Jerusalem: Sababu tatu za kuzuka kwa ghasia kati ya Wapalestina na Wayahudi

Jerusalem: Sababu tatu za kuzuka kwa ghasia kati ya Wapalestina na Wayahudi

Dunia nzima waislam akili zao ni moja wanawaza fujo mda wote kuua kuandamana kujitoa mhanga,
Kusingekuwepo uislam tungekaa kwa aman sana ila nashukuru mungu aliwapa nguvu Israeli, na wazungu maana wanashughulikiwa kisawa sawa very good
Cha ajabu Tanzania kunawaislamu na hawafanyi hayo je ww kwa akili zako unajiona uko sawa?

kasome kwanz uislamu ndo urudi kuandika

Maana hapo unaonekana hata uislamu wenyw huujui
 
Shida maeneo hawa watu vipi ? Waende hata jangwani huko wakaanzishe maisha mapya. Wote hao ni ndugu waamue mambo kifamilia zaidi
 
Nini chanzo cha haya yote, tangu tukiwa watoto mpaka sasa tu watu wazima tunasikia Israel, Palestina na ukanda wa Gaza, mara wakristo, wayahudi na waislamu, naomba mwenye habari kamili ya hii vita isiyo na mwisho atupe series yake

Hawa wakristo na wayahudi wanatofautiana wapi wakati wote asili yao ni hapo? Hawa wayahudi wanatofautiana wapi na wapalestina kama wote ndiyo wenye nchi?
Nasikia chanzo Cha yote hayo ni mkate wa dengu. Mtu aliuza haki ya uzaliwa wake wa Kwanza kwa mkate wa dengu, kuanzia hapo, mdogo akaanza kubarikiwa. Chuki na Vita vikaanza
 
Mkuu natamani sana kuijua hii historia maana huwa sielewi hao wapalestina walitokea wapi mpaka kwenda kuvamia nchi ya watu? Na wao waisrael walikuwa wapi mpaka wapalestina wanajenga mizizi
Israel nchi imeundwa 1940s

Baada ya UNO kugawa eneo l Palestine
 
View attachment 1781647

Hawa jamaa naona kama kila kitu utata, hata ramani haieleweki,
  • Palestina hapo iko wapi hapa kwenye ramani?
  • Ukanda wa Gaza nao ni upi?
  • Yordani nayo ni kama nchi lakini haina mji mkuu
  • Nani anagombania nini hapo?
1.Hakuna taifa linaloitwa Palestina ila kuna mamlaka ya kiuongozi ya Palestina ambayo inaongoza baadhi ya maeneo ndani ya Israel,ikiwa imeshikilia maeneo kama Bethlehem,Baadhi ya Maeneo ya Jerico,Gaza na maeneo kadhaa.
2.Yordani ni nchi kamili na mji mkuu wake ni Aman.
 
1.Hakuna taifa linaloitwa Palestina ila kuna mamlaka ya kiuongozi ya Palestina ambayo inaongoza baadhi ya maeneo ndani ya Israel,ikiwa imeshikilia maeneo kama Bethlehem,Baadhi ya Maeneo ya Jerico,Gaza na maeneo kadhaa.
2.Yordani ni nchi kamili na mji mkuu wake ni Aman.
Unaonekana hata history huijui nenda kasome history ya kuanzishawa kwa Israel
 
Unaonekana hata history huijui nenda kasome history ya kuanzishawa kwa Israel
Nimeongea uhalisia uliopo sasa,hakuna taifa linaitwa Palestina,hao unaowaita wapalestina wote wanatumia passport za Israeil na wako huru kuchangamana kwenye maeneo yenye wakazi wa Israeil tofauti na Waisrael ambao hawaruhusiwi kuingia maeneo yaliyoko chini ya mamlaka ya Palestina
 
Nimeongea uhalisia uliopo sasa,hakuna taifa linaitwa Palestina,hao unaowaita wapalestina wote wanatumia passport za Israeil na wako huru kuchangamana kwenye maeneo yenye wakazi wa Israeil tofauti na Waisrael ambao hawaruhusiwi kuingia maeneo yaliyoko chini ya mamlaka ya Palestina
Kasome history ya nchi hzo mbili na uweke udini pemben alfu ujekuona kma kuna haki inatendeka hapo
 
Kwani naaongea uongo,fuatiria masuala yote ya Imaani kwa kinachoendelea sasa hivi duniani,Selikali yote ya Saudia Arabia sasa hivi wako ndani ya Mwezi mtukufu wa Ramadhani,Ukija kwenye kwenye Ukristo utaukuta Roma,au labda unazani waisiraeli ni walokole kama wewe?
 
Unaomba historia kwa asiyejua historia pole sana,labda kwa kukusaidia baada ya Vita kuu ya pili ya Dunia walitaka waletwe East Africa Uganda Maana kabla ya hapo walikuwa hawana kwao walikuwa wametapakaa Dunia nzima,Inchi ya Israel imeasisiwa baada ya vita ya pili ya Dunia na waliwakuta Waparestina. Nitakupa na Stori ya kidini ili Uelewe sio kushabikia vitu ambavyo hamvijui kwa Miemuko ya Dini
 
Walikuwa kimya kumbe, wanachaji betri na kujaza mafuta, sasa naona wapo fit, zipigwe tu!
Assad apumzike huko Syria.
Ila Israel buana akirushiwa jiwe yeye anatupa kombora la masafa marefu kabisaa.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Acha ya uane tu wakati mababu zetu wanaenda kuunzwa utumwani hakuna ata mmoja wao apo alitutetea mimi naanzaje kuwa na huruma nao huruma mimi sina anayo Mungu tu.
 
Cha ajabu Tanzania kunawaislamu na hawafanyi hayo je ww kwa akili zako unajiona uko sawa?

kasome kwanz uislamu ndo urudi kuandika

Maana hapo unaonekana hata uislamu wenyw huujui
Waislamu wapi watz ambao hawafanyi hayo?

Ukikuwepo enzi za utawala wa JK wewe?

Unafikiri wale mashehe waliopo mahabusu ni kwasababu wavaa kanzu ndio maana wako pale?

Unaikumbuka ishu ya kuchinja iliyotokea kule mwanza na kuanza kusambaa nchi nzima?

Magufuli ndio alikuja kuwakomesha ila tulikuwa tunaelekea huko huko.
 
Kasome history ya nchi hzo mbili na uweke udini pemben alfu ujekuona kma kuna haki inatendeka hapo
Historia yao naijua vizuri na nimeisoma kwa pande zote,Ukirudi kwenye historia ni lazima imani za kidini ndio zihusike,kwa hivyo nikiangalia kwenye misingi ya dini.Taifa la Israeli lina wakazi jumuishi ambao wayahudi ni 75%,waislamu ni 17%,wakristo ni 2%,wasamalia,wabahai na imani ndogo ndogo wao ni 6% na wanaojimbulisha kama wapalestina ni takribani 60%ya waislamu,43% ya wasamalia,32%ya wakristo na 6% Ya Wayahudi.Hapo utaona jinsi wayahudi walivyo wameza hao wengine kwa idadi na ndio watawala wenyewe nguvu kwa miaka mingi maeneo hayo huku wakimilki idadi kubwa ya ardhi .Kwa hiyo nikifuata misingi ya dini lazima Imani kubwa hapo ni wayahudi na ndio watawala wa miliki yote ya Israeli kama taifa na Palestina inabaki mamlaka ndani ya Israeli.
 
Wa
Ghasia zilizuka nje ya msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa zamani wa Jerusalem

REUTERS: Ghasia zilizuka nje ya msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa zamani wa Jerusalem

Jerusalem imekuwa ikigonga vichwa vya habari kufuatia ghasia ambazo zimekuwa zikiripotiwa mjini humo kati ya Wapalestina na vikosi vya usalama vya Israeli ambazo zimewaacha mamia wakijeruhiwa mbali na mshambulizi ya kulipa kisasi kutoka pande zote mbili yakiripotiwa.

Ghasia hizo ziliongezeka siku ya Jumatatu usiku baada wanamgambo wa Kipalestina kurusha roketi kutoka ukanda wa Gaza hadi Jerusalem.

Kundi la wanamgambo la Hamas limetishia kuwashambulia maafisa wa polisi wa Israel baada ya mamia ya Wapalestina kujeruhiwa katika eneo takatifu la Waislamu mjini Jerusalem siku ya Jumatatu.

Likijibu, Jeshi la Israel lilifanya mashambulizi ya angani dhidi ya ngome za wanamgambo katika ukanda wa Gaza.

Maafisa wa afya wa Palestina katika eneo la Gaza wanasema kwamba watu 22 wakiwemo watoto waliuawa katika shambulio hilo.
Jeshi la Israel limesema kwamba takriban wanachama 15 wa kundi la Hamas linalotawala Gaza ni miongoni mwa waliokufa.

Roketi zilirushwa kutoka Gaza hadi Jerusalem siku ya Jumatatu

REUTERS: Roketi zilirushwa kutoka Gaza hadi Jerusalem siku ya Jumatatu

Siku ya Jumanne, Shirika la haki za kibinadamu la Palestina Red Crescent, liliripoti kwamba zaidi ya Wapalestina 700 walijeruhiwa katika ghasia hizo na maafisa wa usalama wa Israel mjini Jerusalem na eneo la West Bank.

Hizi hapa sababu tatu zilizopelekea kuzuka kwa mzozo huo.

1. Siku ya kusherehekea Jerusalem​

Jerusalem imeshuhudia ghasia ambazo hazajiwahi kutokea tangu wikendi ya 2017, zikisababishwa na jaribio la muda mrefu la Wayahudi kujaribu kunyakua nyumba za familia za Kipalestina katika eneo lililonyakuliwa na Israeli la mashariki mwa Jerusalem.
Ghasia hizo za Jumatatu zilizuka nje ya msikiti wa Al Aqsa , katika mji wa zamani wa Jerusalem.

Wapalestina waliwarushia mawe maafisa wa polisi wa kukabiliana na ghasia kutoka Israel ambao nao walijibu kwa kuwarushia risasi bandia za mipira na vitoa machozi .

Shirika la haki za kibinadamu la Palestina Red Crescent lilisema siku ya Jumatatu kwamba zaidi ya watu 300 walijeruhiwa.

Vikosi vya polisi vya Israel vilisema kuwa idadi kubwa ya maafisa wa polisi ilijeruhiwa pia.

Zaidi ya Wapalestina 300 walijeruhiwa wakati wa ghasia za siku ya Jumatatu

Zaidi ya Wapalestina 300 walijeruhiwa wakati wa ghasia za siku ya Jumatatu

Msikiti wa Al Aqsa upo katika eneo takatifu linalojulikana na Waislamu kama Haram al Sharif, na Hekalu la Mlimani kwa Wayahudi.
Vikosi vya polisi wa Israel vilisema kwamba maelfu ya Wapalestina waliweka vizuizi katika eneo hilo wakitarajia kutokea kwa ghasia wakati wa maandamano ya Kiyahudi siku ya Jumatatu ili kuadhimisha siku ya Jerusalem.

Maandamano hayo yanaadhimisha hatua ya Israel kunyakuwa eneo la mashariki la Jerusalem 1967 , wakati wa vita vya siku sita ambapo ilifanikiwa kuchukua udhibiti wa mji wote.

Mji huo wa zamani upo mashariki mwa Jerusalem , ikiwa ni nyumbani kwa baadhi ya maeneo matakatifu ya kidini duniani ikiwemo:

Msikiti wa Al-Aqsa, Hekalu la mlimani, Ukuta wa magharibi wa dini ya Wayahudi na kanisa la Wakristo la mtakatifu Sepulcher.

Na eneo hilo linatambulika kuwa mji mtakatifu na Wayahudi, Wakristo na ni mji wa tatu mtakatifu katika Uislamu.

Hatma ya eneo la Jerusalem mashariki ndio kiini cha ghasia kati ya Israeli na Wapalestina na kila upande unapigania haki yake.

Israel inasema kwamba eneo lote la mji huo ni mji wake mkuu , ijapokuwa hilo halitambuliwi na jamii ya kimataifa , na Wapalestina wanadai kwamba eneo hilo ndio mji mkuu wa taifa la Kipalestina litakaloundwa katika siku zijazo.

Wakati wa maandamano hayo ya kuadhimisha siku ya Jerusalem, mamia ya vijana wa Israel walipeperusha bendera na kuelekea katika maeneo hayo ya Waislamu , wakiimba nyimbo za kizalendo.

Wapalestina wengi wanachukulia hatua hiyo kama uchokozi.

Polisi wa Israel walitembelea eneo hilo kuamua kuwapiga marufuku Wayahudi wakati wa maadhimisho ya siku ya Jerusalem.

Maandamano ya kuadhiisha siku ya Jerusalme yanaadhimishwa kufuatia hatua ya Israel kunyakua mji huo

Maandamano ya kuadhiisha siku ya Jerusalme yanaadhimishwa kufuatia hatua ya Israel kunyakua mji huo

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alitetea ulinzi uliowekwa.

"Hii ni vita kati ya wavumilivu na wasio na uvumilivu, kati ya wasiofuata sheria na wanaofuata sharia," alisema.

"Wale wanaotaka kuchukua haki zetu mara kwa mara hutulazimisha kusimama kidete, kama maafisa wa polisi wa Israeli wanavyofanya."

Kwa upande wake rais wa Palestina Mahmoud Abbas alishutumu vitendo vya Israel.

"Shambulio la kinyama la vikosi vya Israel dhidi ya waumini waliokuwa katika msikiti mtakatifu wa Al Aqsa na maeneo yake ni changamoto mpya kwa jamii ya kimataifa," alisema msemaji wake Nabil Abu Rudeineh.

2. Uwezekano wa kuzifurusha familia za Wapalestina

Wimbi jipya la ghasia linatokana na juhudi za siku nyingi za Wayahudi kuzifurusha familia kadhaa za Kipalestina kutoika katika makazi yao karibu na wilaya ya Sheikh Jarrah mashariki mwa jerusalem.

Jerusalem ilishuhudia ghasia mbaya zaidi tangu 2017

Jerusalem ilishuhudia ghasia mbaya zaidi tangu 2017
.​

Umauzi wa mahakama mwaka huu uliounga mkono kufurushwa kwao ulizua shutuma kutoka kwa Wapalestina.

Mahakama ya kilele nchini Israel ilikuwa inatarajiwa kusikiliza kesi siku ya Jumatatu lakini kikao hicho kikaahirishwa kutokana na ghasia hizo.

3. Hali ya hofu wakati wa Ramadhan

Wimbi hili la ghasia linajiri katika siku za mwisho za mwezi mtukuafu wa Ramadhan.

Kizuizi cha Ramallah

Hofu ilitanda tangu kuanza kwa mwezi wa Ramadhan katikati ya mwezi Aprili , huku kukiwa na msururu wa matukio ambayo yamesababisha ghasia.

Wakati Ramadhan ilipoanza , ghasia za usiku zilizuka kati ya polisi na Wapalestina wakipinga vizuizi vilivyoweka nje ya lango kuu la Damascus katika mji wa zamani wa Jerusalem ambalo lilikuwa limewazuia kukongamana eneo hilo usiku kucha.

Lakini ghasia hazikutokea Jerusalem pekee kwani sehemu nyengine pia zilirekodiwa katika mji wa Haifa , Kaskazni mwa Israel na mji wa karibu wa Ramallah katika eneo la West Bank.

Wapatanishi wa mashariki ya kati , wakiwemo Marekani, muungano wa Ulaya, Urusi na Umoja wa Mataifa wameonyesha kukerwa na ghasia hizo na kutoa wito kwa pande husika kuvumiliana.

CHANZO: BBC Swahili
Wanauana wenzao wanakaa mezani wanapiga pesa alafu wanajiita wapatanishi, katika hii dunia ukikosa akili ni shida sana lazima watu wakutumie kama kitega uchumi, Kwani nini wasikubaliane namna ya kukaa pamoja,
 
Hao jamaa ni ndugu ugomvi wao wa kikuda sana yaani hata hawaeleweki eleweki wanataka Nini yaani watu wanaishi nchi moja ila wamegawana madaraka kila mtu anajifanya mjuaji kwa zaidi ya mwenzie

Waacheni Kama walivyo akili zao ni nusu hao!
 
Mkuu natamani sana kuijua hii historia maana huwa sielewi hao wapalestina walitokea wapi mpaka kwenda kuvamia nchi ya watu? Na wao waisrael walikuwa wapi mpaka wapalestina wanajenga mizizi
Kwa Kifupi sana, Waisrael Zamani walitekwa na kwenda kutumikishwa nchi zingine kama ulaya nk, kama Waafrika walivyofanywa, na wapalestina ni kama wamasai walivyoingia kenya na nchi nyingine.
 
Back
Top Bottom