Jeshi la polisi latolea ufafanuzi tukio la bodaboda kusemekana kutekwa, wasema ni mhalifu aliyekuwa anatafutwa muda mrefu na polisi

Jeshi la polisi latolea ufafanuzi tukio la bodaboda kusemekana kutekwa, wasema ni mhalifu aliyekuwa anatafutwa muda mrefu na polisi

Ndugu zangu Watanzania,

Jeshi letu la Polisi Nchini limetoa ufafanuzi wa kina juu ya video mjongeo iliyokuwa ikisambaa mitandaoni ikionyesha dereva bodaboda au mtu mwenye pikipiki akikamatwa na watu waliovaa kiraia nakisha baadaye kupakizwa kwenye gari nyeusi na kuondoka naye.

Jeshi letu la polisi limesema tukio hilo lilifanywa na askari wetu kwa mtu huyo ambaye alikuwa ni mhalifu wa makosa mbalimbali ya uporaji kwa kutumia pikipiki.

Kwa hiyo watanzania tuache mihemuko na lawama na kutupa maneno yasiyo na ukweli. Tuwe watu wa subira na kushirikiana na vyombo vyetu vya ulinzi kupata taarifa rasmi.

View attachment 3245354
Vijana acheni tamaa za kuzidi mtakufa wengi sana hiki kipindi cha miaka 2025 mpaka 2045
 
Yangewakut ya kuwakuja , mje huku musoma mtumie njia hyo kama hajawa majivu wakamataji na Gari hyoo
 
Tii Sheria bila shuruti mambo kama haya hayakupati,uibe,uibe wake za watu unategemea nini
Huna akili wewe dada, hakuna anayesema wahalifu wasikamatwe tuna hoji kwanini wakikamata mtu wasitoe taarifa kwa uongozi wa mtaa au kwa watu waliokuwa karibu? huna maana kabisa. Husikii matukio ya utekaji? jinga sn ww mama
 
Yaan wewe hukishtukii kwamba watu wote wanapinga haukua utaratibu sahihi wa ukatamataji ila wew unaona ni sawa? Lucas Mwashambwa
Wapo sahihi kabisa na ninashangaa kwanini hawakuwa na kirungu cha kumregeza Miguu wakati analeta ubishi wake wa kukamatwa. Tii sheria bila shuruti. Nawachukia sana wahalifu na waporaji. Embu fikiria wewe uhangaike kwa jasho lako kutafuta mali fulani au kitu fulani halafu mtu anakuja anakuibia? Utajisikiaje? Mimi nasema walimkamata kistaarabu sana.
 
Huna akili wewe dada, hakuna anayesema wahalifu wasikamatwe tuna hoji kwanini wakikamata mtu wasitoe taarifa kwa uongozi wa mtaa au kwa watu waliokuwa karibu? huna maana kabisa. Husikii matukio ya utekaji? jinga sn ww mama
Acha kutukana watu matusi humu . Hili siyo jukwaa la vichaa na wendawazimu
 
Kuna mahali nimekataa wakamatwe? Ila wanakamatwa kwa kufuata taratibu?
Maana kuna miongozo ya police

Au hiyo miongozo haiwahusu?
Wewe omba Mungu majambazi yaije kukuvamia kukupora nyumbani kwako halafu ukipiga simu waje haraka wanakwambia tunamtafuta mjumbe wa nyumba kumi au wa serikali ya mtaa unaoishi atuthibitishie kwanza kama kuna hilo tukio ndio tuje tuwakamate

Ona tukio kama hili wahalifu wanafanya tukio halafu wanatoroka unataka polisi waombe kibali wapi

Hyvi vishetia vyenu uchwara bakini navyo kwenye majoho yenu

Wewe utakuwa jambazi

View: https://youtu.be/2jEczHaZ8Og?si=LMX0VyjGmAvb9Ig_
 
Huyo jamaa inawezekana ni mhalifu ndio maana anatetea wahalifu. Ngoja siku moja yamkute ya kumkuta ndio ataona umuhimu wa askari wetu.
 
Uzuri tumeona kwenye video. Huo haukuwa ukamataji, ulikuwa utekaji.

Ni vile tu hizo video zimeenda viral ndo wametoka ku confirm kuwa ni wao maana hakukuwa na namna yeyote na kukana.

Kutufanya wajinga ndo wanasingizia ulikuwa ukamati. Nchi ishakuwa failed state hii.
 
Mhalifu Apatiwe Wakili Tumuone Mahakamani Jumatatu mapema.

Sujapendezwa na Ukamataji Ule.

Kila nikikumbuka Filamu ya Kikenya ya Nairobi Half Life siamini polisi wenye mavazi ya kiraia. Ni possible alikuwa mhalifu lakini mhalifu anayetumiwa na polisi.
 
Back
Top Bottom