Jenga Greenhouse kwa gharama nafuu

Jenga Greenhouse kwa gharama nafuu

Mama Joe,
Umeme, Taa na Feni si unazungumzia sebule sasa hapo?
Vipi ukiongezea na Ka-TV na Makochi kabisa?
Tuseme unaweza ukawa mbunifu ukaweka na kitanda Pia?.
Ili kunogesha unapiga kabisa na kabati la nguo humohumo ndani ya Greenhouse!!!

Michango kama hii, kwenye Uzi wa muhimu kama huu, nadhani kwa Kiingereza inaitwa "counterproductive". Haisadii!

Ninaomba tuendelee kuelimishana kuhusu Greenhouses, ambazo Majirani zetu wamepiga hatua kubwa sana!
 
Last edited by a moderator:
Habari za siku mkuu, umerudi kivingine, nakuaminia na nimeipenda hii ngoja tutafute hela kidogo. Maelezo yako yamenivutia japo nimekuwa nikizisoma na kuzisikia muda mrefu ila hapa nimevutika zaidi. Nyongeza tu, zaidi ya maji hakuna gharama nyingine? mfano umeme au taa, feni? Nikipata muda nitakuja kuona shamba darasa na kujifunza zaidi.

Habari ni njema kabisa Mama Joe, Kwakweli kwa Tanzania na hali yetu ya hewa ilivyo nzuri hatuna sababu ya kuingia gharama ya ziada kama umeme na feni na taa...Kama ingekuwa tunafunga greenhouse Europe au South Africa, nchi zenye theluji na baridi kali wakati wa winter basi tungefunga na Heater, Temperature control, themometer na automatic blowers ili kubadilisha mazingira ya greenhouse yaendane na matakwa ya mazao, kwa mfano inapokuwa ni -4 degrees basi heater zitawaka automatically na kuweka chumba kikawa na joto mpaka litakapofikia 25 degrees halaf temperature control itaizima na kuendelea kuzimika mpaka hapo themometer itakaposoma joto limekwisha tena na thermostat itawasha tena heaters na kufanya mzunguko huu kuendelea mpaka winter inaisha.
Ama kwa zile nchi zisizopata jua la kutosha kama vile za scandinavia na south/north pole basi greenhouse tungeifunga LED lights za kutosha tu ili kuweza "Kuyadanganya" mazao kwamba jua linawaka wakati nje ni giza totoro na mazao yataendelea kukua kama kawaida.
Kama tungekuwa kwenye majangwa ya waarabu basi tungebadili mfumo huo wa heater tukaweka wa baridi kwa kutumia Air conditions, Coolers and blowers za baridi...

Kifupi niseme tu, Kwa Tanzania yetu hii, tumebarikiwa mengi kiasia cha kuepuka gharama hizi za ziada. Kama utataka kuweka taa ni chaguo lako lakini hakuna umuhimu huo, kwani nyanya, hoho, tango havina sababu ya kutumia taa ili viendelee kuishi...

Karibu sana.

NB: NikukumBushe tu, Greenhouse Hizi ninazojenga zinaishi miaka hadi Kumi (10) kwa zile structure ya wooden poles, na miaka mitano hadi saba kwa poly covers na insect netting... Sasa Kwa investment ya 3.5m-5, ukaweza kupata return katika miezi minne ya uzalishaji (kuanzia mwezi wa tatu wa kupanda hadi wa saba) kisha ukaendelea kuvuna kwa mwaka mzima, na Baada ya mwaka mmoja ukarudia tena kupanda kwa gharama ya 290,000 tu (miche/mbegu) na ile mil3.5 haijirudii tena mpaka baada ya miaka mingine 10, basi ni uwekezo bora kabisa na mkombozi mwema wa mwafrika, Tuamke tu na kuchangamkia hii fursa.

TULIME ILI TULISHE TAIFA LETU. TUACHE KUINGIZA NYANYA KUTOKA SOUTH AFRICA NA KWINGINEKO.

UNAWEZA KUMUHITAJI MWANASHERIA MARA MOJA TU KWA MAISHA YAKO YOTE LAKINI UNAMUHITAJI MKULIMA KILA SIKU YA MAISHA YAKO, HATA UKIWA MWANASHERIA UNAWEZA KUWA MKULIMA PIA NA UKAENDELEA KUHITAJIKA KILA SIKU BADALA YA SIKU MOJA KWA MWAKA.
 
Mkuu;

Makadirio yagreenhouse kwa hekari nzima yapoje? na je hiyo miche unayootesha inatsha kupanda kwa eneo gani?
Na je una wataalamu wataoweza kutrain vijana wangu wa shamba? Ahsante
 
Mkuu;

Makadirio yagreenhouse kwa hekari nzima yapoje? na je hiyo miche unayootesha inatsha kupanda kwa eneo gani?
Na je una wataalamu wataoweza kutrain vijana wangu wa shamba? Ahsante

Heka moja ina 70*70m,
Kitaalamu nisinge shauri ujenge greenhouse ya mbao kwa ukubwa huu kwasababu gutter za maji zitasumbua baadae zitakapoanza kuchoka. Alternatively unaweza kujenga greenhouse nne kubwa, zenye urefu wa mita 30 na upana wa mita 15, spacing kati ya greenhouse kwa urefu itakuwa ni mita 10 na upana kutakuwa na spacing ya mita 2.5, hii itasaidia strength ya greenhouses na good aeration system ili kuweza kufanya mazao yapate temperature nzuri. Gharama ya kila greenhouse moja ya 15*30 ni 14m, kwahiyo kwa 4 ni 56m. Ukiwa nazo nne katika shamba la heka moja, unaweza kufanya crop rotation nzuri sana, yaani katika greenhouse moja ukalima nyanya, nyingine hoho, nyingine tango na nyingine maua au strawberry nk.. hii itakuguarantee return in 4months za production na profit ya min 70m per yr on your first year of production.
Miche Naotesha kulingana na matakwa ya mteja, ukitaka miche ya idadi yoyote ile, ninayo nursery ya kukidhi mahitaji hayo.
Wataalamu tupo na mimi mwenyewe ndio ntakuwa muhusika wa training kwa masimamizi wa mashamba ya wateja wangu.

Karibu sana.
 
nashukuru kwa ufafanuzi kwani umeonyesha hata return inawezekana kwa muda gani ngoja basi tutafute tutakuja.
 
Usinicheke ninajifunza mwenzio, hii si mara ya kwanza hapa jamvini kuna mtu aliileta maelezo ila ilikuwa complicated sana na fan sijui thermometer na mambo mengine. Tulijaribu kumuuliza ina maana lazima tuwe na umeme maana hizo feni za ventilation, hakujibu hapo tulikata tamaa wengi tu. Hapa nilikuwa ninataka kuhakikisha hii ikoje.
Mama Joe,
Umeme, Taa na Feni si unazungumzia sebule sasa hapo?
Vipi ukiongezea na Ka-TV na Makochi kabisa?
Tuseme unaweza ukawa mbunifu ukaweka na kitanda Pia?.
Ili kunogesha unapiga kabisa na kabati la nguo humohumo ndani ya Greenhouse!!!
 
Usinicheke ninajifunza mwenzio, hii si mara ya kwanza hapa jamvini kuna mtu aliileta maelezo ila ilikuwa complicated sana na fan sijui thermometer na mambo mengine. Tulijaribu kumuuliza ina maana lazima tuwe na umeme maana hizo feni za ventilation, hakujibu hapo tulikata tamaa wengi tu. Hapa nilikuwa ninataka kuhakikisha hii ikoje.
Nilikua nakutania bana,
Lakini si umeona amesema sometimes inatakiwa uyadanganye mazao yajihisi kama vile yako nje? Kwa hiyo kama unalima mazao yanayostawi kwenye ubaridi inabidi ufunge kileta baridi ambacho kinatumia umeme, Na kama unalima mazao yanayostawi kwenye joto inabidi ufunge kileta joto (Taa) ili mazao yajihisi yako kwenye joto ha ha ha!!K

Ila kwa kweli hapa tunapata darasa tosha kutoka kwa mamaNa,

Hii kitu kusema ukweli ilikua ndotoni kwangu muda mrefu tu. Sasa mdau hapa kaileta wacha nipate shule, ikiniingia nitamtafuta.
 
Last edited by a moderator:
naelewa ila kwakweli ameileta ktk mazingira halisi ya Kitanzania hizo zingine hazitufai mazao ya tropics yanatosha.
Nilikua nakutania bana,
Lakini si umeona amesema sometimes inatakiwa uyadanganye mazao yajihisi kama vile yako nje? Kwa hiyo kama unalima mazao yanayostawi kwenye ubaridi inabidi ufunge kileta baridi ambacho kinatumia umeme, Na kama unalima mazao yanayostawi kwenye joto inabidi ufunge kileta joto (Taa) ili mazao yajihisi yako kwenye joto ha ha ha!!K

Ila kwa kweli hapa tunapata darasa tosha kutoka kwa mamaNa,

Hii kitu kusema ukweli ilikua ndotoni kwangu muda mrefu tu. Sasa mdau hapa kaileta wacha nipate shule, ikiniingia nitamtafuta.
 
Mkuu naomba unitumie email kwa selu.business@gmail.com[/email] tafadhali. Nitakuwa na maswali mengi huko

Nauza Materials na kusadia ujenzi wa Greenhouse za ukubwa mbali mbali. Kwa sasa Nina materials zinazoweza kucover greenhouse ya ukubwa wa mita nane kwa mita kumi na tano (8x15m), Zina uwezo wa kuzuia jua, kuzuia wadudu na vihatarishi mbali mbali vya mazao.
Bei ni Mil2.5 kwa materials pekeyake yaani 1/8 of an ancre drip lines, Polythene Cover (UV400 Protected sheets), 70% Micron insect Netting...Hizi zitakuwezesha kujenga Greenhouse yako bila matatizo. Kitakachohitajika kutoka kwako ni Wooden Poles (nguzo kama zinazojengewa baa za makuti nk), tanki la lita 500 la maji na maji ya uhakika.
Ntakupatia mafundi na muongozo mzima wa kujenga greehouse yako ili kufanikiwa.
Faida za kulima katika greenhouse ni nyingi mno, ikiwemo matumizi mazuri na sahihi ya ardhi, kwani kiwanja cha ukubwa wa mita 8x15 kinaweza kukupa Nyanya hadi Tani 30 kwa mwaka, Pilipili hoho tani 20 kwa mwaka na mazao mengine mengi yanayolimwa katika controlled environment.
Kuna wataalamu wa kutosha hivi sasa hapa Dar Es Salaam wanaoweza kukupa muongozo, mbegu bora na fertilizers za uhakika.. Tuwasiliane kwa simu namba 0714881500 ili kupeana muongozo..

Karibuni sana.
Ili uweze kufanikiwa katika kilimo hiki, unahitaji maji ya uhakika minimum lita 200 kwa siku kwa ajili ya kumwagilia nyanya kwa matone, Nitakupatia mabomba (driplines) zitakazokuwezesha kufanikisha hili.

NB: Kumbuka Greenhouse inajengwa kwenye eneo lililo wazi, lisilo na miti mirefu inayozuia jua...
Pia ni Muhimu kufanya Soil Test na Water Test ili ujue ni kipi unahitaji kuongeza kwenye ardhi yako ili upate mazao ya uhakika... Naweza kukusaidia kufanya soil na water test kwa gharama nafuu kabisa kutoka nchi ya Jirani (kenya). Gharama ni 250,000 kwa huduma hii pekeyake (Complete Soil analysis & Water Test).
NB::: UJENZI WA GREENHOUSE YA MFANO UMEKAMILIKA. IPO MIKWAMBE KIGAMBONI::: KARIBUNI SANA.

View attachment 140539 View attachment 140540 View attachment 140541 View attachment 140542 View attachment 140543 View attachment 140547
 
Hapa nang'ana na eden za masika ningekuwa na greenhouse si ningekuwa najila pesa kwa wakati huu maana kwa sasa huku Moshi nyanya haishikiki. Ngoja nijipange mie. Walao niandae hiiyo 14 m.. Mungu akipenda mwisho ea mwaka nitakuita mkuu.
 
Kweli kabisa, kipindi hiki cha mvua ndio burudani kwa mkulima wa kwenye greenhouse kwani anavuna bila matata na bei anapanga yeye vizuri kabisa.
Karibu sana ndugu.
Tuko Pamoja.
 
Na hapo kwa organic inputs ndiyo umenikuna. Huna za outdoor ?
Karibu sana,
Unamaanisha nini sina za outdoor?
Nafanya Drip irrigation installation kwa ukubwa wowote wa shamba, na kukuandalia matuta organically.
Pia natoa ushauri wa kitaalamu na kufanya mpango mkakati wa shamba (farm planning), mfano una shamba lako la heka kadhaa na unapenda kufanyiwa analysis ya nini ulime kwa wakati upi na kwa soko lipi...
Muda si mrefu ntaweka tovuti yetu hewani ili mjionee ni jinsi gani tunaweza kupambana na changamoto za kilimo kwa kutumia teknolojia rahisi kabisa na za bei nafuu.

Karibu sana.
 
kwa mliopo dsm na maeneo ya karbu nawashauri mumtembelee mamana pale kigambon utapata shamba darasa safi kabisa me nlifika pale siku ya jumanne week hii, na nilihamisika na niko kwenye hatuwa za mwisho ili nianze mradi huu, tukiwa wengi na tukaungana kwa kubadilishana mawazo na mitazamo mapinduzi ya kilimo (Agriculture revolutionit is possible in our country ) fulsa ipo katika kilimo cha kitaalam!!
 
Namaanisha mbegu, pamoja na dawa za organic zisizo za greenhouse. =mamaNa;8954928]Karibu sana,
Unamaanisha nini sina za outdoor?
Nafanya Drip irrigation installation kwa ukubwa wowote wa shamba, na kukuandalia matuta organically.
Pia natoa ushauri wa kitaalamu na kufanya mpango mkakati wa shamba (farm planning), mfano una shamba lako la heka kadhaa na unapenda kufanyiwa analysis ya nini ulime kwa wakati upi na kwa soko lipi...
Muda si mrefu ntaweka tovuti yetu hewani ili mjionee ni jinsi gani tunaweza kupambana na changamoto za kilimo kwa kutumia teknolojia rahisi kabisa na za bei nafuu.

Karibu sana.[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom