Jeshi la Israel (IDF) lakanusha kuhusika na Shambulio la hospitali huko Gaza

Yani waweke Video alafu waiondoe bila watu wengine kuidaka.... Wewe unaishi ulimwengu gani, yani uposti kitu mtandaoni kinachofatiliwa na watu wengi alafu kikae dakika kadhaa ukifute bila watu kukichukua.... Kama ni kweli walipost kisha kufuta video ingekwisha sambaa...

Pili HAMAS sio kundi la kuchukulia poa poa wale jamaa wana silaha nzito nzito, ndio maana waliweza kufanya mashambulizi mazito kwa Israeli... Hizo roketi unazozizungumzia nenda kaziangalie huko YouTube, zinaweza kusafiri mji hadi mji, yani mtu yuko mwanza anatungua Dodoma... Ndio walichokuwa wanafanya wanatungua Tel-Aviv kutokea Gaza... Wewe akili zako unahisi Hamas wana bunduki tu na vikombora vya kutungua maembe... Wale wazee wako Vizuri, ndio maana pia kwa Israel imekuwa ngumu kuwatuliza, ingekuwa ni hizo silaha unazozungumzia wewe HAMAS wangekuwa wameshatulizwa....
 
.
 
Ndiyo maana balozi wa Palestine UN kakutana na wanahabari na kaonesha video na tweets za Israel,na kasema Israel walisema toka mwanzo kwamba tokeni mahospitalini which means hospitals ni target,siku za uwongo wa Israel zimekwisha,mitandao ya kijamii inawatafuna,tofauti na zamani CNN na BBC tu ambao hawatoi maovu ya Israel, Hamas hawana bom moja la kuua watu 600,acha uwongo,na Wala Israel hawakusema Hamas Bali Islamic jihad na ni roketi moja lililoenda sivyo,rocket ya Islamic jihad haiwezi ua watu 600 na kubomoa ahli baptist hospital
 
Lakini la ki-Israel linaweza?
 
Uwezo wa roketi kuua watu 500 hai justify muhusika ni nani, hizo silaha za Hamas unafahamu zinakotokea?
Tuongee kisayansi,roketi ya Islamic jihad inaweza watu 500 na kubomoa completely hospital!?..balozi wa Palestine UN kakutana na wanahabari na kaonesha video na tweets za Israel
 
Islael inauwa watu hadi muda huu wameua watu 4000 nusu ya vita ya urusi na ukraine ina maan wakiongeza miez miwili washavuka mgogoro wa urusi na ukraine

Islael ni taifa la hovyo.

Magaidi washughulikiwe Hamna namna! Hamas wamejificha nyuma ya raia na kuwafanya ngao unategemea nini zaidi ya civilian casualties
 
Kwanza unafahamu kuwa HAMAS wanatumia Binadamu kama ngao yao kujilinda na mashambulizi ya Israel... Hamas wanachokifanya ni kwenda maeneo yenye kuhifadhi watu kama mashuleni, misikitini, mahospitalini kisha kufanya mashambulizi ya makombora, hili endapo Israel wakijibu mashambulizi waonekane wanapiga na kuua watu.... Yani HAMAS wanachofanya sasa hivi ni kuhakikisha Israel analaumiwa juu ya raia... Sasa kama HAMAS anapenda wapalestina kwa nini hawatoe kama chambo kwa manufaa yake... Kwa nini HAMAS anakataza raia wasitoke, kwa nini asiende yeye kama yeye vitani mpaka awe na raia
 
Hili ni swali la kijinga sana ulilouliza... Silaha ziko sehemu nyingi sana Duniani, kupata silaha sio shida... Al-shabab tu hapo wanapata Silaha, Sembuse Hamas ambao wanasapotiwa na IRAN na nchi zote za uarabuni.
Acha kutetea ujinga mkuu hamas hana silaha zenye uwezo mkubwa kiasi hicho cha kuuwa watu 500.
 
Mkiambiwa ni taifa teule na ni urithi wa Mungu mnabisha. Makombora yenu yanawarudia wenyewe
Isaya 19:25
kwa kuwa BWANA wa majeshi amewabariki, akisema, Wabarikiwe watu wangu Misri; na wewe Ashuru, kazi ya mikono yangu; na wewe Israeli, urithi wangu.
 
Siyo rahisi hivyo israel ifanye shambulio kama hilo ukizingatia kuna ujio wa Biden hapo Tel Aviv, nina wasiwasi kama sio bahati mbaya (misfire) ya Hamas basi kuna uhuni umefanyika kutibua ziara za biden hapo middle east.
Pitia twitter utagundua ilikuwa uongo maana wanaposema pamepigwa bomu hakuna chochote kinachoonesha bomu limepigwa,majengo yote yamesimama, magari tu ndo yameungua
 
True... Uwenda Hamas wali-misfire au kuna propaganda... Lakini HAMAS wamekaa kimya juu ya hili tukio
Hamas wanajua kuwa hakuna bomu linaweza piga sehemu na hiyo sehemu ikabakia nzima nzima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…