Jeshi la Kenya dhidi ya M23: Je, Kenya itaweza kufanya kile ilichofanya Tanzania mwaka 2013?

Jeshi la Kenya dhidi ya M23: Je, Kenya itaweza kufanya kile ilichofanya Tanzania mwaka 2013?

Askari tunaopeleka ni kwa ajili ya kwenda kuwafunza Jeshi la Kongo jinsi ya Upiganaji na nidamu ya Jeshi sio kama walivyo sasa Askari yuko Frontline amelewa chakari na ana simu mkononi anasikiliza miziki.
Wale jamaa mambo wanayoyapenda Ni ya kukata mauno tu,mambo ya kijeshi wanalazimishwa tu 😄
 
Inakuaje brothers and sisters,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Leo ndio siku ya mwisho waliopewa waasi wa Congo ili kusalimisha silaha zao kwa serikali, kinyume na hapo hatua kali za kijeshi zitachukuliwa kwa kundi lolote la waasi ambalo limekaidi amri hiyo. Na oparation hiyo itahusisha majeshi ya Afrika mashariki kutoka Burundi, Congo, Uganda na Kenya huku Kenya ikionekana kuongoza oparation hiyo ambayo kundi kuu la waasi nchini Congo la M23 likisema kwamba haliitambui oparation hiyo na kwamba yeyote atakaethubutu kwenda kuwachokoza katika maeneo yao wata deal nae.

Tusisahau kwamba mwaka 2013 nchi za Malawi, South Africa zikiongozwa na jeshi la Tanzania ambalo lilisimamia oparation zote za chini ziliweza kulisambaratisha kundi hilo la M23 katika kipindi kifupi cha week kadhaa tu, na kusababisha waasi hao kukimbia ng'ome zao na kuacha silaha zao na kwenda kuomba hifadhi katika nchi jirani za Rwanda na Uganda.

Sasa baada ya miaka 9 ya ile oparation kabambe iliyoongozwa na Tanzania, leo waasi hao wamerudi tena kwa kasi ile ile huku Kenya ikionekana kutaka kuchukua nafasi ya Tanzania ili kurudisha tena amani katika maeneo hayo ya mashariki mwa Congo.

Sasa tukiachana na hizi nchi zingine zilizoshiriki au zinazoshiriki katika oparation hizo kama vile SA, Malawi, Burundi na Uganda.

Swali langu je Kenya itaweza kufanya kile ilichofanya Tanzania?

Au jeshi lake linakwenda kupokea kichapo kile inachopokea serikali ya Congo?

Lets wait to see what's gonna happen. Maana yamebakia masaa matano tu ule muda waliyopewa waasi uishe.

God bless Congo,
God bless Tanzania,
God bless our continent Africa.

Thank you 🙏
Kenya inawamudu vizuri mno hao mamluki wa Rwanda..
Moronight walker mtu chake
 
Wale jamaa mambo wanayoyapenda Ni ya kukata mauno tu,mambo ya kijeshi wanalazimishwa tu 😄
Nimewaona Askari wa M23 wako well trained na wananidhamu ya hali ya juu na wana inteligence ya hali ya juu huenda hata kwenye hilo jeshi la Kongo wana "Batu" wao wanaowapa full information za Movement za Jeshi la Kongo na reinforcement zinazokuja😆😂
 
Hii ndo itatumika kuingiza silaha,, Rwanda na uganda ni landlocked, wanategemea bandari ya dar au mombasa,, ikitokea wakawekewa vikwazo vya kuingiza silaha,,
Zitaingia kwa aircargo
😄😄 Silaha wanazopitishia kwny hizo Bandari Ni zile za kawaida tu, Rwanda silaha zao wanatumia dege la jeshi Qatar C-130 kusafirishia,hata kupeleka vifaa vya kijeshi Mozambique walitumia ndege hio,Drones zile za Turkey kuzileta kigali wametumia ndege za Uturuki,na last week flight radar24 imeonyesha ndege za kijeshi ya mizigo ya nchi ya Israel zimetua Kigali karibu Mara 4 nadhani Kuna silaha zimepelekwa pale.
 
Uganda aliwapa hifadhi waasi mwaka 2015, leo anakwenda kupambana nao aliowapa hifadhi, kwanini hakuwamaliza kipindi amewahifadhi? Au hili ni igizo?
Hili suala la M23 ni mchezo wa siasa za ukanda tu (geopolitics) ..ndio maana kuna wakati hali inatulia na baada ya muda inachafuka sana
 
Yule huwa ana mikwala tu,mkwala aliompiga jk na tz tungekua maboya tungenywea,tukafanya tuliyofanya na akaja kuyajenga na mkwere
PK anaijua Congo zaidi ya waijuavyo wacongo wenyewe. Kumbuka hao M23 washatumika katika nafasi tofauti tofauti tena nyeti kule Congo. Kwahiyo aliposema hivyo kwa Tshisekedi alikuwa anajua anachomaanisha, hii ni tofauti na ule mkwara wa Tanzania maana system ya Tanzania ni tofauti na system ya nchi nyingi za Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla. Ndio maana mpaka leo tupo salama.

Na kwa kulijua hilo JK alitamba kwa kuwaambia watanzania walale usingizi mnono na ikibidi hata waache milango wazi hadi asubuhi, hakuna panya yeyote atakaejaribu kuja kutushambulia iwe kwa upande wa Rwanda, Malawi wala Msumbiji.

Na kweli nchi nyingi za Afrika zinasema kuwa Tanzania iko strong kwa upande wa intelejensia hasa kuhusu swala la usalama wa mipaka.

Tanzania ni kama Marekani, viongozi wengi wa ukanda huo sisi ndio tumewaweka, hata hao wahutu wa Burundi kuwa leo katika serikali ni kwa sababu ya msaada mkubwa wa Tanzania, halikadhalika M7 na wengine ambao haina haja ya kuwataja.

So tunawafahamu ki nje ndani na tunajua ni jinsi gani ya kuwadhibiti pale wanapotaka kuleta kiburi.

Ila kwa upande wa Congo PK anafahamu hadi mahali anapoendaga kuoga Tshisekedi, na muda ambao huwa anakwenda kulala nk.
 
Ile ilikuwa mission maalum ya Monusco ambayo ni kati ya order chache UN wanaruhusu matumizi ya nguvu. Baada ya mafanikio JWTZ imerejea kwenye kulinda amani sio kuingia vitani na makundi ya waasi.

Kenya wameenda vitani kupitia mlango wa EAC. Kwangu ni jaribio la kwanza la kivita Jeshi la Kenya wanakutana nalo ambalo ni complicated. Kama ni M23 wale wale kimbinu na vifaa ( kivuli cha RDF) basi tusishangae aibu kwa jeshi la Kenya ambalo lina uzoefu mdogo wa gorilla war.

Guerilla War hakuna fundi wake, kwa sababu unapigana na watu wanaojificha kwenye raia
 
Kenya wameenda vitani kupitia mlango wa EAC. Kwangu ni jaribio la kwanza la kivita Jeshi la Kenya wanakutana nalo ambalo ni complicated. Kama ni M23 wale wale kimbinu na vifaa ( kivuli cha RDF) basi tusishangae aibu kwa jeshi la Kenya ambalo lina uzoefu mdogo wa gorilla war.
Sio kweli.....Alshabaab ni complicated na hatari ila Kenya imemudu muziki wao
 
Nimejaribu kuwafuatilia M23 sana nimegundua sio wale wa 2013 sasa hivi wana silaha Nzito na wako well organized nimeona wakishambulia possitions za Jeshi la DRC kwa Grad Missille launchers.
 
Back
Top Bottom