A
Anonymous
Guest
Baadhi ya Polisi wanatuibia sana, mara kumi kitengo cha kui-track simu ikipotea kiondolewe rasmi, sio uongo wala nini, mara zote tukiibiwa simu tunaenda kuripoti Polisi. Loss report kwanza kwenye vituo tunatoa zaidi ya Sh. 10,000 na kiukweli huwezi ku-report popote zaidi ya hapo.
Haya unatoa vithibitisho vyote kwamba simu ni yako. Wanakuomba uwape Sh 70,000, haya unalipa, cha ajabu unaanza kuzungushwa mpaka unachoka.
Kuna kipindi niliongea na jamaa yangu fundi simu akaniambia kuwa baadhi ya Polisi huwa ndio wanafatilia na wakizishika badala ya kumrejeshea mhusika, wanamuomba tena huyo mwizi awalipe hela ili wamuachie, hivyo wewe ukirudi kituoni mara zote unaambiwa haijapatikana.
Ni mara ya nne sasa nafanya hivyo, nafuatilia hatua zote na kulipia hiyo karibu laki na ni mfumo wa vituo vyote lakini sijawahi kupata simu.
Sasa si mara kumi tujuie hizo huduma hazipo kuliko kufanya huo utapeli.