Jenerali Ulimwengu: Hakukuwa na Uchaguzi huru na haki

Hilo la kuchoma kura ni la uongo kabisa...hizo zinazodaiwa kura fake mliziandaa nyie chadema na wewe chadema ukaziona mlizoziandaa wenyewe na mkazichoma Moto baada ya kufanya stage ya kupiga video za uzushi...Hilo la waangalizi wa uchaguzi itoshe tu kusema ripoti za waangalizi ziliona utoto wa upinzani...kuhusu mawakala chadema na vyama vingine vyote vya upinzani hazikuwa na resources kuweka mawakala kwenye vituo vyote...hamkuwa na fedha kuwalipa mawakala wenu...wakala hawezi kukaa kwenye kituo bila hata maji kuanzia saa kumi na moja alfajiri mpaka usiku wa manane...kwa hili chadema wakaja na utoto kuwa eti mawakala wamefukuzwa...nimewahi kuhusika na uchaguzi miaka ya nyuma mawakala wa vyama vya upinzani wanaleta huruma Sana kwani ni wachache tu ambao hulipwa...kuhusu low voter turnout hili ni tatizo la dunia nzima...uchaguzi wa 2010 kwa mfano waliojitokeza kupiga kura walikuwa below 50 per cent...nilihusika katika utafiti kufahamu sababu za low voter turnout...sababu hizo siwezi kuziweka happy...

Kwenye uchaguzi huu wa 2020 chadema ilishindwa fair and square ..hakuna wa kulaumu Bali wao wenyewe chadema...kumleta kibaraka Lissu kuwa mgombea kwa tiketi ya Chadema lilikuwa ni kosa kubwa la kimkakati...ndiyo maana baadhi tulisema kuwa kwa kosa Hilo chadema isingeweza kupata hata viti kumi vya ubunge au asilimia hata 20 ya kura za urais...watanzania hawapendi ukoloni na ubeberu..Lissu alikuwa anapigiwa debe na mabeberu kwa hiyo likamkosesha kura nyingi..kwenye kampeni yeye Lissu akawa anamtaja Magufuli muda mwingi huku Magufuli kwa mkakati ulioandaliwa akawa hamtaji kwa jina huyo kibaraka..
 
Jenerali uko vizuri Mungu akubariki!!!!
Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu(kwa sauti ya jiwe)
 
Duh...kazi ipo...huyo Boniface una maana yule meya bondia aliyemdunda mwandishi wa habari kwenye uchaguzi wa 2015? Ni Nani atamwamini yule hupendelea kuvaa magwanda Kama ya mpigania Uhuru? Tanzania Election Watch? Nilikuwa naiangalia Sana..ilijaa Wakenya went chuki na nchi hii...kile kimama chenye umri mkbwa nilikuwa siku zote kinasoma tu ripoti iliyoandaliwa...wale walikywa ni paid agents na mabeberu...
 

Unaona usivyo na hoja sasa, Nguo zinahusiana nini na kuripoti jinai polisi
Yule mama Jaji, Ni Mganda na siyo Mkenya
Hii inaonyesha unaongea bila facts
 

Hilo la kufukuzwa kwa wakala nina ushahidi nalo wala sizui. Kura fake zilikuwa kila mahali, mbona polisi hawakuzikamata kama wanavyokamataga bangi au bidhaa zozote haramu? Kama hizo kura zilikuwa ni za cdm, kwanini polisi hawakumtia yoyote hatiani kwa hizo kura fake, ili uchaguzi usiingie doa?

Usihusishe uchaguzi huu na zilizopita, maana hizo zilizopita walikuwa na mawakala kila sehemu walipokuwa na mgombea. Huu mchezo wa kuanza kuhujumu mawakala, na kunajisi uchaguzi waziwazi bila hofu umeanza baada ya Magu kuwa rais, sio kwamba huko nyuma ilikuwa hakuna wizi, ila safari hii ni zaidi ya wizi. Chaguzi zote zilizopita hatukuwahi kuona wagombea wa upinzani kuenguliwa kwa wingi kama sasa kutokana na mizengwe ya wazi. Hizo sababu za watu kutokijotekeza kupiga kura ni kukosa imani na box la kura. Hizo nyingine unazoficha ni mbwembwe tu.

Eti watanzania hawana imani na mabeberu, hizo propaganda mfu za ccm ndio unazitumia kujenga hoja hapa? Nchi hii imejaa miradi kibao ya wazungu, mbona hao watanzania wasiigomee ili hiyo propaganda mfu ipate uhalali? Deni kubwa la nchi hii ni la hao hao wazungu, limetoka wapi kama watanzania hawana imani na mabeberu? Hao watanzania unaosema wanawachukia mabeberu, si ndio hao kuanzia rais, waziri, mbunge, mtendaji wa mtaa, mpaka raia wa kawaida anaona fahari kupiga picha na mzungu? Nenda leo kijijini huko kwenye hao unaosema ni watanzania, kisha uwe na mzungu uone wanavyomtetemekea na kumuorodhoshea matatizo yao ili awatatulie. Hizo propaganda mfu za mabepari kawapelekee wenye upeo mdogo boss.
 
Hilo la bidhaa za wazungu tunazitumia eti huku tukiwaambia kuwa ni mabeberu tulilisikia pia kwa kibaraka Lissu wakati wa kampeni....dah...siwezi kuendelea na debate hi kwa kuwa it is turning into a secondary school debate rather than a debate of serious and learned people..
Yaani ni sawa na debate ya village life is better than town life...
 

Hamna anayekulazimisha kuendelea na mjadala maana unasaka ushindi. Ila ufahamu hizo propaganda mfu za mabeberu wanaambiwa watu wasiojua lolote, na wepesi wa kukubaliana na hoja za kizee.
 
Hamna anayekulazimisha kuendelea na mjadala maana unasaka ushindi. Ila ufahamu hizo propaganda mfu za mabeberu wanaambiwa watu wasiojua lolote, na wepesi wa kukubaliana na hoja za kizee.
Propaganda mfu za mabeberu..

Hoja ya kizee...

Dah
 
Mkuu kasema kipi kibaya au ambacho siyo kweli?
Kukosoa hatukatai kukosoa ila kuna watu kama huyu dingi ,kila kitu kwake kuhusu nchi yake ni.negative tangu utawala wa awamu ya nne , huoni kama kuna tatizo kweli? Mbaya zaidi anaelezea mataifa ya nje
 
Hope moyoni mwako unaamini hivyo pia.
 
Jenerali yuko sawa, utawala huu umerejea madarakani kwa HILA na MABAVU. Hakukua na uchaguzi wowote ule.
 
Misimamo thabiti itaishi kumbukizi zitadumu comrade jabari kwenye tasnia ya habari, siasa na haki za kidemokrasia

Mungu akulinde umetimiza haki yako na ulinzi wa taifa mzalendo wa kweli asiyerubuniwa na mirungura ya watawala

Historia itakurejea kuwa ulikuwa nhuli kwenye kusema na kupigania ukweli utamalaki
Heko kwako generali ulimwengu hakuna kupepesa macho ukweli utakuweka huru

Wajukuu wako watajivunia kuwa wewe ni mkweli na mzanlendo kwa nchi yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…