Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bila hata Sheria za kimataifa ni Nani Kati Yao ana uchumi wa kupigana Vita?Nchi maskini hizo zingepambana kutafuta Maisha Bora kwa wananchi wake tu.Sheria za kimataifa haziruhusu hilo, labda ipangwe mbinu ambayo dunia haitoweza kuitambua kiurahisi.
Watume magaidi au wamuundie makundi ya waasi au magaidi kama walivyomuundia Gadafi na SaddamSheria za kimataifa haziruhusu hilo, labda ipangwe mbinu ambayo dunia haitoweza kuitambua kiurahisi.
Kama jeshi la Kenya lilishindwa kuwadhibiti vijana wawili pale katika uvamizi wa maduka ya east gate mchana kweupe na camera zikiwa wazi, je wataweza kuwadhibiti maelfu ya vijana walioshiba mazoezi, wenye mioyo migumu iliyotoboka na isiyojali chochote kuhusu kufa au kuishi.Jeshi la Kenya hawajawahi kupigana vita kwenye mazingira ya misitu mikubwa na migumu kama ya Kongo. Unapigana na watu waliozaliwa na kukulia kwenye hiyo misitu!
Ni jaribio kwa KDF ambalo mabwana vita wa ukanda huu wametega sikio kutokana na uzoefu mdogo wa jeshi la Kenya kwenye vita vya msituni! Pengine hata kuhusisha Uganda lengo ni kuchota uzoefu wao kwenye misitu ya Kongo.
Meja General (mstaafu) Mwakibolwa atakuwa na cigar yake anaangalia majirani wanatokaje na hii mbugi [emoji2]
Mkuu inaonekana wewe sio mfuatiliaji wa mambo yanayoendelea katika nchi za East Afrika.Watume magaidi au wamuundie makundi ya waasi au magaidi kama walivyomuundia Gadafi na Saddam
Kenyata na Ruto wamewaponza watoto wa wenzao 🤣🤣🤣😄😄 Sasa hapo ni ukikaa nchale ukisimama nchale,itabidi wapigane nao tu maana itakua aibu wasipopigana nao,mbwembwe walioingia nazo Congo zilikua za hatari..
Hao M23 Jana wamesema wamesitisha mapigano,lkn hawatatoka kwny maeneo waliyoyashikilia na wakishambuliwa na jeshi la Kenya then watajibu mashambulizi ipasavyo.
Twitter Kule wakenya kibao wanasema jeshi Lao lirudishwe nyumbani 😄😄,huku Wacongo nao Twitter wakilalamika wakisema walidhani KDF wakifika tu watawatoa wahuni wa M23 lkn wanashangaa kuwaona KDF huko Kwny mahotel ya Goma wakila Maisha na totozi tu.Kenya na Ruto wamewaponza watoto wa wenzao 🤣🤣🤣
Sidhani kama ni muda muafaka kuuliza swali lako. Ulivyoliweka ni kwamba nia yako ni kulinganisha uwezo wa jeshi la Kenya na la Tanzania. Muda huu inabidi tuelekeze juhudi zetu katika kuondoa uasi unaozifanya nchi za Afrika kupoteza muda na mali katika migogoro isiyo na kichwa wala mkia badala ya kujikita katika kuleta maendeleo ya nchi.Inakuaje brothers and sisters,
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Leo ndio siku ya mwisho waliopewa waasi wa Congo ili kusalimisha silaha zao kwa serikali, kinyume na hapo hatua kali za kijeshi zitachukuliwa kwa kundi lolote la waasi ambalo limekaidi amri hiyo. Na oparation hiyo itahusisha majeshi ya Afrika mashariki kutoka Burundi, Congo, Uganda na Kenya huku Kenya ikionekana kuongoza oparation hiyo ambayo kundi kuu la waasi nchini Congo la M23 likisema kwamba haliitambui oparation hiyo na kwamba yeyote atakaethubutu kwenda kuwachokoza katika maeneo yao wata deal nae.
Tusisahau kwamba mwaka 2013 nchi za Malawi, South Africa zikiongozwa na jeshi la Tanzania ambalo lilisimamia oparation zote za chini ziliweza kulisambaratisha kundi hilo la M23 katika kipindi kifupi cha week kadhaa tu, na kusababisha waasi hao kukimbia ng'ome zao na kuacha silaha zao na kwenda kuomba hifadhi katika nchi jirani za Rwanda na Uganda.
Sasa baada ya miaka 9 ya ile oparation kabambe iliyoongozwa na Tanzania, leo waasi hao wamerudi tena kwa kasi ile ile huku Kenya ikionekana kutaka kuchukua nafasi ya Tanzania ili kurudisha tena amani katika maeneo hayo ya mashariki mwa Congo.
Sasa tukiachana na hizi nchi zingine zilizoshiriki au zinazoshiriki katika oparation hizo kama vile SA, Malawi, Burundi na Uganda.
Swali langu je Kenya itaweza kufanya kile ilichofanya Tanzania?
Au jeshi lake linakwenda kupokea kichapo kile inachopokea serikali ya Congo?
Lets wait to see what's gonna happen. Maana yamebakia masaa matano tu ule muda waliyopewa waasi uishe.
God bless Congo,
God bless Tanzania,
God bless our continent Africa.
Thank you 🙏
Uchumi wa Rwanda unategemea zaidi vita vinavyoendelea huko Congo.Bila hata Sheria za kimataifa ni Nani Kati Yao ana uchumi wa kupigana Vita?Nchi maskini hizo zingepambana kutafuta Maisha Bora kwa wananchi wake tu.
Leo wamepeleka troops zingine Goma! Wanajipanga tu isitokee aibu! Ukiona jambo TZ wamejikalia pembeni ogopa [emoji2]Twitter Kule wakenya kibao wanasema jeshi Lao lirudishwe nyumbani [emoji1][emoji1],huku Wacongo nao Twitter wakilalamika wakisema walidhani KDF wakifika tu watawatoa wahuni wa M23 lkn wanashangaa kuwaona KDF huko Kwny mahotel ya Goma wakila Maisha na totozi tu.
Kwa upande wa wakenya washajua fika kwamba ndugu zao wamepelekwa kuuwawa kwa faida ya viongozi waliopo madarakani.Twitter Kule wakenya kibao wanasema jeshi Lao lirudishwe nyumbani 😄😄,huku Wacongo nao Twitter wakilalamika wakisema walidhani KDF wakifika tu watawatoa wahuni wa M23 lkn wanashangaa kuwaona KDF huko Kwny mahotel ya Goma wakila Maisha na totozi tu.
Ya ni kweli mkubwa, wote tunaomba amani itawale katika ukanda wetu wa Afrika mashariki.Sidhani kama ni muda muafaka kuuliza swali lako. Ulivyoliweka ni kwamba nia yako ni kulinganisha uwezo wa jeshi la Kenya na la Tanzania. Muda huu inabidi tuelekeze juhudi zetu katika kuondoa uasi unaozifanya nchi za Afrika kupoteza muda na mali katika migogoro isiyo na kichwa wala mkia badala ya kujikita katika kuleta maendeleo ya nchi.
😄😄 Kama Western wasipoingilia kwa kutishia vikwazo na blah blah nyingine then Kenya inaweza kupatwa na aibu isiyoitegemea mkuu.Leo wamepeleka troops zingine Goma! Wanajipanga tu isitokee aibu! Ukiona jambo TZ wamejikalia pembeni ogopa [emoji2]
Hebu tuwekee hapa records kuonyesha uchumi wa Rwanda ulitetereka kwa kiasi gani kuanzia kile kipindi cha 2013 ambako M23 walibondwa na kuachia maeneo hayo mpk hii majuzi walipoanza kupigana tena ili tuone ktk kipindi hicho chore Cha miaka 8 uchumi wa Rwanda ulikuaje.Uchumi wa Rwanda unategemea zaidi vita vinavyoendelea huko Congo.
Yale maeneo yanayodhibitiwa na M23 yana utajiri mkubwa wa rasilimali, kwahiyo Askari wa Rwanda wanaingia kimya kimya wanachukua rasilimali na kupeleka nchini kwao na baadae kusafirisha katika nchi zinazohitaji hizo rasilimali kwa bei chee.
Congo isha setiwa kabla hata ya uhuru ili ije kuwa shamba la bibi kwa wakubwa kutoka dunia ya kwanza waje kujichotea na kuondoka. Kwa maana hiyo hakuna mtu wala nchi itakayoweza kuleta amani pale Congo
Waasi walipokimbia usidhani kuwa walikimbia mikono mitupu, wanaweza kuwa waliacha migobole lkn wakakimbia na dhahabu, almasi na rasilimali zingine ambazo zilikuwa rahisi kwao kubeba. Na nchi ambayo iliwapokea kwa wingi hao vijana ni Rwanda ikifuatiwa na Uganda.Hebu tuwekee hapa records kuonyesha uchumi wa Rwanda ulitetereka kwa kiasi gani kuanzia kile kipindi cha 2013 ambako M23 walibondwa na kuachia maeneo hayo mpk hii majuzi walipoanza kupigana tena ili tuone ktk kipindi hicho chore Cha miaka 8 uchumi wa Rwanda ulikuaje.
Maana miaka yote hio ya 2013-2022 hao M23 wakiwa wamenyang'anywa hayo maeneo bado hao Rwanda walikua Kwny fastest growing economy in Africa na Wala hawakutetereka.
Dialogue ndio itamaliza mgogoro huo na kulijenga upya Jeshi la Kongo ili liwe na uwezo wa kulinda mipaka yake bila kuhitaji usaidizi.Ulichoandika ni ukweli, hii vita ni ngumu na haiwezi kumalizwa kwa mikwara ya jeshi la Kenya lililojaa wanajeshi wenye vitambi.