Ndugu zangu Watanzania,
Jeshi letu la Polisi Nchini limetoa ufafanuzi wa kina juu ya video mjongeo iliyokuwa ikisambaa mitandaoni ikionyesha dereva bodaboda au mtu mwenye pikipiki akikamatwa na watu waliovaa kiraia nakisha baadaye kupakizwa kwenye gari nyeusi na kuondoka naye.
Jeshi letu la polisi limesema tukio hilo lilifanywa na askari wetu kwa mtu huyo ambaye alikuwa ni mhalifu wa makosa mbalimbali ya uporaji kwa kutumia pikipiki.
Kwa hiyo watanzania tuache mihemuko na lawama na kutupa maneno yasiyo na ukweli. Tuwe watu wa subira na kushirikiana na vyombo vyetu vya ulinzi kupata taarifa rasmi.
View attachment 3245354