukabadilishwa na General Kiwelu akateuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
 
Jenerali Tumainiel Kiwelu amefariki tarehe 18 Mei 2021 na atazikwa shambani kwake Mbezi Luis Dar es salaam tarehe 22 May 2021

Bwana ametoa Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe.

View attachment 1792046

View attachment 1792059
R.I.p dingi, huyu dingi alitujengea uwanja wa Nelson Mandela hapa swax miaka hiyo ,tukampa na mtaa KWA jina lake kabisa (mtaa wa kiwelu) upo mpaka leo, pumzika salama mzazi.
 
Back
Top Bottom