Jeshi la polisi Mbeya limewakamata watu watano kwa kuhusika na mchezo wa upatu wa LBL

Jeshi la polisi Mbeya limewakamata watu watano kwa kuhusika na mchezo wa upatu wa LBL

Hivi serikali inashindwa kufuatilia hizi kampuni za ponzi na kufahamu mapema kabla ya watu kutapeliwa?

Wa kuwajibishwa ni hao waliotoa kibali, ponzi unaielewa mapema hata kwa akili za kuvukia barabara...

Waliosababisha watu kutapeliwa ni hizo mamlaka zilizotoa kibali, wananchi waliamini hio kampuni kwa sababu waliona ni legit na inatambulika...

Sasa hapo wamemkamata huyo tapeli akitoka ana mabilioni yake kwenye account anaendelea kula maisha..
 
Vijana lukuki wa Chuo waliwekeza pesa za Boom huko LBL wakawa wanawavuta na wanachuo wenzao kwa mbwembwe nyingi huku wakiwa na ndoto za kununua magari na kufungua biashara kubwa baada ya kumaliza chuo.
HAKUNA PESA YA BILA JASHO
 
MBEYA: JESHI la Polisi mkoani Mbeya, linawashikilia watuhumiwa watano akiwemo Meneja wa Kampuni ya LBL Gerald Masanya ,31,
1740054114700.jpg
kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya upatu mtandaoni bila kuwa na kibali chochote ambapo ni kinyume na taratibu za kisheria.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Wilbert imeeleza baada ya kupata taarifa za uwepo wa Kampuni ya LBL Mbeya Media Limited kuwa inajihusisha na biashara ya upatu mtandaoni walianza kufuatilia kwa kushirikia na Maofisa kutoka Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mbeya na idara nyingine ambapo walifika maeneo ya Mwanjelwa na kuwakamata watumiwa hao.

Taarifa hiyo imewataja watuhumiwa hao ni Gerald Masanya ,31, ambaye ni Meneja wa Kampuni ya LBL-Mbeya, mkazi wa Nsalaga, Saphina Mwamwezi ,23, ambaye ni sekretari na mkazi wa Ituha, Edda William ,29, mkazi wa Uwanja wa Ndege wa Zamani, Yohana Mkinda ,29, mkazi wa Tukuyu pamoja na Macrine Sinkala ,23,.

Imeelezwa watuhumiwa kupitia kampuni hiyo wamekuwa wakijihusisha na biashara ya upatu mtandaoni na kueleza kuwa wamekuwa wakituma “link” maalum kwa wateja ili kujiunga mtandaoni na kisha wateja hutakiwa kulipa fedha kuanzia Sh 50,000/- hadi Sh 540,000/- na kutakiwa kuangalia matangazo ya “movies” mbalimbali zilizowekwa kwenye “Platform” hiyo kwa madai kwamba watapata faida baada ya kuwekeza fedha zao kwa kipindi fulani.

Imeandaliwa na DAILLY NEWS DIGITAL SWAHILI.
 
Back
Top Bottom