Jeshi la Polisi lazuia mkutano wa Mbowe, atakiwa kuripoti Polisi Kinondoni

Mjomba si ufiche ujinga kidogo,mbowe yuko dar kwa ajili ya kesi na karantin yao iliisha jana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani Yuko dar au dodoma?
Kama yuko dar,anaweza kuwekwa lokapu
 
Siasa bana, Mbowe anajua umuhimu wa kutokusanyika ndiyo maana hayuko Bungeni, na ndiyo maana walifanya mkutano wa chama kupitia mtandao.

Leo nini kimemtuma kutaka kutoka nje kwenda kuonana na waandishi?

Kwa nini asingerekodi halafu akawatumia waandishi au akaifanya live kupitia YouTube?

Nadhani alijua polisi watamzuia na ndicho alichokuwa anahitaji.
 
Hakuna sheria inayozuia mkutano wa kisiasa
Huo ni usanii wa Serikali inayoogopa kwa kuwa imechokwa
Sheria, sheria mpaka lini? Ilipotungwa ilielewa kuna Corona? Ni mtu mzembe tu ndo anahitaji kufanya mkutano enzi hizi za Webex, Zoom, youtube, nk. Hawezi kusema yake kupitia mitandao? Ni mzembe!
 
Sheria, sheria mpaka lini? Ilipotungwa ilielewa kuna Corona? Ni mtu mzembe tu ndo anahitaji kufanya mkutano enzi hizi za Webex, Zoom, youtube, nk. Hawezi kusema yake kupitia mitandao? Ni mzembe!
Mwenyekiti wa ccm alipoongea na waandishi huko chato naye ni mzembe?
 
Hakuna sheria aliovunja na hata kutokuwepo Dodoma bado hajavunja sheria na kama ni kumdai posho apewe document ya madai kutoka ofisi ya Bunge au wito wa madai kutoka mahakamani na akikaidi ndio akamtwe.

Hizi ni chuki tu kisiasa na hamna lingine.
 
Mbona kichwa cha habari ni tofauti na habari yenyewe
 
Waziri Mkuu jana alikagua ujenzi wa Jengo la Tume ya Uchaguzi Dodoma huku akiwa na rundo la watu mbali na waandishi wa habari ila hatukusia Polisi wakimzuia.
 
Bila Polisi ccm ni wepesi kuliko pamba
 
Akapimwe covid 19 kwanza. Pia Kama karantini imeisha aende bungeni Idodomya
 
Kwani siku 14 za quarantine zimeisha? Huyu Mbowe anatakiwa kushughulikiwa kisheria and accordingly!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…