Jeshi la polisi latolea ufafanuzi tukio la bodaboda kusemekana kutekwa, wasema ni mhalifu aliyekuwa anatafutwa muda mrefu na polisi

Jeshi la polisi latolea ufafanuzi tukio la bodaboda kusemekana kutekwa, wasema ni mhalifu aliyekuwa anatafutwa muda mrefu na polisi

Ujinga ni mzigo ndugu yangu. Kulikuwa na ubaya gani, polisi mmoja anawatangazia wananchi kuwa, "Ndugu wananchi sisi ni polisi msiwe na wasiwasi tunamkamata huyu ni mtuhumiwa" Halafu anatoa kitambulisho kuna ubaya gani?
Tena wananchi wange wasaidia kumdhibiti, pia kama wangefanya hivyo ingewapa wananchi imani kubwa kwa polisi. Je wakija wahuni wengine kumchukua mtu kwa njia ile ya kihuni wananchi watatofautije ukamataji wa polisi na unyakuaji wa wahuni?
 
Ni mhalifu mkubwa sana na bila shaka hata yeye alijua sababu ya kukamatwa kwake.
Mkuu Ni mahakama pekee ina haki ya kusema huyu mtu ni mtuhumiwa au la kwa mujibu wa sheria, hapa Luka umepuyanga japo tuko pamoja kumkubali bimkubwa na kazi zake ambazo zimeonekana pakubwa na mayowe yameanzia kenya sasa wana bifu na sisi kila kitu!! Wanatuogopa mno hivi sasa hata kabla SGR haijafika kirumba na kisha ujiji!!

Hakika Maza anastahili mitano tena wala si uchawa bali ni uwezo mkubwa ameonesha.

Nilipanda SGR toka Moro nilipofika Dom nikaona abiria wengi wanashuka huku wanabubujikwa na machozi ya furaha kuwahi kufika.
 
Lucas ameufanya uchawa wake wa kisiasa kuwa ngao ya kujikweza

akijitosa katika bahari ya unafiki kwa kusifia mamlaka bila tafakuri

Ufuasi wake si wa itikadi….. bali wa maslahi binafsi….. ambapo anabadili misimamo kama kinyonga ili kuendana na matakwa ya wakubwa.

Katika ulimwengu wake, ukweli ni kile kinachompendeleza mwenye mamlaka, na uadilifu umesahaulika kwa gharama ya ulafi wa kijipatia fursa

Rubbish
 
Ingetokea mtu akaamua kuwagonga na gari wote hao akiamini ni watekaji kwa kumkamata mtuhumiwa kwa mazingira hayo mngesemaje juzi tu hapa dereva wa TRA alipigwa hadi kufa ninyi bado hamjifunzi tu mnadhani Smg moja inaweza kuwatuloza watu wenye hasira kali jifunzeni kukamata watu kwa weledi ya taaluma yenu.
 
Lucas ameufanya uchawa wake wa kisiasa kuwa ngao ya kujikweza

akijitosa katika bahari ya unafiki kwa kusifia mamlaka bila tafakuri

Ufuasi wake si wa itikadi….. bali wa maslahi binafsi….. ambapo anabadili misimamo kama kinyonga ili kuendana na matakwa ya wakubwa.

Katika ulimwengu wake, ukweli ni kile kinachompendeleza mwenye mamlaka, na uadilifu umesahaulika kwa gharama ya ulafi wa kijipatia fursa

Rubbish
Sasa hapa ndio umeandika nini? Ndio hoja iliyopo mezani hapa? Au una matatizo na mimi? Hoja hujibiwa kwa hoja na siyo porojo.
 
Back
Top Bottom