Swali ni moja tu, IRAN ATATUMIA SILAHA GANI KWENDA MAREKANI KUSHAMBULIA?
Jibu na fafanua, konakona za nini? Si mseme tu hizo silaha Iran hakuna?
Iran hana silaha ya au missile inayojulikana mpaka sasa ya kufika USA, but missile kufika USA sio ndio kumnkomesha USA.
Unapaswa kujiuliza kwa nini USA hataki kutoka middle East?
Kwa sababu ya economic interests.
Kwa sababu ya kuweza kuendesha uzalishaji na usambazaji wa mafuta duniani kwa kutumia dollar ili iwe yenye thamani(strongest) zaidi duniani.
Kuzifanya nchi za kiarabu ziwe weak ili Israel iwe king mashariki ya kati na ku dominate nchi zingine, remember Israel ipo chini ya USA.
Kumbuka hata Sadam alipigwa kwa sababu alitaka kuanza kufanya biashara ya mafuta kwa pesa zinginena sio dollar, USA wakaona huyu jamaa anatumaliza, wakammaliza.
🙂.
Sasa baada ya kujua kwa nini USA hatoki middle east tuangalie. je Iran kuikomesha USA ikome kabisa anahitaji kurusha missile kwenda kupiga New-York? au Washington DC?
Jibu ni Hapana, Iran atampiga USA pigo ambalo hata angeomba apigwe intercontinental ballistic missile angeona ni ahueni kuliko kumfukuza middle east.
Huo ndio ukweli, Iran wapo vizuri mno tena saaana, kwa kweli accuracy ya zile missile kutua kwenye zile kambi za USA ni ya kustahajabisha katika historia, hata USA wenyewe hawakutegemea, guess what? ilikuwa ni warning, kwamba tuna uwezo wa kupiga kambi zote za USA middle East within minutes if not seconds with highest accuracy.
Kumbuka Iran haitaki USA awe pale, siku USA akibugi atajua apambane na Iran uchumi wake udorore au akubali kutoka middle east uchumi wake pia udorore😂😂, ndio maana alipigwa missiles kwenye zile kambi na kuharibu vifaa vyenye thamani ya 2 billion dolars, ila alitulia tu, kama mgonjwa anayepimwa tezi dume.
Iran wapo smart sana wale jamaa, wana uwezo na walisema wana uwezo wa kunda kombora la kufika USA but wanaweka range within middle east, na ninajua kambi zote za USA zipo targeted muda wote yaani ni ku push button tu.
Kwa maana majibu walijibu haraka sana,sasa jiulize wali test hio accuracy wapi?
Ripoti inamnukuu mkuu wa Mlinzi mwenye nguvu ya Mapinduzi ya Iran, Jenerali Mohammad Ali Jafari, akisema: "Tuna uwezo wa kisayansi kuongeza umbali wa kusafiri wa kombora zetu , lakini sio sera yetu ya sasa."
Mwa Jafari aliongezea maadui wengi wa Irani tayari wako ndani ya eneo la kilomita 2,000 (1,240-mile).
Mnamo mwaka wa 2017, Kiongozi Mkuu wa Irani Ayatollah Ali Khamenei aliamuru mipaka juu ya mpango wa kombora la shambulio la nchi hiyo kwa kilomita 2000.
Iran haihitaji Intercontinental Ballistic Missile ambazo kutakuwa na uwezekano mdogo wa kufika USA kwa sababu mpaka hapa NATO wana ushirikiano katika Ballistic Missile Defense System, ambapo nchi zote za NATO wana shirikiana na kusaidiana juu ya shambulio lolote lile la missile.
Wana infra red satellite zitakuwa zina track missile tokana na joto inalotoa, Then taarifa zinatumwa kwenye ground stations zote zilizopo kwenye nchi zote za NATO, then wanakuwa wanajadili kwenye NATO headquarters kufahamu kama ni missile,
wakiona ni missile wanatuma taarifa sasa kwenye command centres zote na weapons systems pia radars kama ile ya USA an/tpy-2 , pia kuna kuwa na sea based radars, zote hizo zinaangalia missile moja na kuifuatilia, jinsi radar zinavyofuatilia missile ndivyo accuracy inaongezeka at the same time kuna kuwa na mawasiliano na systems zoote, then wanaweza ku intercept missile nje ya atmosphere,
Kumbuka wana ushirikiano, missile ikionwa na satellite nchi zooote zinakuwa alerted,
So Iran sio wajinga, tunawatandika tu hapo hapo middle east mpaka mkimbie. 😂 😂
ICBM zenyewe USA kazitumia kwenye vita ipi zikamsaidia? tusiwe tunatajiana tu ooooh ina range ya 15000km za kwenye mdomo.
USA kupigana na Iran hana budi kusogea middle East kuweka kambi, usifikiri wanawaza kama wewe eti wakae nyumbani wawe wanatuma hayo ma ICBM, binafsi i beleive kwenye hizi medium range kwa sababu naona kazi zinazofanya,mfano mzuri zilizotua Iraq.