PK anaijua Congo zaidi ya waijuavyo wacongo wenyewe. Kumbuka hao M23 washatumika katika nafasi tofauti tofauti tena nyeti kule Congo. Kwahiyo aliposema hivyo kwa Tshisekedi alikuwa anajua anachomaanisha, hii ni tofauti na ule mkwara wa Tanzania maana system ya Tanzania ni tofauti na system ya nchi nyingi za Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla. Ndio maana mpaka leo tupo salama.
Na kwa kulijua hilo JK alitamba kwa kuwaambia watanzania walale usingizi mnono na ikibidi hata waache milango wazi hadi asubuhi, hakuna panya yeyote atakaejaribu kuja kutushambulia iwe kwa upande wa Rwanda, Malawi wala Msumbiji.
Na kweli nchi nyingi za Afrika zinasema kuwa Tanzania iko strong kwa upande wa intelejensia hasa kuhusu swala la usalama wa mipaka.
Tanzania ni kama Marekani, viongozi wengi wa ukanda huo sisi ndio tumewaweka, hata hao wahutu wa Burundi kuwa leo katika serikali ni kwa sababu ya msaada mkubwa wa Tanzania, halikadhalika M7 na wengine ambao haina haja ya kuwataja.
So tunawafahamu ki nje ndani na tunajua ni jinsi gani ya kuwadhibiti pale wanapotaka kuleta kiburi.
Ila kwa upande wa Congo PK anafahamu hadi mahali anapoendaga kuoga Tshisekedi, na muda ambao huwa anakwenda kulala nk.