Jenerali Ulimwengu: Hakukuwa na Uchaguzi huru na haki

Jenerali Ulimwengu: Hakukuwa na Uchaguzi huru na haki

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
17,047
Reaction score
63,206
Akihojiwa na kituo cha habari cha Sauti ya Ujerumani, Jenerali ulimwengu amesema kuwa zoezi la uchaguzi mkuu halikuwa huru na haki na kwamba tangu mchakato wa upinzani uanze, wapinzani walitendewa mambo ambayo kimsingi ukiyaangalia siyo fair kabisa.

Jenerali amekumbushia kauli ya Magufuli akiwaeleza watu wenye dhamana ya usimamia uchaguzi (wakurugenzi) kuwa haiwezekani yeye awape kazi awalipe mishahara mizuri halafu watangaze wapinzani kuwa wameshinda.

Pia, amekumbushia kauli ya Samia Suluhu aliyoitoa kwenye kampeni kuwaambia wananchi kuwa wananchi kuwapa kura au kutowapa kura wao bado wataunda serikali.

Jenerali amesema kuwa mawakala wa vyama vya upinzani walio wengi waliondolewa vituoni na pia maeneo kadhaa nchini zilionekana kura feki.

Jenerali amesema Chama cha Mapinduzi kufurahia ushindi wa aina hii ni kujidanganya tu kwa sababu mchakato mzima wa uchaguzi huo siyo fair.

Kwa maelezo zaidi msikilize Jenerali Ulimwengu yeye mwenyewe hapa.
 

Attachments

Toka alivyofurumshwa na Mkapa huyu mh ana hasira na uongozi wa nchi hii. Yeye kwake kila kiongozi wa serikali ni mbaya kuanzia Mkapa, Lowassa, JPM na yeye kama alivyo Mbeligiji mweusi kila kitu anakijua yeye, huyu ndio aligoma kuachia madaraka ya katibu mkuu wa vijana wa Afrika kule Algiers alitakiwa amwachie Prof Kabudi. Ulimwengu ni mtu wa figisu sawa na wale makomandoo wa klabu za Simba na Yanga. Ni mbinafsi mno.
 
Hapo zamani akiwa kijana na njama zao akijidai mwanamapinduzi na mfuasi mkubwa wa itikadi ya ujamaa na kujitegemea hivi leo kila akifungua mdomo kwenye vyombo vya nchi za kibeberu ni kukandia tu chama na nchi iliyomlea.
 
Siku ya kufunga kampeni pale Kawe,Mnyika aliwaambia kwamba ikitokea wakala akatolewa nje mhakikishe hicho kituo kura hazipigwi.

Hivi ilikuwaje mawakala wakawa wanatolewa tu kama kuku na nyie wafuasi mna mangamanga tu?

BTW: Hata chaguzi zilizopita ambazo waangalizi wote (EU,EAC,AU,SADC etc) walisema uchaguzi ulikuwa huru na haki mliyakataa matokeo kwa hiyo hii wala siyo habari.
 
Siku ya kufunga kampeni pale Kawe,Mnyika aliwaambia kwamba ikitokea wakala akatolewa nje mhakikishe hicho kituo kura hazipigwi.

Hivi ilikuwaje mawakala wakawa wanatolewa tu kama kuku na nyie wafuasi mna mangamanga tu?

BTW:Hata chaguzi zilizopita ambazo waangalizi wote (EU,EAC,AU,SADC etc) walisema uchaguzi ulikuwa huru na haki mliyakataa matokeo kwa hiyo hii wala siyo habari.
Uchafuzi wa safari hii ulipita kipimo.
 
Jenerali ananyoosha mulemule, sawa na Lissu, Fatma Karume, Maria Tsehai Sarungi wote hawaogopi.

Hapo angekuwa Pascal angekariri kauli ya uchaguzi umeisha na pongezi za ushindi wa 84% hata kama makaratasi ya kura yalisambaa kitaani yakifungia kitumbua.
 
Back
Top Bottom