Jenerali Ulimwengu ni mtu Hatari sana kwa Ustawi wa Taifa Staarabu. Ana Uhatari Mkubwa katika kauli zake

Huyu jamaa angekuwa nchi yake ya asili hata mwaka asingemaliza, ashukuru huku Kuna amani
Yeyote anayehoji uraia wa Jenerali hana akili atuambie mtanzania ni nani, sasa hivi dewji ambaye ni muhindi anaponda wamasai ambao ni waafrika na kuwataka watoke loliondo ila wajinga hamjazungumzia uraia wake.
 
Hata mwendazake alijifanya mwenye akili kuliko yyt Tanzania kwa hiyo ndg.tuvumilane.,.
 
Nakubaliana na ww Ulimwengu anakuwa kama siyo msomi. Anapenda sana personal attacks kwa watu asiokubaliana nao kimawazo.
 
jenerali Ulimwengu sio manafiki na sio muoga na nimtu mzalendo wa hali ya juu so sishangai vibaraka kama wewe mkijaribu kumchafua
Hana uzalendo wowote ndani yake.
Cheo cha ukuu wa wilaya alishindwa kuonyesha uzalendo wake hata kwenye eneo dogo tu la wilaya!!
NGOMA IKILIA SANA .......................
Ni ishu ya muda tu.
 
Ana akili nyingi. Ndiyo tunvyomuona sisi. He deserves his freedom of expression as stipulated in the constitution.

 
Aisee

Naona chuki binafsi kubwa mno....

Eti anaongea kwa ujivuni.....ujivuni ni staili ya mtu,u have no power over it...wewe attack substance yake sio staili

Naona umejikita kwenye haiba yake na namna yake binafsi anayoongea,hujagusa hoja zake maana huziwezi

Kila mtu ana staili na namna zake,hupendi ni too bad....wewe mwenyewe kwa article yako hii ni jivuni namba moja,nyani haoni kundule?
 

Jenerali anaongea ukweli, ila ww umezoea watu makondoo ndio maana lugha za kujiamini zinakuudhi. Hao akina Warioba, Shivji nk unaowasifia kuongea lugha ya kistaarabu, ni kipi wanachoongea kinatekelezwa kwa kuwa wanaongea kistaarabu? Ustaarabu wa viongozi wetu, lugha kali ndio wanazielewa sio hizo za kubembelezana.
 
Mkapa alimwondolea uraia.
Inadhaniwa ni mtutsi.
Siku tukikubali kuwa Mtutsi anaweza kuwa Matanzanaia sawa na Mgogo wa Dodoma hapo ndipo Tanzania itakapopata maendeleo.

Sioni tatizo lolote kama mtu anasema mambo ya msingi ya kulisaidia taifa au raia asiye mzawa akatuongoza vyema kuliko kuongozwa na Mzawa asiyejali maslahi ya nchi.

Kuwa mzawa peke yake haisadii ...... Hata akina Mobutu Kuku wa Zembango, Idd Amin walikuwa wazawa kwenye nchi zao lakini hawakuzisaidia nchi zao.
 
Watutsi ndivyo walivyo huwa wanajiona wao ndiyo Wana akili kuliko jamii zingine, kwaiyo msimlaumu Jenerali Ulimwengu ndiyo asili yake kwao Rwanda.
Na mara nyingi watu waongea hovyo ukiwapa madaraka huwa wanafeli vibaya.Alikuwa DC alifanya nini?
 
Anatumiwa na mtu mrefu mwembamba kutuvuruga. Uzuri Tanzania hatutokagi kwenye reli. Utaminywa wewe lkn TZ inabaki kwenye njia. Yeye na OMO wanataka kututoa kwenye njia. HATUTOKIIII Ng'o.
 
Pandikizi la Unyarwanda huyo, Tanzania ni ya ajabu sana, foreigners ndiyo wanapaza sauti tena kwa dharau na dhihaka bila ya hofu yoyote, huyo angekuwa nchi kama Kenya angeshaona moto, kwa kifupi hatuna nchi hapa!
Vijana wa juzi hamuifahamu hata historia ya nchi yenu. Eti pandikizi la unyarwanda!
Huyo mzee ametumikia nchi hii toka enzi za mwalimu, na Nyerere alimtumia sana Ulimwengu wakati wa harakati za ukombozi kusini mwa Afrika ndani ya OAU pamoja na kina Salim Ahmed Salim.
Jenerali ana rekodi iliyotukuka zaidi ya wababaishaji na majizi mengi yaliyoko katika utawala sasa hivi.
 
Lazima utamchukia sana Jenerali huyu hana umbea umbea. Juzi kampa makavu Mkapa nadhani huko chini alitikisika, alisema mkapa hakuwa mwandishi na hajawai kubeba Notebook. Akaja akamvaa mwehu Mrema. Akampa makali mengine mwizi wa 1.5T zetu ambaye alijiona ana akili nyingi sana. Alishangaa watanzania kuongozwa na kichaa. Je unataka kumchukia hata pale aliposema Kikwete anatakiwa kushitakiwa kwa kuchezea pesa za watanzania kwa kuhujumu mchakato wa katiba. Huyu Ulimwengu ni hatari alivyomnyonyoa Ndugai alisema alikuwa anaropokaropoka tu alivyosema hatake asikate lazima ataongezewa muda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…