MahinaVeterani
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 710
- 256
Mama Joe,
Umeme, Taa na Feni si unazungumzia sebule sasa hapo?
Vipi ukiongezea na Ka-TV na Makochi kabisa?
Tuseme unaweza ukawa mbunifu ukaweka na kitanda Pia?.
Ili kunogesha unapiga kabisa na kabati la nguo humohumo ndani ya Greenhouse!!!
Habari za siku mkuu, umerudi kivingine, nakuaminia na nimeipenda hii ngoja tutafute hela kidogo. Maelezo yako yamenivutia japo nimekuwa nikizisoma na kuzisikia muda mrefu ila hapa nimevutika zaidi. Nyongeza tu, zaidi ya maji hakuna gharama nyingine? mfano umeme au taa, feni? Nikipata muda nitakuja kuona shamba darasa na kujifunza zaidi.
Mkuu;
Makadirio yagreenhouse kwa hekari nzima yapoje? na je hiyo miche unayootesha inatsha kupanda kwa eneo gani?
Na je una wataalamu wataoweza kutrain vijana wangu wa shamba? Ahsante
Mama Joe,
Umeme, Taa na Feni si unazungumzia sebule sasa hapo?
Vipi ukiongezea na Ka-TV na Makochi kabisa?
Tuseme unaweza ukawa mbunifu ukaweka na kitanda Pia?.
Ili kunogesha unapiga kabisa na kabati la nguo humohumo ndani ya Greenhouse!!!
nashukuru kwa ufafanuzi kwani umeonyesha hata return inawezekana kwa muda gani ngoja basi tutafute tutakuja.
Nilikua nakutania bana,Usinicheke ninajifunza mwenzio, hii si mara ya kwanza hapa jamvini kuna mtu aliileta maelezo ila ilikuwa complicated sana na fan sijui thermometer na mambo mengine. Tulijaribu kumuuliza ina maana lazima tuwe na umeme maana hizo feni za ventilation, hakujibu hapo tulikata tamaa wengi tu. Hapa nilikuwa ninataka kuhakikisha hii ikoje.
Karibu sana Mikwambe, utaelimika zaidi.
Nilikua nakutania bana,
Lakini si umeona amesema sometimes inatakiwa uyadanganye mazao yajihisi kama vile yako nje? Kwa hiyo kama unalima mazao yanayostawi kwenye ubaridi inabidi ufunge kileta baridi ambacho kinatumia umeme, Na kama unalima mazao yanayostawi kwenye joto inabidi ufunge kileta joto (Taa) ili mazao yajihisi yako kwenye joto ha ha ha!!K
Ila kwa kweli hapa tunapata darasa tosha kutoka kwa mamaNa,
Hii kitu kusema ukweli ilikua ndotoni kwangu muda mrefu tu. Sasa mdau hapa kaileta wacha nipate shule, ikiniingia nitamtafuta.
Nauza Materials na kusadia ujenzi wa Greenhouse za ukubwa mbali mbali. Kwa sasa Nina materials zinazoweza kucover greenhouse ya ukubwa wa mita nane kwa mita kumi na tano (8x15m), Zina uwezo wa kuzuia jua, kuzuia wadudu na vihatarishi mbali mbali vya mazao.
Bei ni Mil2.5 kwa materials pekeyake yaani 1/8 of an ancre drip lines, Polythene Cover (UV400 Protected sheets), 70% Micron insect Netting...Hizi zitakuwezesha kujenga Greenhouse yako bila matatizo. Kitakachohitajika kutoka kwako ni Wooden Poles (nguzo kama zinazojengewa baa za makuti nk), tanki la lita 500 la maji na maji ya uhakika.
Ntakupatia mafundi na muongozo mzima wa kujenga greehouse yako ili kufanikiwa.
Faida za kulima katika greenhouse ni nyingi mno, ikiwemo matumizi mazuri na sahihi ya ardhi, kwani kiwanja cha ukubwa wa mita 8x15 kinaweza kukupa Nyanya hadi Tani 30 kwa mwaka, Pilipili hoho tani 20 kwa mwaka na mazao mengine mengi yanayolimwa katika controlled environment.
Kuna wataalamu wa kutosha hivi sasa hapa Dar Es Salaam wanaoweza kukupa muongozo, mbegu bora na fertilizers za uhakika.. Tuwasiliane kwa simu namba 0714881500 ili kupeana muongozo..
Karibuni sana.
Ili uweze kufanikiwa katika kilimo hiki, unahitaji maji ya uhakika minimum lita 200 kwa siku kwa ajili ya kumwagilia nyanya kwa matone, Nitakupatia mabomba (driplines) zitakazokuwezesha kufanikisha hili.
NB: Kumbuka Greenhouse inajengwa kwenye eneo lililo wazi, lisilo na miti mirefu inayozuia jua...
Pia ni Muhimu kufanya Soil Test na Water Test ili ujue ni kipi unahitaji kuongeza kwenye ardhi yako ili upate mazao ya uhakika... Naweza kukusaidia kufanya soil na water test kwa gharama nafuu kabisa kutoka nchi ya Jirani (kenya). Gharama ni 250,000 kwa huduma hii pekeyake (Complete Soil analysis & Water Test).
NB::: UJENZI WA GREENHOUSE YA MFANO UMEKAMILIKA. IPO MIKWAMBE KIGAMBONI::: KARIBUNI SANA.
View attachment 140539 View attachment 140540 View attachment 140541 View attachment 140542 View attachment 140543 View attachment 140547
Namba yangu ni 0714881500,Mamana hebu tupia number yako hapa
Nimeshakutumia ndugu, lakini naona ni vema kila mwenye maswali yanayohusiana na kilimo hiki ayaulize hapa ili kuendeleza uzi huu na kunufaisha wengi.Mkuu naomba unitumie email kwa selu.business@gmail.com[/email] tafadhali. Nitakuwa na maswali mengi huko
Kweli kabisa, kipindi hiki cha mvua ndio burudani kwa mkulima wa kwenye greenhouse kwani anavuna bila matata na bei anapanga yeye vizuri kabisa.Hapa nang'ana na eden za masika ningekuwa na greenhouse si ningekuwa najila pesa kwa wakati huu maana kwa sasa huku Moshi nyanya haishikiki. Ngoja nijipange mie. Walao niandae hiiyo 14 m.. Mungu akipenda mwisho ea mwaka nitakuita mkuu.
Karibu sana,Na hapo kwa organic inputs ndiyo umenikuna. Huna za outdoor ?