Maisha ya mwanadamu, hata angekuwa mmoja ni yenye thamani kubwa kwa kiasi kisichopimika kwa kigezo chochote kile. Ndiyo maana:
Tunalaani vikali ule uharamia uliofanywa na magaidi ya Hamas dhidi ya jamii ya Israel .
Lakini pia tunalaani mauaji hata ya mpalestina mmoja asiye na mkono wake ndani ya ugaidi ule wa Hamas uliotendwa dhidi ya Waisrael; sawa na tunavyoulaani utawala wa Rais Samia kukumbatia uovu unaofanywa na Jeshi la Polisi dhidi ya wananchi wasio na hatia, kwa kuwateka, kuwatesa, kuwaua na kuwapoteza.
Wapalestina walioshiriki uharamia dhidi ya Israel, kwa namna yoyote ile, kinachowapata ni halali yao, lakini maisha ya Wapalestina wasio na uovu wowote ule ni muhimu sana kulindwa.
Wapalestina siku watakapojitenga na mataifa gaidi ya kiarabu, wakarudi kwenye hekima, naamini wataishi kwa amani na ndugu zao Waisrael maana hawa ni ndugu wa karibu ambao uhasama wao unachochewa zaidi na mataifa ya Kiarabu, hasa Iran. Wapalestina wakijitenga na Iran, wakawa karibu na mataifa kama Saudia na Jordan, nina hakika huo mgogoro utaisha hata ndani ya mwaka mmoja.
Hofu kubwa ya Israel, kuwapa Wapalestina nchi ni kugeuzwa nchi hiyo kuwa makao ya magaidi yatakayokuwa tishio kwa usalama wa watu wake. Bila ya Iran, Wapalestina wapo tayari hata kuungana kikamilifu na kuwa Taifa moja na Israel, linalotambua na kuzingatia haki za wananchi wa jamii zote. Kabla ya ugaidi wa Hamas, maelfu ya Wapalestina, baadhi walikuwa wakiishi na kufanya kazi Israel, wengine walikuwa wakifanya kazi Israel na kurudi Gaza. Hawa wote sasa wamefukuzwa kwa kuhofia kuwa huenda baadhi yao wapo na kundi la kigaidi la Hamas.