Jenerali Ulimwengu: Hakukuwa na Uchaguzi huru na haki

Nimeanza kufuatilia vyema uchaguzi wa vyama vingi muhula wa mwisho wa Mkapa hivyo najua ninachosema. Hakuna gazeti lililokuwa huru kuandika habari hasi hata kama zina ukweli wa kiasi gani. Hizo kura fake tumeziona kwa macho yetu, na ni bora zilichomwa maana bado zingeingizwa kwenye majumuisho ya kura. Vyombo vya dola vilikuwa sehemu ya huo wizi, ulitarajia wapewe ushahidi ili waufanyie nini? Hilo la kutolewa, au kucheleweshwa kwa mawakala tumeliona kwa macho yetu, na wengine walihojiwa kwenye vituo kadhaa vya televisheni. Hao waangalizi wengi wa uchaguzi tunajua walipewa vibali katika mazingira gani, hivyo hata kabla ya ripoti zao kutoka zilikuwa predictable. Unapoona 2/3 ya wapiga kura hawataki kujitokeza kupiga kura, ujue watu wameshaona upigaji kura ni upuuzi kama upuuzi mwingine.
Hilo la kuchoma kura ni la uongo kabisa...hizo zinazodaiwa kura fake mliziandaa nyie chadema na wewe chadema ukaziona mlizoziandaa wenyewe na mkazichoma Moto baada ya kufanya stage ya kupiga video za uzushi...Hilo la waangalizi wa uchaguzi itoshe tu kusema ripoti za waangalizi ziliona utoto wa upinzani...kuhusu mawakala chadema na vyama vingine vyote vya upinzani hazikuwa na resources kuweka mawakala kwenye vituo vyote...hamkuwa na fedha kuwalipa mawakala wenu...wakala hawezi kukaa kwenye kituo bila hata maji kuanzia saa kumi na moja alfajiri mpaka usiku wa manane...kwa hili chadema wakaja na utoto kuwa eti mawakala wamefukuzwa...nimewahi kuhusika na uchaguzi miaka ya nyuma mawakala wa vyama vya upinzani wanaleta huruma Sana kwani ni wachache tu ambao hulipwa...kuhusu low voter turnout hili ni tatizo la dunia nzima...uchaguzi wa 2010 kwa mfano waliojitokeza kupiga kura walikuwa below 50 per cent...nilihusika katika utafiti kufahamu sababu za low voter turnout...sababu hizo siwezi kuziweka happy...

Kwenye uchaguzi huu wa 2020 chadema ilishindwa fair and square ..hakuna wa kulaumu Bali wao wenyewe chadema...kumleta kibaraka Lissu kuwa mgombea kwa tiketi ya Chadema lilikuwa ni kosa kubwa la kimkakati...ndiyo maana baadhi tulisema kuwa kwa kosa Hilo chadema isingeweza kupata hata viti kumi vya ubunge au asilimia hata 20 ya kura za urais...watanzania hawapendi ukoloni na ubeberu..Lissu alikuwa anapigiwa debe na mabeberu kwa hiyo likamkosesha kura nyingi..kwenye kampeni yeye Lissu akawa anamtaja Magufuli muda mwingi huku Magufuli kwa mkakati ulioandaliwa akawa hamtaji kwa jina huyo kibaraka..
 
Jenerali uko vizuri Mungu akubariki!!!!
Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu(kwa sauti ya jiwe)
 
Watu walipeleka Polisi ushahidi wa kura walizozikamata, Polisi wakawajibu kuwa hawahusiki na mambo ya uchaguzi (Jacob Boniface alipeleka mzigo wa kura Polisi wakakataa kufile kosa). Sasa kama Polisi nao waligoma kudeal na matatizo ya uchaguzi ulitaka watu wayapeleke wapi?-It seems system nzima ilishiriki kuhujumu uchaguzi huu kwa manufaa ya Mtu mmoja na genge lake (CCM).

Kuhusu waangalizi kuona kasoro za Uchaguzi, inaelekea wewe hujawasikiliza waangalizi wa Tanzania Election watch , wameelezea waziwazi kuhusu kura kukutwa kwenye masanduku kabla ya kura kupigwa

Lakini pamoja na hayo Waangalizi hawakwenda vituo vinavyofikia 100 nchi nzima wakati kulikuwa na vituo vya kura zaidi ya 80000 nchi nzima, zaidi ya vituo 70000, mawakala wa wapinzani hawakuruhusiwa, waliruhusiwa vituo visivyofika 20000. Kituo nilichopigia mimi Wakala wa Chadema hakuruhusiwa kuingia katakata, na tulikuwa naye nje yeye akijaribu kuingia anakataliwa, sisi tukiwa kwenye msitari kusubiri kupiga kura!

Kuhusu kukamatwa mabegi ya kura ni kweli zilikamatwa na video zipo, nyingine zilikamatwa mbele ya maaskari lakini ni jukumu lako tu kujiuliza hata baada ya maaskari kuzikamata shauri liliishia wapi!

Naona mpo kwenye denial lakini hakukuwa na uchaguzi pale!
Duh...kazi ipo...huyo Boniface una maana yule meya bondia aliyemdunda mwandishi wa habari kwenye uchaguzi wa 2015? Ni Nani atamwamini yule hupendelea kuvaa magwanda Kama ya mpigania Uhuru? Tanzania Election Watch? Nilikuwa naiangalia Sana..ilijaa Wakenya went chuki na nchi hii...kile kimama chenye umri mkbwa nilikuwa siku zote kinasoma tu ripoti iliyoandaliwa...wale walikywa ni paid agents na mabeberu...
 
Unaona usivyo na hoja sasa, Nguo zinahusiana nini na kuripoti jinai polisi
Yule mama Jaji, Ni Mganda na siyo Mkenya
Hii inaonyesha unaongea bila facts
 
Hilo la kuchoma kura ni la uongo kabisa...hizo zinazodaiwa kura fake mliziandaa nyie chadema na wewe chadema ukaziona mlizoziandaa wenyewe na mkazichoma Moto baada ya kufanya stage ya kupiga video za uzushi...Hilo la waangalizi wa uchaguzi itoshe tu kusema ripoti za waangalizi ziliona utoto wa upinzani...kuhusu mawakala chadema na vyama vingine vyote vya upinzani hazikuwa na resources kuweka mawakala kwenye vituo vyote...hamkuwa na fedha kuwalipa mawakala wenu...wakala hawezi kukaa kwenye kituo bila hata maji kuanzia saa kumi na moja alfajiri mpaka usiku wa manane...kwa hili chadema wakaja na utoto kuwa eti mawakala wamefukuzwa...nimewahi kuhusika na uchaguzi miaka ya nyuma mawakala wa vyama vya upinzani wanaleta huruma Sana kwani ni wachache tu ambao hulipwa...kuhusu low voter turnout hili ni tatizo la dunia nzima...uchaguzi wa 2010 kwa mfano waliojitokeza kupiga kura walikuwa below 50 per cent...nilihusika katika utafiti kufahamu sababu za low voter turnout...sababu hizo siwezi kuziweka happy...

Kwenye uchaguzi huu wa 2020 chadema ilishindwa fair and square ..hakuna wa kulaumu Bali wao wenyewe chadema...kumleta kibaraka Lissu kuwa mgombea kwa tiketi ya Chadema lilikuwa ni kosa kubwa la kimkakati...ndiyo maana baadhi tulisema kuwa kwa kosa Hilo chadema isingeweza kupata hata viti kumi vya ubunge au asilimia hata 20 ya kura za urais...watanzania hawapendi ukoloni na ubeberu..Lissu alikuwa anapigiwa debe na mabeberu kwa hiyo likamkosesha kura nyingi..kwenye kampeni yeye Lissu akawa anamtaja Magufuli muda mwingi huku Magufuli kwa mkakati ulioandaliwa akawa hamtaji kwa jina huyo kibaraka..

Hilo la kufukuzwa kwa wakala nina ushahidi nalo wala sizui. Kura fake zilikuwa kila mahali, mbona polisi hawakuzikamata kama wanavyokamataga bangi au bidhaa zozote haramu? Kama hizo kura zilikuwa ni za cdm, kwanini polisi hawakumtia yoyote hatiani kwa hizo kura fake, ili uchaguzi usiingie doa?

Usihusishe uchaguzi huu na zilizopita, maana hizo zilizopita walikuwa na mawakala kila sehemu walipokuwa na mgombea. Huu mchezo wa kuanza kuhujumu mawakala, na kunajisi uchaguzi waziwazi bila hofu umeanza baada ya Magu kuwa rais, sio kwamba huko nyuma ilikuwa hakuna wizi, ila safari hii ni zaidi ya wizi. Chaguzi zote zilizopita hatukuwahi kuona wagombea wa upinzani kuenguliwa kwa wingi kama sasa kutokana na mizengwe ya wazi. Hizo sababu za watu kutokijotekeza kupiga kura ni kukosa imani na box la kura. Hizo nyingine unazoficha ni mbwembwe tu.

Eti watanzania hawana imani na mabeberu, hizo propaganda mfu za ccm ndio unazitumia kujenga hoja hapa? Nchi hii imejaa miradi kibao ya wazungu, mbona hao watanzania wasiigomee ili hiyo propaganda mfu ipate uhalali? Deni kubwa la nchi hii ni la hao hao wazungu, limetoka wapi kama watanzania hawana imani na mabeberu? Hao watanzania unaosema wanawachukia mabeberu, si ndio hao kuanzia rais, waziri, mbunge, mtendaji wa mtaa, mpaka raia wa kawaida anaona fahari kupiga picha na mzungu? Nenda leo kijijini huko kwenye hao unaosema ni watanzania, kisha uwe na mzungu uone wanavyomtetemekea na kumuorodhoshea matatizo yao ili awatatulie. Hizo propaganda mfu za mabepari kawapelekee wenye upeo mdogo boss.
 
Hilo la bidhaa za wazungu tunazitumia eti huku tukiwaambia kuwa ni mabeberu tulilisikia pia kwa kibaraka Lissu wakati wa kampeni....dah...siwezi kuendelea na debate hi kwa kuwa it is turning into a secondary school debate rather than a debate of serious and learned people..
Yaani ni sawa na debate ya village life is better than town life...
 
Hamna anayekulazimisha kuendelea na mjadala maana unasaka ushindi. Ila ufahamu hizo propaganda mfu za mabeberu wanaambiwa watu wasiojua lolote, na wepesi wa kukubaliana na hoja za kizee.
 
Propaganda mfu za mabeberu..

Hoja ya kizee...

Dah
 
Mkuu kasema kipi kibaya au ambacho siyo kweli?
Kukosoa hatukatai kukosoa ila kuna watu kama huyu dingi ,kila kitu kwake kuhusu nchi yake ni.negative tangu utawala wa awamu ya nne , huoni kama kuna tatizo kweli? Mbaya zaidi anaelezea mataifa ya nje
 
kwa niliyosoma kutoka katika thread hii nimeamini upinzani wa Tanzania unawatu wenye shida katika akili zao yani wanateseka hawana amani wala matumaini tena .

hata katika maisha ya kawaida ukiona mtu ameshikilia Sana mambo yaliyopita ujue afya yake ya akili haiko sawa.

sawa uchaguzi haukuwa huru na wahaki so what? mnachoweza kubadilisha ni kipi sasa JPM . ameshaapishwa mkae mtulie mjue hakuna tena marudio wala huruma itakayowaona nyinyi kila mtu ameshawasahau na kuwapuuza

Askari hanaga mwangwi vitani pigeni mbiu kusonga mbele tambueni madhaifu yenu, yafanyieni kazi mapungufu mliyoyaona waacheni mbwa waliokimbia nchi na kwenda kubweka huko nje hawanga'ti ni mbwa koko.

eti vikwazo vikwazo mkae mkjua kila mtu katika hii nchi anauwezo wa kuwa kiongozi vipi chadema bila lisu, mdee , mbowe nyarandu, lema haiwezekani?

mkiendelea na huu ujinga wenu huku mitandaoni mtaendelea kuwa kituko. magufuli alikuwa bora mara 10 zaidi ya upinzani ndiyo maana akashinda kwa kishindo.

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
Hope moyoni mwako unaamini hivyo pia.
 
Jenerali yuko sawa, utawala huu umerejea madarakani kwa HILA na MABAVU. Hakukua na uchaguzi wowote ule.
 
Misimamo thabiti itaishi kumbukizi zitadumu comrade jabari kwenye tasnia ya habari, siasa na haki za kidemokrasia

Mungu akulinde umetimiza haki yako na ulinzi wa taifa mzalendo wa kweli asiyerubuniwa na mirungura ya watawala

Historia itakurejea kuwa ulikuwa nhuli kwenye kusema na kupigania ukweli utamalaki
Heko kwako generali ulimwengu hakuna kupepesa macho ukweli utakuweka huru

Wajukuu wako watajivunia kuwa wewe ni mkweli na mzanlendo kwa nchi yako.
 
Back
Top Bottom