Ni eneo la kimakati lililowaumiza Israel vichwa kwa muda mrefu, kilele cha mlima Hermon kiliwapa advantage kubwa Syria na Hezbollah kuichunguza na kuishambulia Israel.
Israel imetwaa eneo hili bila pingamizi katika kile kinachodhaniwa "hakuna kitu cha Bure", Israel waliweza kutoa msaada mkubwa wa kudhoofisha majeshi ya Assad kwa kufanya mashambulizi ya anga kwenye kambi za Assad, msaada huu umechangia pakubwa waasi kuitwaa nchi, hivyo wamewapa eneo hili la kimkakati kama "Asante"
Faida kwa Israel kuchukua udhibiti wa kilele cha Mlima Hermon
Kilele cha Mlima Hermon ni mahali pa juu kabisa, kinachowezesha Israeli kufuatilia harakati za kijeshi za Syria na Hezbollah kutoka mbali.
Mahali hapa pa juu hufanya kuwa vigumu kwa adui kushambulia Israeli moja kwa moja bila kutambuliwa.
Israel inaweza kusakinisha mifumo ya hali ya juu ya rada na vifaa vya mawasiliano kwa ajili ya kuchunguza harakati za vikosi vya adui, mizinga, makombora, au ndege zisizo na rubani.
Movement za Hezbollah za kusafirisha silaha kutoka Syria kwenda Lebanon au mipango ya uvamizi zinaweza kufuatiliwa mapema.
Kilele hiki kinatoa nafasi nzuri ya kijeshi kulinda mipaka ya kaskazini ya Israel, hasa kutoka kwa shambulio lolote la anga au ardhini.
Milima ya Hermon ni njia muhimu ya usafirishaji wa silaha kati ya Syria na Hezbollah. Udhibiti wa Israel utaifanya kuwa vigumu kwa wapinzani kutumia njia hiyo.
View attachment 3172549