Jeshi la polisi limebariki huu wizi Kariakoo?

Niliwahi kusimamishwa na jamaa hapo Karume akafanya kunipigisha stori kama ulivyosema. Hadi leo nilichokuwa najua ni kwamba alikuwa anatafuta namna ya kumpa sapoti katika biashara yake na nilijua wazi hanifahamu wala simfahamu ila ni mbinu tu ya kutafuta mteja. Hilo la kukaba ndio nalijua sasa hivi, na sikuwahi kuwaza kama kuna element za utapeli
 
mnaomaindi mimi kuleta hii hoja kwahiyo mnaona hili suala ni sawa au?yaan hamuoni kama ni tatizo?
 
Marehemu Zacharia na utajiri wake wote lakini alikuwa kila siku kabla hajaingia msikitini anakunywa juice ya kwenye madeli pale msikitini kitumbini nendeni mkaulize hata leo hii hayupo lakini mtaambiwa , sembuse watu wengine wa kawaida ??
huku mitandaoni bhana kila mtu anakunywa Juice Mac juice tu na misosi ya samaki samaki mlimani city,safi sana wakuu
 
Mwendo wangu nikiwa natembea aisee mpka awaze kunisimamisha tyr nishamaliza kilometer 3.
 
usisimame barabarani kwa kuitwa na mtu usiemjua, akikuita itikia ongea nae huku unatembea usimpe nafasi ya kusimama hata kama ni mlemavu
 
Hapo polisi asilaumiwe kama wewe unajua kabisa huyu kiumbe sijawahi kuonana naye ananizuga ilistory ziende wewe nawe unaenda hvyohvyo kwanini unywe juice yake? hyo nitamaa yako imekuponza, yupo kazini anatafuta pesa nahyo ndio ameona njia yake yake ya haraka kuuza juice. Huyo jamaa ataakipelekwa mahakamani hakuna sheria yakumtia hatiani. Ni ufala wako na tamaa zako ndio zitakuwa imekuponza.
 
kwa hiyo hawa jamaa hawana kosa au vipi
 
Kila jambo mnataka mamlaka ziwasaidie like B.O.T wakat pesa ulienda kopa mwenyewe,sijui polisi wakat ulisimama mwenyewe na kuongea na mtu usijemjua na juice unapokea...nk kichwan humo hamna ubongo wa kupambanua mambo white ni ipi na black ni ipi...

Endeleeni subiria wengine watatue matatizo yenu wakat na wao Wana matatizo Yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…