Jeshi la Kenya dhidi ya M23: Je, Kenya itaweza kufanya kile ilichofanya Tanzania mwaka 2013?

Uganda aliwapa hifadhi waasi mwaka 2015, leo anakwenda kupambana nao aliowapa hifadhi, kwanini hakuwamaliza kipindi amewahifadhi? Au hili ni igizo?
Ukweli ni kwamba Uganda ndio Rwanda na Rwanda ndio M23, kwahiyo anaefikiri kuwa Uganda imekwenda kupambana na M23 anajidanganya mwenyew akili yake.
 
Usisahau tulikwenda kuokoa kisiwa kimoja huko karibu na Mtwara
Ya ni kweli mkuu, hapo nilikuwa nimetaja tu kwa uchache. Kisiwa chenyewe kinaitwa Comoro ambacho kipo chini ya himaya yetu, japo wanajitawala wenyewe.
 
Masase masase..bhamutu bhana kimbia kumiji yao.

#MaendeleoHayanaChama
Baache bachukue muyi muzima, alakini basichukui muziki yetu ya kiliwanzenza, ile njo ambianse yetu batu ba Congo.
 
Vipi Kenya hawajaanza kuwavurusha hao M23?
Jeshi la Kenya limejificha nyuma ya migongo ya jeshi la Congo kwa kisingizio cha kupokea maelezo ya vita. Walichokishuhudia na kukiona Kenya maeneo yale kimewafanya wafikirie mara mbili ni namna gani wanaweza kuwapokonya silaha waasi hao.

Maana wanasilaha nzito nzito na vijana hodari sana kwa mapambano ya ardhini.
 

Tanzania tulisambaratisha vipi wakati jamaa bado wapo na wanasumbua? Au maana ya kusambaratisha ni nini?
 
Tanzania tulisambaratisha vipi wakati jamaa bado wapo na wanasumbua? Au maana ya kusambaratisha ni nini?
Kusambaratisha maana yake ni kuwatimua watu maeneo husika. Ni mfano wewe ukute watoto watukutu wanacheza na mtoto wako, wewe uamue kutumia ukubwa na ubabe wako kuwatimua au kuwafukuza wale watoto watukutu, ila baada ya wewe kuondoka wale watoto watukutu warudi tena kwa style ile ile baada ya kujua kwamba wewe sasa haupo.
 
Vita tamu sana hii,kitakachoifanya ikose utamu wake Ni Marekani na Ulaya kuingilia kwa kutishia kuweka vikwazo na blah blah blah za ICC kwa M23& Supporters wake lkn nilitamani Sana kuona jinsi KDF wanavyokula kichapo kitamu mchana kweupe.
Kweli kabisa, yale matamko ya magharibi huenda yakawavunja nguvu kwa namna fulan M23. Ila kama watakwenda vita ya mtu mbili kwa mtu mbili Kenya lazima atolewe kamasi.
 
Na kwa kiherehere Cha KDF kujifanya wanataka Sana hio mission na kutaka ukuu wa hio operation naona bongo ilishtuka mapema yenyewe ikabaki kwny vikosi vya FIB Brigade.
 
Kweli kabisa, yale matamko ya magharibi huenda yakawavunja nguvu kwa namna fulan M23. Ila kama watakwenda vita ya mtu mbili kwa mtu mbili Kenya lazima atolewe kamasi.
Hao mkuu Ndio wataharibu kabisa utamu kamili wa hili varangati,kwa kulazimisha M23 wa-withdraw afu KDF iseme imepata ushindi wa mezani.

Wangeacha zipigwe kwanza tujionee kwny mbinu za kimedani hali ikoje.
 
Tanzania tulisambaratisha vipi wakati jamaa bado wapo na wanasumbua? Au maana ya kusambaratisha ni nini?
Ile ilikuwa mission maalum ya Monusco ambayo ni kati ya order chache UN wanaruhusu matumizi ya nguvu. Baada ya mafanikio JWTZ imerejea kwenye kulinda amani sio kuingia vitani na makundi ya waasi.

Kenya wameenda vitani kupitia mlango wa EAC. Kwangu ni jaribio la kwanza la kivita Jeshi la Kenya wanakutana nalo ambalo ni complicated. Kama ni M23 wale wale kimbinu na vifaa ( kivuli cha RDF) basi tusishangae aibu kwa jeshi la Kenya ambalo lina uzoefu mdogo wa gorilla war.
 
Na kwa kiherehere Cha KDF kujifanya wanataka Sana hio mission na kutaka ukuu wa hio operation naona bongo ilishtuka mapema yenyewe ikabaki kwny vikosi vya FIB Brigade.
Kenya ilikuwa wanawasikia tu hao vijana kupitia taarifa za habari, ikajua kwamba ni wepesi kivile. Lakini baada ya kufika kwenye uwanja wa mapambano na kujionea wenyewe, sasa wanashindwa kujua wafanyaje maana ndo tayari washafika on front na dunia au Afrika sasa inawaangalia wao watachofanya kwa vijana hao.
 
Hao mkuu Ndio wataharibu kabisa utamu kamili wa hili varangati,kwa kulazimisha M23 wa-withdraw afu KDF iseme imepata ushindi wa mezani.

Wangeacha zipigwe kwanza tujionee kwny mbinu za kimedani hali ikoje.
Kwa sasa kuna vijana wengi wa kisomali wanakwenda kupigana upande wa M23 ili kuwasaidia ndugu zao dhidi ya adui yao mkubwa Kenya.

Ikumbukwe Kenya ni adui mkubwa wa alshabab (somalis) na pia kihistoria watutsi na somalis ni jamii moja. So mpaka hapo vita itakuwa tamu.
 
Jeshi la Kenya hawajawahi kupigana vita kwenye mazingira ya misitu mikubwa na migumu kama ya Kongo. Unapigana na watu waliozaliwa na kukulia kwenye hiyo misitu!

Ni jaribio kwa KDF ambalo mabwana vita wa ukanda huu wametega sikio kutokana na uzoefu mdogo wa jeshi la Kenya kwenye vita vya msituni! Pengine hata kuhusisha Uganda lengo ni kuchota uzoefu wao kwenye misitu ya Kongo.

Meja General (mstaafu) Mwakibolwa atakuwa na cigar yake anaangalia majirani wanatokaje na hii mbugi [emoji2]
 
😄😄 Sasa hapo ni ukikaa nchale ukisimama nchale,itabidi wapigane nao tu maana itakua aibu wasipopigana nao,mbwembwe walioingia nazo Congo zilikua za hatari..

Hao M23 Jana wamesema wamesitisha mapigano,lkn hawatatoka kwny maeneo waliyoyashikilia na wakishambuliwa na jeshi la Kenya then watajibu mashambulizi ipasavyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…