Jerry Silaa kutolewa ardhi, tutarajie tena migogoro ya ardhi kuanza kuibuka upya na matapeli wa ardhi kuanza kutembea vifua mbele

Mkuu na ww umeamua kuwa upande wa matapeli wa ardhi ambao usiku na mchana wanampiga vita Silaa na kumzushia uongo mbali mbali?
Bahati nzuri namfahamu vizuri sn Silaa, mtu wa maana alikuwa ni Lukuvi akapigwa vita na mafisadi
 
Sijasema wote, ila wengi wao, mfano wizara ya ardhi, lukuvi, na hata yulo slaa walijitahidi kiasi fulani, kulinganisha na wengine, lakini hawakudumu, nenda, wizara ya mambo ya ndani, afya, na jenista wanatembelea ngekewa tu
Ya nimekuelewa mkuu 😃😂
 
Niaje waungwana

Japo hakuna mtu mwenye dhamana ya kumpangia raisi kile anachoamua, lakini katika hili la kumtoa Silaa ardhi na kwenda kumtupa huko kwenye habari kwa kweli Rais wetu amefanya kosa la kiufundi sana.

Jerry alikuwa ashaanza kuwashughulikia vibaka na matapeli wa ardhi wote, yaani mmoja baada ya mwingine hadi kupelekea wengine kutupwa ndani. Sasa leo anapotolewa na kupelekwa wizara nyingine ni kuwapa nafasi wale wote waliokuwa washaanza kurudisha ardhi walizotapeli kabla kiama hakijawashukia waendelee nazo na pengine kuendelea kutapeli na zingine kwani aliekuwa anawapa tumbo joto kaondolewa na kupelekwa kungine.

Najiuliza, kwanini hiyo wizara ya habari asingepewa hata Mwana FA, ili Silaa aendelee kuwanyoosha wezi na vibaka wa ardhi za watu!

Anyway acha tuone mwisho wa game utakuaje. Lakini mama kama unatusikia na kufanikiwa kusoma uzi huu tafadhali TUNAOMBA (kwa herufi kubwa) UMRUDISHE JERRY SILAA W/ ARDHI 🙏🙏
watu wa sampuli hizi ndio ccmu wanawapenda
 
Attachments

  • 84629a3e6ea9add71c5ec3941d245808.mp4
    8.1 MB
Hata mimi ninahisi hivyo...pesa ni kama shetani,pengine Jerry alishakula kwa urefu wa kamba yake kama Makamba
kwan mnamuona mama yenu ni mtu mzur ? kuna kero gan kaishughulikia ? mama ashamuona dogo anajizolea umaarufu kaamua kumtulia kisomi , sasa huko kwenye habari si kama mtu katolewa Mpakani kapelekwa Mlimba akafie Mbele sababu alikuwa anazuia madili ya watu mipakani huko .
 
Huyo Slaa anapungukiwa na communication skills. Hiyo Wizara asingeiweza.
mwiz huwa mnatumia communication skills gan kumhukumu ? ifike muda muache utapeli na ufisadi na sio kutaka mupigiwe magoti kuombwa kuacha uhaini wenu kwa watu wa daraja la chini
 
Bahati nzuri namfahamu vizuri sn Silaa, mtu wa maana alikuwa ni Lukuvi akapigwa vita na mafisadi
tatizo lenu waswahili huwa mnaangalia maisha binafsi ya mtu na sio utendaj wake , kwa upuuz huu mzungu aliwatawala na sasa mwarab anarudi kiwatawala tena mpk mpate akilo ya kujua mnataka kiongoz mweny lifestyle utakayo au anaetimiza mahitaji yako ya msingi
 
Watanzania tusiwe shallow minded, ni Nini Cha maana amefanya huyu waziri, kuvunja nyumba za watu na kuzuia kituo Cha mafuta ndio ilikuwa hitaji la watanzania, kutokuweza kuongoza Wizara yake na kuacha miji kuwa holela na yeye kutokuwa na Plan ya mbeleni Ndio tumsifie Kwa lipi!? Jamani tuwe serious
Wale Watu wameanza kufurahia huku
 
tatizo lenu waswahili huwa mnaangalia maisha binafsi ya mtu na sio utendaj wake , kwa upuuz huu mzungu aliwatawala na sasa mwarab anarudi kiwatawala tena mpk mpate akilo ya kujua mnataka kiongoz mweny lifestyle utakayo au anaetimiza mahitaji yako ya msingi
Kama Kafulila ni mzalendo umewahi kumuona anapinga Mwarabu kuuziwa raslimali za nchi au ndiyo mpiga debe wa uuzaji? DP World alikuwa anashangilia kupita kiasi ndiyo uzalendo wake?
 
Niaje waungwana

Japo hakuna mtu mwenye dhamana ya kumpangia raisi kile anachoamua, lakini katika hili la kumtoa Silaa ardhi na kwenda kumtupa huko kwenye habari kwa kweli Rais wetu amefanya kosa la kiufundi sana.

Jerry alikuwa ashaanza kuwashughulikia vibaka na matapeli wa ardhi wote, yaani mmoja baada ya mwingine hadi kupelekea wengine kutupwa ndani. Sasa leo anapotolewa na kupelekwa wizara nyingine ni kuwapa nafasi wale wote waliokuwa washaanza kurudisha ardhi walizotapeli kabla kiama hakijawashukia waendelee nazo na pengine kuendelea kutapeli na zingine kwani aliekuwa anawapa tumbo joto kaondolewa na kupelekwa kungine.

Najiuliza, kwanini hiyo wizara ya habari asingepewa hata Mwana FA, ili Silaa aendelee kuwanyoosha wezi na vibaka wa ardhi za watu!

Anyway acha tuone mwisho wa game utakuaje. Lakini mama kama unatusikia na kufanikiwa kusoma uzi huu tafadhali TUNAOMBA (kwa herufi kubwa) UMRUDISHE JERRY SILAA W/ ARDHI 🙏🙏
Mama anashauriwa na matakataka! Yameoma Jerry Silaa ameyabana yameamua kumfitini kwa mama! Mama naye sijui hashughulishi ubongo?
 
Back
Top Bottom