Jengo Maarufu Zanzibar kwa utalii, Beit Al Ajaib laporomoka

hebu nitajie umri wa hili jengo kesha tuone kama limekuwa historia au ni la miaka mi2 kama unavohisi majengo ya warabu sio imara🐸🐸
1883.Ukienda Rome kuna majengo ya 14.....na yapo imara. Sema hufanyiwa renovation pia.
 
Lilikuwa likifanyiwa ukarabati.

Nilikuwa naenda kuangalia movies Zanzibar International Film Festival hapo.

Inasemekana Sultani alivyolijenga, kuna nguzo fulani katikati aliweka maiti za watumwa.
Sasa ni wakati muafaka wachimbue hizo maati zilizo daiwa kufukiwa chini ya nguzo ikiwa zimesimama paoja na nguzo hizo.
Waletwe wataalamu wa mabaki ya binadau ili wachunguze tuhuma hizo, na zikithibiti basi Jamshi,aliyekuwa mtawala wa Mwishowa Zanzibar kama sultani bado yuko hai Oman awajibike.
 
Ivi hilo limeporomoka lenyewe au limebomolewa ? Huo uzio Wa mabati ni wa nini ? Wakati hua hua kuna fence ya kwaida tu
 
Awajibike kwa jengo lililojengwa kabla hajazaliwa?
 
Tabu ya waswahili.Sultan wa Oman atatuma watu waje kujenga kumbukumbu ya babu zake.
Kwani wewe babu zako wana kumbu kumbu gani zaidi ya vyungu vya udongo na vibanda vya msonge?
sasa wenzio angalau walijenga Ghorofa ya Miti ,udongo na mawe kwa kuitelekeza juu ya Nguzo za Vyuma .Takriban miaka 150 iliyopita ,lazima wajipongeze na kutunza utaalamu wao kwa zama hizo.
 
Hizo zilikuwa ni mbinu za kuwaaminisha watu kuwa waarab ni wabaya.
Jemshid ana miaka zaidi ya 90 na ni mzima wa afya na anatembea kwa miguu yake miwili tena bila mkongojo.
 
Ubaya wa hao watu wanaoitwa Waarabu hauhitaji concept hii.

Biashara ya utumwa tu inatosha kuuonesha ubaya wao.
Mmiliki wa soko la watumwa alikuwa ni mwingereza mwenyewe. Nenda Kanisa la Mkunazini kasome historia.
 
Kwa hivyo Muarabu hajafanya biashara ya watumwa Zanzibar?

Biashara ya watumwa Africa Mashariki kwenda Arabuni ilianza lini? Muingereza alifika lini? Muarabu alifika lini?

Nani aliipiga marufuku?
Umembana kila kona hawezi chomoka hapo....
 
Ila kwa huo uzio wa mabati inamaanisha lilikuwa likifanyiwa ukarabati?
Ulikuwa babaisha toto tu huo uzio. tangu 2012 hadi leo hii ukarabati gani wanaofanya? Nikipita hayo maeneo sikuwa nikiona shughuli zozote za ukarabati zikiendelea. Baniani mbaya kiatu chake dawa, wamiliki halali wa hilo naskia wametoa pesa nyingi wametoa ili jengo walikarabati kwa faida ya SMZ wenyewe kuvutia watalii lakini waaapi!!! Kwenye safu ya uongozi akiwepo mtu anaitwa Balozi Seif Ali Iddi lazima hela zisionekane zimeenda wap 😀

Wanajenga mahakama mpya, tangu kiwanja kitupu mpaka jengo lishakuwa na sura tena, hili la foro hata nguzo moja wameshindwa kuimaliza. Na hio mahakama mpya imeanza kujengwa mwaka huu tu. Serikali ilioacha kiti kwa Mwinyi wamejua kuifisidi nchi!

Nasubiri nione kama kuna mafuvu ya watu kwenye zile nguzo, maana wanamapinduzi walisema nguzo za lile jengo zilijengwa kwa mafuvu ya watumwa 😀
 
Wanamapinduzi nilisikia wanasema kila nguzo ina mafuvu ya watumwa. Ni muda muafaka sasa yatafutwe, wataalamu waje wafanye utafiti wanaweza kutwambia walikuwa watu gani/wa wapi n.k

Hata Bungi miembe mingi walisema kila kwenye muembe kuna mafuvu ya watumwa.... miembe inakatika lakini bado fuvu halijapatikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…