Tarehe 23 April 2016, PAC iliomba Kuunda kamati ndogo kwa mujibu wa Kanuni ya 117 fasili 18 ili kufuatilia utekelezaji wa Agizo la PAC la bunge la 10 lililotolewa tarehe 23.10.2014 kwa Jeshi la Polisi Kuhusu utekelezaji wa Mradi wa kielektroniki wa utambuzi wa alama za vidole AFPIS
Msingi wa Agizo ni Ripoti ya CAG 2012/2013 kutokana na kutokukamilika na kutokufanya kazi ipasavyo kwa mradi huo.
Kazi ya Mradi huo ilikuwa ni kati ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya LUGUMI ENTERPRISES LIMITED.
Polisi waliagizwa Mitambo ifanye kazi ndani ya miezi sita.
CAG aliripoti tena utekelezaji kuwa AFPIS inafanya kazi katika vituo 14 tu kati ya vituo 108
Kamati ilimtaka katibu mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani alete taarifa ya utekelezaji. Katibu mkuu taarifa yake ikaonyesha mitambo imefungwa vituo 153 pamoja na makao makuu ya polisi tofauti na taarifa ya CAG ilivyosema. Kamati ikaomba kuhakiki kujiridhisha na kujionea, na kamati ndogo ikaundwa kuhakiki.
HADIDU REJEA – kamati ifanye uhakiki iwapo vilinunuliwa na kufungwa
kamati imemaliza kazi yake, Imeiwasilisha PAC na PAC imeijadili na kuikabidhi kwa Spika kama Kanuni zinavyotaka.
MATOKEO YA TAARIFA YA KAMATI
i. Kamati imejiridhisha kwamba VIFAA VIPO Vituo vyote 153 na makao makuu ukiacha kasoro zilizojitokeza.
ii. Kilichobaki ni vifaa hivyo kufanya kazi
iii.Nimekabidhi matokeo (maoni, Ushauri na mapendekezo) yote ya kamati kwa serikali
AGIZO
i. Serikali ihakikishe mfumo huu unafanya kazi ndani ya Miezi mitatu kutoka leo hii ili kuboresha uwezo wa jeshi la polisi.
ii. Maswala yote yaliyobainika kuwa na dosari za kiutendaji yapatiwe ufumbuzi haraka.
iii. PAC ihakiki maelekezo niliyoyatoa na baada ya uhakiki kamati itoe taarifa bungeni wakati wa uwasilishaji wa taarifa yake ya mwaka.
iv. Ninatarajia sasa swala hili litafika mwisho na CAG atafunga hoja yake baada ya kujiridhisha utekelezaji wa maagizo niliyoyatoa.