Wakuu kuna ishu inaendelea huko makao makuu ya Polisi kuhusu jeshi la Polisi kutumika Kwa matakwa ya mtu binafsi.
Huu ujumbe nimepenyezewa kwamba mambo si shwari kabisa.
"Kuna hatari mbele kuelekea 25.11.2017 Makonda anatakiwa kutambua hili-huku nikutugawa maofisa wa Jeshi vipande vipande na mwisho wa siku jeshi zima.
Ni vizuri sasa hali hii isijirudie na kuelekea 25.11.2017. OCD wa Kinondoni alihamishwa kitengo kingine kuepusha purukushani wakati wa sekeke la Uvamizi wa Clouds na kulinda heshima kati ya IGP na Maofisa wadogo.
Kwa upande wa Wananchi subira ya vuta heri-hatua na uamuzi uliofanywa katika Fiesta siyo kuwakomoa ni kuwanyima wakazi wa Dar burudani tunapaswa kuwa na busara sana lakini tusinyamaze.
Nimemuandikia bwana mdogo Email juu ya kuchukua hatua ya kuuarifu umma na kutoa Taarifa rasmi kwenye mamlaka husika juu ya huu unyama, ikibidi nimemuambia azungumze kwenye kipindi kesho.
Kufanya hivi kutawafungulia milango mbele ya Safari kuwa ni nani mchawi na nani anastahili kubeba Mzigo haiwezekani tutumiwe na mtu mmoja Kwa maslahi yake binafsi. Ugomvi ule ulimalizika sielewi kwanini sasa kuna vita hivi na sisi Polisi tutaoneka wabaya tukitumika kwa matakwa ya mtu binafsi.
Kesho tuonane Collesum, Nipo Safarini kwasasa.
Huo ndiyo ujumbe nilionyetishwa wakuu.