Jesca Magufuli: Wadogo zetu wanalipiwa ada ya chuo na Rais Samia

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Wakati akifanya mahojiano na Millard Ayo hivi karibuni, Jesca Magufuli ameeleza kuwa Rais Samia Hassan ameendelea kuwa na mchango mkubwa katika familia yao.

Ameeleza kuwa bado anaendeleza matibabu ya bibi yao ambaye amekuwa akiugua hata kabla John Magufuli hajafariki. Aidha wadogo zao waliokuwa chuo bado wanaendelea kulipiwa ada na Rais.
Your browser is not able to display this video.
 
Huyu Jesca huko BOT hakumtoshi? Hadi atake ubunge tena?
Pension za baba ake, zinafanya nn hadi watoto walipiwe na Rais? Mafao ya mjane yanaenda wapii?

Akae kimya bhana, hatutaki kupatwa na hasira waja. Lol
 
Wakati watoto wa Ben Saanane na Azory Gwanda wanawaza na kuamini ipo siku watawaona tena baba zao maana hawajui hata uko walipo ni hai au wafu.

Ni mtanzuko wa fikra kwa familia ya Akwelina wasijue wala kuamini binti yao hayupo tena kwa makosa ya mtawala mwendawazimu.

Hizi interview za huyu binti ni stage managed kumuandaa na safari ya kisiasa hivyo mimi siwezi kuingia kwenye huo mtumbwi .

Maovu aliyoyafanya baba yao ni beyond repair na wala simlaumu ni mfumo mbovu wa nchi umeshindwa kuyaibua mengi .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…