Niweke mambo sawa tu.
Iran inaogopwa sana na tuangalie kwa nini inaogopwa?
Toka mwaka 1979 Iran wanaivimbia USA huku wanaitazama USA usoni,licha ya vikwazo vikali imezidi kuwa na vikundi vya kijeshi middle east ikiwemo Lebanon,Syria,Iraq na sasa Yemen.
Kwa maana moja niseme Iran middle East ameiweka kiganjani.
Ukizungumzia vikwazo kwa Iran sio mambo mageni, Iran imewekewa vikwazo ni zaidi ya miaka 40 sasa huku miaka 30 mfululizo ikiwa ni vikwazo vikali zaidi lakini USA ameamua kucheza karata yake ya mwisho hapo 2019 kwa kuongeza sanctions [emoji23] [emoji23] .
Licha ya Iran kuwa chini ya vikwazo katika huo muda wote wametengeneza ndege vita kama Saeqi ambayo ina uwezo mkubwa wa radar, pia ina uwezo mkubwa wa kutazama ramani chini, avionics mpya na pia wanaweza kuzizalisha kwa wingi.
Kngine ni kwamba jeshi la Iran lina nguvu sio mchezo, wana nguvu katika middle east kuwazidi Saudi ,Bahrain na hao Israel hio iko wazi.
Kumbuka nchi inaipiga drone ya USA kama vile RQ 4 na pia RQ 170 na pia ilisha wateka askari wa marekani, kupiga hizo drone na hazijarudishwa kwenda USA, so jiulize nchi gani nyingine itaweza hivyo?
Iran imeisaidia Syria kuendelea kusimamisha uongozi wao pia Russia imetoa msaada wake.
Wamewamaliza ISIS nchini Iraq na sasa tazama Houthi wa Yemen wanazidi kujitanua zaidi na mliona Saudi ilifanywa nini kwenye vile visima vya mafuta.
Yote hayo yanatokea mbele ya macho ya USA.
Licha ya Iran kutopata msaada wa kijeshi ulimwenguni, waliweza kuindoa Iraq katika eneo lake ndani ya miezi michache mno, kumbuka kuwa wakati huo wakati wa mapinduzi uwezo wake wa kijeshi ulipungua, vifaa vya kijeshi viliharibiwa na hao wakandarasi wa magharibi kabla ya kukimbia, kumbuka hio vita Iran mapinduzi yamefanyika 1978 hadi 1979 na mwaka huo huo Iraq ikisaidiwa silaha bora toka magharibi, askari na pesa toka mataifa mengi ya kiarabu, nchi za ulaya na USA, Licha ya silaha bora toka USA na USSR, Iraq ilipewa msaada wa kifedha na hata silaha za sumu toka kwa wazungu,intelejensia za ku target lengo likiwa kuimaliza kabisa Iran amabayo si muda walikuwa wamefukuzia mbali uongozi ambao ulikuwa ni wa ukandamizaji toka USA.
Lakini Iran ilipambana kiume kwa miaka 8, bila kuomba poo wala samahani, mpaka Sadam akaanza kupiga sumu, what? USA alishika kichwa.(Hii story nitaandaa uzi maalumu kusimulia jinsi gani Iran iliweza kuhumili hii vita licha ya kuwa na uhaba wa silaha na kukosa msaada)
Ndio nasikiaga humu wapuuzi wanasema USA hajaamua, eti akiamua anaimaliza Iran, niwacheke kwanza, kama waliishindwa Iran ya 1979 wataiweza Iran ya leo?
Licha ya kuwa chini ya vikwazo vibaya zaidi katika historia kwa miongo minne, Iran imekuwa inaendeleza uwezo wake katika nuclear, imekuwa na uwezo mkubwa kisayansi kiasi cha kushangaza, sayansi kiwango cha juu mashariki ya kati ukiwatoa Israel inayopewa msaada na USA na mwenzake Saudia.
Iran ina akiba kubwa mno ya mafuta na gesi,utajiri wa madini pia hivyo jamaa wapo vizuri, juzi hapa wamesafirisha mafuta meli 5 toka Iran mpaka Venezuela, USA imebaki ina tazama tu.[emoji23]