Jerry Silaa kutolewa ardhi, tutarajie tena migogoro ya ardhi kuanza kuibuka upya na matapeli wa ardhi kuanza kutembea vifua mbele

Jerry Silaa kutolewa ardhi, tutarajie tena migogoro ya ardhi kuanza kuibuka upya na matapeli wa ardhi kuanza kutembea vifua mbele

Yule mzee aliyekuwa anajieleza kisha akamkatisha na kuita polisi wamkamate ni mwanajeshi?kwa hiyo unataka kusema yule mzee ndio ameenda kushitaki juu kwenye mfumo?
But anyway serikali yetu inafeli sana kuhamishahamisha watendaji hovyo yaani hawako strategic hata kidogo mtu ambaye alikuwa anafuatilia kwa ukaribu chanzo cha migogoro ya ardhi akawa anawashughulikia matapeli wanamtoa wanampeleka wizara nyingine ina maana kwenye Watanzania zaidi ya milioni 60 hakuna mtu wa kumuweka kwenye wizara ya habari na akafiti?
Ndio maana miaka yote tunarudi palepale.
Sasa hivi matapeli wa ardhi na nyumba wataanza kufanya sherehe
Fact
Hii sio sawa kabisa
Rais Samian sikuhizi mrudishe Jerry slaa
 
Ni mtendaji mzuri sana ila mm nahisi uligusa pabaya sana ila nakuamini na unataka kuweka hadharani ndio imekutoa hapo ulipo songa mbele hakuna upinzani ila ni ndani ya Ccm
 
Wizara ya ardhi sio ya kukurupuka.
Ni Wizara ambayo ili iende vizuri, jenga mifumo tu, basi. Ni kama ilivyo Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Ulinzi, au ya Fedha.
 
Tanzania yangu mizizi ya upigaji inaanzia jumba jeupe!

Sasa ikijifanya kuwashungulikia dagaa!! utashangaa kambale wenye ndevu wanakuonya kwa kuhamishwa wizara!

Raisii wa type ya Magufuli ndo ilikuwa kiboko yao
 
Tukio baya lililomwondoa ni kuvamia wakazi wa CCT Morogoro na kuwatisha wananchi kuwaweka ndani bila kosa wakati wakielezea changamoto za ardhi yeye akadata kwa ujeuri wa madaraka akamfukuza mwanajeshi aliyekuwa akijieleza kwa dharau na hasira akishirikiana na dada mmoja mweupe hivi
Very true
 
Tanzania yangu mizizi ya upigaji inaanzia jumba jeupe!

Sasa ikijifanya kuwashungulikia dagaa!! utashangaa kambale wenye ndevu wanakuonya kwa kuhamishwa wizara!

Raisii wa type ya Magufuli ndo ilikuwa kiboko yao
Itabidi tumwe keze Mama yetu anajua ni msikivu na anapenda mawazo yetu
 
Niaje waungwana

Japo hakuna mtu mwenye dhamana ya kumpangia raisi kile anachoamua, lakini katika hili la kumtoa Silaa ardhi na kwenda kumtupa huko kwenye habari kwa kweli Rais wetu amefanya kosa la kiufundi sana.

Jerry alikuwa ashaanza kuwashughulikia vibaka na matapeli wa ardhi wote, yaani mmoja baada ya mwingine hadi kupelekea wengine kutupwa ndani. Sasa leo anapotolewa na kupelekwa wizara nyingine ni kuwapa nafasi wale wote waliokuwa washaanza kurudisha ardhi walizotapeli kabla kiama hakijawashukia waendelee nazo na pengine kuendelea kutapeli na zingine kwani aliekuwa anawapa tumbo joto kaondolewa na kupelekwa kungine.

Najiuliza, kwanini hiyo wizara ya habari asingepewa hata Mwana FA, ili Silaa aendelee kuwanyoosha wezi na vibaka wa ardhi za watu!

Anyway acha tuone mwisho wa game utakuaje. Lakini mama kama unatusikia na kufanikiwa kusoma uzi huu tafadhali TUNAOMBA (kwa herufi kubwa) UMRUDISHE JERRY SILAA W/ ARDHI 🙏🙏
Kweli angeonywa tuu sio kuondolewa kabisa.
 
Watanzania tusiwe shallow minded, ni Nini Cha maana amefanya huyu waziri, kuvunja nyumba za watu na kuzuia kituo Cha mafuta ndio ilikuwa hitaji la watanzania, kutokuweza kuongoza Wizara yake na kuacha miji kuwa holela na yeye kutokuwa na Plan ya mbeleni Ndio tumsifie Kwa lipi!? Jamani tuwe serious
ok waambie wizara sio mtu ni system
 
Watanzania tusiwe shallow minded, ni Nini Cha maana amefanya huyu waziri, kuvunja nyumba za watu na kuzuia kituo Cha mafuta ndio ilikuwa hitaji la watanzania, kutokuweza kuongoza Wizara yake na kuacha miji kuwa holela na yeye kutokuwa na Plan ya mbeleni Ndio tumsifie Kwa lipi!? Jamani tuwe serious
Mtaje kwa jina ni Waziri gani aliyewahi kufanyia kazi mawazo hayo ya ndoto zako.
 
dah kiukwel nimewazq sana.slaa aliwaweza wizaran.kutwa alikua anashinda field. anayekuja ni big kweli kweli
 
Yaani hii nchi ukitaka upendwe
Furahisha Maboss (CCM)
Au furahisha wananchi bila kuwabugudhi vigogo
Lasivyo utaondolewa au kuhamishwa wizara huku unaambiwa Umefanya kazi nzuri sana

Kama kutoa kauli tata kunamfanya mtu atoke kwenye nafasi
Nadhani hata Sir100 hatoshi hapo
Yani mambo mengine yanasikitisha sana ki ukweli.
 
Mtaje kwa jina ni Waziri gani aliyewahi kufanyia kazi mawazo hayo ya ndoto zako.
Huyu uliemuuliza hawezi kukupa jibu la maana zaidi ya kubwabwaja tu bila ushahidi. Inaonekana ni mmoja wa matapeli ya ardhi ambayo hayataki kuona tukimpigania waziri Silaa arudishwe w/ ya ardhi.

Anajua Silaa akirudishwa huenda na yeye atafikiwa na kunyang'anywa viwanja vyote alivyowadhulumu wanyonge. Huku si kuleta mzaha katika wizara nyeti na ngumu kama hiyo!!
 
dah kiukwel nimewazq sana.slaa aliwaweza wizaran.kutwa alikua anashinda field. anayekuja ni big kweli kweli
Anaekuja kutoka ofisini tu kwenda msalani ni shida, je ataweza pilika pilika za kuingia mtaani kusikiliza kero za wananchi kweli!
 
Huwa unakesha humu JF halafu hujui kwamba nchi ni mifumo! Watu tumesema hapa Jerry hatengenezi mifumo, anafanya show binafsi, kisha anapata milungula. Sasa Wizara imebaki kama ilivyo, hakuna substantial system aliyotengeneza
Ushahidi wa kupokea mlungula uko wapi mkuu? Au na ww umekuwa miongoni mwa watu wanaookota maneno mitaani na kuleta humu bila ushahidi na facts za kueleweka?

Yani kwa uzoefu wako hapa jukwaani nilitegemea ungekuja na ushahidi wa hiki ulichoandika ili sisi wote tumuhukumu. Kumbe ni porojo za kisiasa tu ambazo zinaonekana hazina ukweli wowote.
 
Back
Top Bottom