JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Muda mfupi baada ya RC wa zamani wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuandika mtandaoni kuwa kuna makundi matano yanamuwinda ili kumuua, Jeshi la Polisi limesema kama kweli ana hofu anatakiwa aende kutoa taarifa Kituo cha Polisi.
Akizungumza na Kipindi cha Jahazi cha Clouds FM, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema: “Raia yeyote wa nchi hii ana haki ya kutoa taarifa Polisi kama ni kweli na ni jambo ‘serious’.
“Mimi sijaliona hilo tamko lake, najua watu ambao wapo serious wanaenda Polisi. Siwezi kushauri kuhusu hilo, watu unaowaongelewa wana weledi, wanajua taratibu, na ninajua wanajua, kwanza siamini, wana maarifa ya kutosha.
“Hao watu unaowazungumzia wana maarifa ya kutosha kujua wafanye nini, kama hana imani basi ofisi za Serikali zingefungwa, kama watu wanakwenda afu wewe unasema huna imani, mtu mmoja akisema hana imani lakini robo tatu wakienda na kupata huduma nani tumfuate hapo,” Muliro.
Source: CLOUDS FM
Pia soma:
Paul Makonda: Kuna makundi matano yanataka kuniua, likiwemo wanaotafuta kulipa kisasi kwa Wasaidizi wa Magufuli