Je si kweli kuwa Watanzania walifanywa mazuzu?Dume zima kuendelea kumsimanga marehemu ni dalili za uoga.
German East Africa, Rwanda na Burundi zilikuwa part ya Tsnganyika.Uongo huu...
Lini Rwanda ilikuwa sehemu ya Tz mpaka Nyerere awe na uwezo wa kuwachagulia kiongozi ?
Unaweza ukaenda Ulaya au kusoma Ulaya ukawa huna bado exposure. Kujadili kwako hoja kunaonesha ulivyo. Kuongea kijerumani si hoja hizo lugha tumeziongea tukiwa bado wadogo, hadi Kirusi. Na usiseme kuna kundi dogo Ujerumani. Unasema kwa dhania. Mtu mwenye akili timamu uwezi kuongelea mtu badala ya maendeleo. Kuna watu wanasoma lakini kawajaelimika. So unadhani ukimsema vibaya mtu ndo maendeleo. This is Rubish!Kama una mazuri yake umekatazwa kuyasema? Anzisha uzi wa mazuri ya mungu-mtu wako. Usifunge watu midomo waliopitia mabaya ya yule dikteta kuyasema. Hili ni jukwaa huru. Wee ni nani mpaka ufunge watu midomo? Hata Muumbaji wetu ametupa uhuru wa kuchagua kati yake na shetani.
Mzee Mwinyi alisema maisha ni hadithi. Jiandikie hadithi yako nzuri wakati ukiwa hai. Kama ulikuwa mtu wa kutukana, kuua, mwenye hasira, mwonevu, mvunja katiba, mwongo... km huyo kipenzi chako ndio hadithi yako hiyo uliyojiandikia. Haiwezi kubadilika baada ya kuzikwa.
Unataka umlazimishe Lissu aliyepigwa risasi kwa amri ya yule jambazi amsifu? Hautafanikiwa. Kama una sifa zake nzuri, anzisha uzi. Watu tuliathirika na udikteta wake hatutaacha kusema. Kama kujinyonga, jinyonge.
Eti sina exposure! Jifariji tu. Ujerumani nimesoma (MSc Heidelberg) na Kijerumani naongea, angalau cha kuombea maji. Hakuna watu wanamsifia Hitler Ujerumani ya leo. Kuna kundi dogo sana la watu wanaitwa neo-nazis ndio wanakubali sera zake. Ni dogo kama mlivyo Sukuma gang kwa sasa hapa Tanzania.
Yaani unataka nimsome kwenye kitabu dikteta ambaye nimeishi maisha yake nikiwa mtu mzima? Sihitaji kusoma vifo vya akina Mawazo, Azory na wengineo kwenye vitabu. Sihitaji kusoma kuenguliwa kwa wagombea kwenye chaguzi eti kwenye vitabu ama kura za kwenye mabegi za 2020 kwenye vitabu. Ni mambo niliyoshuhudia.
Nadhani umepata elimu ya kutosha bure.
Nimekuelewa lakini si mara ya kwanza Jenerali kuongea anayoyaongea. Na mrengo wake unajulikana siku zote.Jenerali aliyasema hayo katika kikao kilichohusu mambo ya maridhiano kwa nia njema kabisa. Kabla ya kujadiliana kuhusu maridhiano alielezea umuhimu wa kuelewa nini kilichojiri hadi tukafikia kutokuelewana na sasa tunahitaji kuwa na maridhiano kwa pande zote. Na kama mchambuzi wa mambo ya siasa ameekeza kwa kifupi tu kilichotufikisha hapo. Hajataja jina la mtu yeyote bali kalaumu uongozi ambao ulifanya mambo yaliyowatenganisha wananchi. Nimeona umelakamikia sana maoni yake hadi kufikia kuanza kutaja majina. Kama ni kweli au si kweli tuwaachie wananchi walioyaona mambo yalivyokuwa waamue wenyewe.
Tahahira siku zote udhani yeye ni mjanja, na chakushangaza ujiona mjanjaaa kumbe ni mbumbumbu wa kutupwa. Usukuma gang nikiwa nao ni jambo jema. Make sukuma ni kabila Tanzania. So linaubaya gani. Wasukuma ni kama makabila mengine. Kila kabila linamazuri na mabaya yake. Nadhani umenielewa weye kunguni.Wewe ni zwazwa a.k.a sukuma gang
Mimi naamini huku kudai sana hiyo katiba mpya ni katika sehemu ya ujinga wetu kwa maana ya kwamba tunajiaminisha kuwa matatizo yetu yote Tanzania ni kwa sababu hatuna katiba nzuri, kwamba tukiwa na katiba nzuri basi kila kitu kitakaa sawa chenyewe. Mtazamo huo unatufanya tujione sisi kama wananchi kuwa hatuna tatizo lolote bali tatizo ni kukosekana kwa katiba nzuri tu, sijajua nje ya Tanzania wenzetu wanatutazama vp au wana mtazamo gani kwenye hili kwamba wenzetu nao wanaona kuwa watanzania wale tatizo lao wamekosa katiba nzuri tu ndio maana wako vile walivyo? Sidhani, ila nachojua ni kwamba ujinga wetu unaonekana dhahiri hata hivi jinsi tunavyoidai hiyo katiba mpya.Kusolve tatizo lazima uwe na pa kuanzia.
Msingi wa uendeshaji wa nchi ni KATIBA!
KATIBA mbovu ndo imechangia kuwafanya hao Watanzania kuwa jinsi walivyo!!
This man is very much braveAkitoa mada Kwenye Mkutano wa TCD, Generali Ulimwengu alisema, kuna Mtanzania Mmoja alikufa miaka michache iliyopita alitupulizia uzuzu na wote tukawa mazuzu.
Geberali apewe ulinzi
Tazama Video
View attachment 2182469
Hata hivyo sio ajabu maana waafrika hadi leo bado wanalalamikia utumwa(kama ni wao tu pekee ndio walifanywa kuwa watumwa) na kuona kuwa ndio umewafanya wasiendelee.Je si kweli kuwa Watanzania walifanywa mazuzu?
Kwamba COVID walilazimishwa kuita changamoto ya kupumua! huu kama si ujinga ni kitu gani!
Kwamba, watu wachemshe nyasi ili kuepuka changamoto ya kupumua, huu si ujinga ni kitu gani!
Kwani yule waziri aliyesafiri kwenda kunywa mchachai madagascar kama haukuwa uzuzu ni nini?
Kwamba, tunatumia fedha za ndani wakati deni la Taifa linaongezeka. Huu si uzuzu ni kitu gani!
Kwamba, uchumi unakuwa leo Mwigula anatuambia ulikuwa taabani, kama si uzuzu ni nini
Kwamba, maiti za kutoka South Africa zinasafiri hadi Coco Beach! huu kama si uzuzu ni nini
Orodha inaendelea
Hata hivyo, JPM kama kiongozi hana immunity yu kutosemwa kwa kisingizio cha Marehemu
Nyerere ni marehemu miaka 23 na kila siku anasemwa kwa mazuri na mabaya, seuse JPM
JPM aliishi kwa gharama za umma yeye ni public figure, watu wana haki ya kusema
Alichosema Jenerali Ulimwengu ni ukweli mtupu! hata kama unauma bado ni ukweli
Then hiyo kutokuipenda ionesheni kwenye kuikosoa vikali ccm.
Jamii inapaswa ijue maovu ya chama hicho!!
Unaongelea mambo ya kabla ya mwaka 1914 ...Dark days...German East Africa, Rwanda na Burundi zilikuwa part ya Tsnganyika.
Magu alianza vizuri sana,lakini alishindwa kuvumilia siasa za wapinzani au mtu yeyote aliyekwenda kinyume na yeye.Alifanya hivyo kuanzia Oktoba 2015 had Januari 2016 tu. Kipindi hicho dunia nzima ilimpenda. Baada ya hapo akabadilika. I do not know shetani gani tu alimshukia!!
Umeandika gazeti reeefu!! Uzuzu mtupu! Wewe ni yale mazuzu ya Magu yaliyojifichaNachoshangaa Tanzania ya leo, badala ya kukaa kuwaza nini tunahitaji kwa nchi hii iendelee, tumekalia kulalamika ati alikuwa mazuzu. Hivi kama ulikubali kuwa zuzu unamlalamikia nani?
Rais alopita alikuwa na yake kaondoka, hata tukae tumseme mara mia haitobadili kitu. Na cha ajabu kesha tangulia mbele ya haki. Kwanini kama nchi tusijikite katika kuangalia ya sasa na yajayo. Kuliko kila siku vikao na hotuba zisizo na tija kwa nchi yetu.
Kuna nchi nyingi Ulaya ziliongozwa na madikiteta na walikuwa na mabaya hata zaidi ya rais alopita. Lakini uwa sisikii wakipoteza muda kukaa na kulaumu na kumsema au kuwasema vibaya hao madikteta. Ulaya wanaangalia kuendeleza nchi zao na si kukalia umbea.
Mrusi anakombora la supersonic, Mmarekani, Mwingereza na Australia wameungana kubuni ugunduzi utakao saidia namna ya kujikinga na makobora ya supersonic.
Akili ya mtanzania inawaza kumsuta na kumsema vibaya marehemu ambaye hawezi wajibu. Tunajioona kuwa sisi ndo sisi. Huyu Ulimwengu amekuwa kiongozi wa nchi hii, hivi nini alianyia nchi hii ambacho tunaweza tukakikumbuka? Au yeye ni kukosoa kila siku, na cha maana hatukioni toka kwake. Nasi tunakaa kumshangilia. Na kuonesha ameishiwa kila siku hutumia maneno yale yale.
Watanzania tubadilike, tuwaze namna ya kuendeleza nchi yetu. uangalie ni maeneo yapi tunahitaji kuyapa nguvu na kukuza uchumi. Tuwekeze kwenye elimu ya kisasa.
Mzee Ulimwengu amekuwa ktk siasa muda mwingi huko nyuma. Allizunguka ulimwengu. Uwa nikiangalia Tanzania hatuna scholarship maalum kwa nchi za nje. Ukiachana na zile zinazojumuisha nchi zinazoendelea, au Jumuia ya Madola.
Zaidi tulionayo pekee inayopokea watanzania wasiozidi wawili ni ya Mwl Nyerere Scholarship ktk chuo alichosoma huko Uingereza. Ukilinganisha na mataia kama Nigeria, Uganda, Ethiopia, Rwanda na hata Burundi ambazo zinakuwa na scholarship huko nje kwa wingi.
Hivi balozi zetu wanaanya nini? Wanashindwa kushawishi vyuo vya nje au serikali za huko kuwa na scholarship maalum kwa ajili ya watanzania? Tunahitaji watanzania wengi waende nje wasome na kuwa na teknolojia, warudi kuitumikia nchi. Rwanda wameanya hivyo. Ethiopia, Nigeria na hata Ghana.
Nilikuwa chuo huko nje, viongozi kutoka Ethiopia wamekuwa na ziara kadhaa ktk hicho chuo kujenga mahusiano, na kinapokea waethiopia wengi wakipata scholarship. Niliwahi kuona baadhi ya viongozi wa kitanzania ktk dini wakitembelea lakini sikuwasikia wakiongea chochote kile zaidi ya kuonesha ukubwa wao na kusemana. Kuna kiongozi mmoja ilibidi tuwe na mabishano ya muda kisa anamsema kiongozi mwenzie ili wazungu wamuone mbaya. Na alikuwa wanapanga kumwondoa. Hii ndo akili zetu watanzania hata tunapozuru nje hatuachi asili ya kusemana.
China ni tajiri na wanatechnolojia kubwa lkn bado wanapeleka vijana wao wengi nje kwenda kusoma, Korea kusini, India na nyinginezo. Tanzania tunahitaji mabadiliko. Nakumbuka nilipoingia kuanza kazi za serikali huko nyuma, wapambe walianza kunieleza mabaya ya yule alopita ktk hiyo ngazi niliokuwepo. Nilichoona ni vema iwe msimamo wangu sikunyanyua mdomo kumsema au kuuliza juu ya mtangulizi wangu. Nililenga nini kinatakiwa kutekelezwa katika majukumu yangu na si kumuongelea mtu. Hii iliondoa tabia zao za umbea, na hawakuendelea kumsema huyo mtangulizi. Nilibaki kumheshimu na hata kuna muda tuliongea kwa uzuri tu kwenye simu.
Watanzania tuache majungu tujikite ktk kuleta mabadiliko ya kimaendeleo. tuache kujipendekeza, wakati mwingine tunatumia hela nyingi kusherehesha mambo yasiyo na maana badala ya kujikita kuleta maendeleo kwa wananchi. Serikali ipo kuwatumikia wananchi na si wananchi kuitumikia serikali. Serikali ipo kutatua kero za wananchi na si viongozi kujiona wao ni wamaana sana kuliko wananchi.
Wananchi leo akili zetu zimeishia katika katiba, hivi kuna nchi ngapi duniani zingine hazina katiba lakini wanamaendeleo makubwa. Tazama nchi za Umoja wa nchi za Kiarabu. Uingereza isiyo na katiba ya kuandikwa. unahitaji viongozi wanao iwazia Tanzania mioyoni mwao. Viongozi ambao wapo kuhakikisha Tanzania inapiga hatua ya kimaendeleo kuliko tubaki kama tulivyo kila iitwapo leo.
Kuna research nyingi huko vyuoni, lkn zinaachwa tu kuchakaa na baadae kuchomwa moto huko vyuoni. Wasomi wamegeuka machawa wa wanasiasa.
Kwa nini nchi yetu tusiwe na chombo ambacho kinachunguza hizi research na zile bora wahusika watambulike na research zao zitumike kuleta mabadiliko ktk nyanja mbalimbali. Nchi moja nayoijua huko Ulaya utumia vigezo hivi na wanapopata research muhimu hata sheria ubadilishwa ili kukidhi haja. Hii inatia moyo vijana wetu, na pia kuendesha nchi kisayansi na si kichawa.
Namalizia hata tukimsema JPM mara mia, haitotusaidia kitu. Na tunapoteza muda wetu bure wakati yeye kapumzika, na uenda anatuangalia na kusikitika na hasa kucheka kama alivyozoea. Chuki uwa haina lolote la maana juu ya mwanadamu. Bali upendo hata kwa wale wanaokuchukia. Hii uleta kuishi maisha ya amani zaidi.
Umeandika gazeti reeefu!! Uzuzu mtupu! Wewe ni yale mazuzu ya Magu yaliyojificha
Naam, tulikuwa tunaogopa kupigwa risasi, mwili kuwekwa kwenye gunia na kutupwa baharini.
Ngoja waje. Hayati alikuwa na wakati mzuri wa kutufanya tumseme vizuri akifa. Lakini alikaza shingo matokeo yake kaacha msala
Mbona mimi namshambulia na kukosoa maovu aliyoyafanya kwa taifa, born and bred Catholic(dini za kuletewa na wageni japo tuna zetu 'original' za Kiafrika).Acha kutafuta huruma kwa kutumia. dini!! Kama una hoja mtetee Jiwe !