Hao wanaoisema KDF hawajui JW ilipigwa ambush hapo Congo na tukapata vifo vya wanajeshi wetu. Au tarehe 15 hapo Mozambique si tulipigwa ambush JW wakakimbia. Nimesoma huu uzi mwanzo nikaona nisichangie, wanaichukulia KDF kama jeshi la Burundi sijui.
Na ingetokea KDF waende wenyewe tu au waende na South Africa na Malawi kama sisi ili kuwe na fair comparison. KDF wako vizuri kuanzia kwenye silaha, mafunzo na teknolojia, hata maonyesho yao siku ya uhuru yalinganishe na East African countries.
Hawa hapa wako na hand launched drones kufanya reconnaissance kwenye mission hiyo
View attachment 2428719
Ndugu umeweka picha na maelezo marefu lkn tayari ishaonesha kuwa huna unalolijua kuhusu namna mambo ya kijeshi yanavyokuwa. Sasa tulia nikupe somo kidogo huenda nikakutoa tongo tongo zilizopo machoni.
Ni hivi, Mwaka 2013 Tanzania tukishirikiana na Malawi pamoj na SA tulikwenda Congo kwa lengo la kuwapokonya silaha kwa nguvu, na kuwatimua katika ngome zao waasi wote ambao walikaidi agizo lililotolewa na nchi za SADC la kuweka silaha chini. Na kwa vile lengo la kupeleka jeshi letu kule ilikuwa ni kuwanyang'anya silaha kwa nguvu na kuwatimua, basi tulipofika kule hatukuleta maneno mengi kama yanayoletwa na askari wa Kenya sasa.
Sisi tulipofika tu maeneo husika kazi ikaanza bila kuongeza hata dakika moja na oparation ilikuwa kabambe sio ya kitoto hadi kupelekea waasi hao pamoja na wale wa Uganda na Burundi kukimbia ngome zao, wengine kujisalimisha na wengine kukubali kuweka silaha chini hata baada ya muda waliopewa kupita.
Baada ya oparation ile ambayo ilikuwa chini ya SADC, Tanzania na nchi zilizoshiriki oparation ile zikaunganishwa katika kikosi cha Umoja wa Mataifa ambacho kipo kule kwa lengo la kuwalinda raia.
Sasa basi ukiangalia mambo ya kijeshi utagundua kwamba hapo kuna mambo mawili tofauti. Nayaandika hapo chini kwa namba.
1) Oparation ya SADC ilikuwa ni ya kwenda kupambana moja kwa moja na waasi ili kuwanyang'anya silaha na kuwatimua katika ngome zao (Guerrilla War). Hii oparation iliwaruhusu kutumia silaha yoyote kulingana na uzito vita wanayopigana na UN haikuwa na uwezo wa kuingilia oparation ile.
2) Hii ya pili ni ya peacekeeper ambayo kazi yake ni kuwalinda raia dhidi ya mashambulizi ya waasi, hii ya peace keeper huwa mnapewa silaha hafifu na huongozwa kwa sheria za UN ambazo hazimruhusu askari kumfuata adui alipo na kuacha position yake ya kuwalinda raia. Ndio maana askari wengi (sio wa Tanzania peke yao) wanaoendaga kwenye mambo ya peacekeeper huwa wanauwawa sana kutokana na sheria mbovu za Umoja wa Mataifa. Hii ni tofauti na sheria za hapo juu namba 1.
Tukija kwa Kenya, yenyewe imekwenda kwa mgongo wa EAC kama ilivyokuwa Tanzania kwa SADC, wanaruhusiwa kutumia mbinu yoyote kuwadhibiti hao waasi kama ilivyofanya Tanzania, cha muhimu wasiuwe tu raia.
Sasa cha kushangaza marufuku hiyo imeisha juzi saa 12, lakini mpaka leo hii siku ya tatu Kenya imeshindwa kuingiza jeshi kuwapokonya askari hao kwa nguvu kama ilivyofanya Tanzania.
Narudia tena, Tanzania haikuzidisha hata dakika moja. Ila Kenya ishazidisha siku 3 sasa bila kufanya lolote.