Kutoka kwa Emmaus Bandekile Mwamakula
Ndugu Watanzania!
Usiku huu tumeongea na mawakili wasomi Dickson Matata na Hekima Mwasipu ambao ni mawakili wa Malisa GJ na Mhe Boniface Jacob na tumejulishwa yafuatayo:
1. Malisa na Boniface wanakabiliwa na tuhuma mbili ambazo ni uchochezi na kuleta taharuki kwa jamii kwa kuchapisha taarifa kuhusu kifo cha Robert Mushi aka Babu G kwa kulihusisha Jeshi la Polisi na kifo hicho wakati marehemu amefariki kwa ajali.
2. Walalamikaji ni Jeshi la Polisi wenyewe.
3. Usiku huu Polisi wamekwenda na Boniface nyumbani kwake Msakuzi, Dar es Salaam kwa ajili ya kumfanyia upekuzi.
4. Pia usiku huu, wamesha magari na kwenda na Malisa nyumbani kwao Moshi Kilimanjaro kwa ajili ya kumfanyia upekuzi.
5. Kuwa Polisi watawahoji watuhimiwa baada ya kuwafanyia upekuzi.
6. Kwamba taarifa zaidi kuhusu dhamana zao zitajulikana kesho baada ya kufanya upekuzi.
Sisi Askofu Mwamakula tunaendelea kufuatilia kwa karibu sana suala hilo kwa kuwa ni jambo linalogusa hisia za watu wengi na pia linabeba maslahi ya taifa na umma wote wa Watanzania kwa ujumla. Chimbuko la tuhuma hizo liko pia katika kurasa zao. Sisi Askofu pia tumeendelea kuwajuza watu kupitia ukurasa huu tangu jana.
Bado tunaendelea kuwaza kuwa kama ni kweli Jeshi la Polisi limetuhumiwa na watu hao, ni taasisi ipi huru itayokahoji na kuwachunguza Polisi wanaotuhumiwa kufanya hayo ambao Jeshi la Polisi linalalamika kuwa linasingiziwa?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 25 Aprili 2024; saa 4:09 usiku