butron
JF-Expert Member
- Jun 3, 2013
- 5,640
- 7,943
Huu ujinga wa kukijua chama badala ya kuijua serikali na nchi na matatizo ya Wananchi ndiyo mzizi wa umasikini ulipo.Kwani wanaokijua chama wametusaidia nini?Viongozi wetu wanapatikanaje?
Na tunapimaje uwezo wao wa kuongoza? Je tuna mfumo wa kuwatengeneza? Job Description ya Kuwa Rais, Waziri Mkuu, Spika kwa Tanzania inataka vitu gani?
Nimekumbuka hayo kutoka kwa hawa Nguli wawili. Mwaka 2015 baada ya vikao vya CCM DODOMA, Prof na Mwalimu wangu, Prof Mwandoshya alikuja na mshangao kwa CCM na Vikao vyake "kwanini tumemchagua mtu ambaye haijui CCM, hajawahi hata kuwa mjumbe wa kamati ya Siasa ya Tawi" kauli hii ilimtia matatani sana, akaamua kutumia muda mwingi nyumbani kwake Matema Beach Kyela ili pia Kujilinda. Yaliyofuatia wana CCM Wanayajua.
Mwaka 2021 baada ya kifo cha Hayati Magufuli akashika kijiti Mama Samia. Akaibuka Nguli Mwingine, Jenerali Ulimwengu, akamwambia Mama "Kaa kwa kutulia, Tanzania huijui" alimshauri Mama kupata wasaa kuijua Tanzania. Wakati ule sikumwelewa vema Jenerali, lkn sasa naanza kumwelewa.
Hawa watu wawili Prof. Mwandosha na Jenerali Ulimwengu ni watanzania wanaoijua nchi. Kauli zao zinaonesha chngamoto kubwa ya kuwapata viomgozi wetu.
Je, hawa wanaotuongoza wanajua wanakotupeleka?
Kenya waliweka kando KANU na wanasonga sisi bado tunaabudu CCM!
Huyo Mwandosya Barabara ya kutoka Tukuyu kwenda kwao haina lami toka tupate Uhuru, kashindwa ata na Mwakyembe kwao Kyela lami kibao na ukumbuke Mwakyembe na yeye hakijui chama pia.
Tukatae utapeli wa CCM,nadhani kamati ya Bashiru ilifichua ubadhirifu wa Mali za chama,Je hao wanaokijua chama walikuwa wanajua kuwa Mali za chama zinatafunwa na wachache?Ni Magufuli asiyekijua chama ndiyo alikuja kuwafungua macho Wana CCM;sasa mtu ambaye hajui chama alijuaje kuwa chama kina Mali!