Wao wanapata faida gani kwa kutazama movie? Jiulize swali dogo, niliona wanawambia kuwa walikaribisha Tanzania na serikali kuja kuondoa umasikini?Hakuna biashara pale mkuu,,unachotakiwa kufanya ni kuweka 50,000 Hadi 540,000.
Kisha wao wanakutumia movies tano Kwa siku (trailer).unatakiwa uzitazame zote Kila clip inakuwa na sekunde 10 then wao wanakulipa 18,000 per day ikiwa umeweka 540,000.usipotazama wao wanakata 18,000 ktk Ile pesa yako
Return yao ni kubwa kuliko hata government bonds, ambapo ukiweka ela ndani ya mwezi ela uliyowka imerudi. Kwanini sasa matajiri ambao wanatumia mabilioni ya ela kununua governemnt bonds tena pesa inakaa miaka ili wapate return ambayo haifiki hata 25% wasingeweka huko hiyo ela?
WAnasema kampuni imeanzias uingereza, hivi kuna watu wanaojua uwekezaji kama wazungu? Kwanini wao wawekeze kwenye stocks ambazo return yake ni ndogo?
It is a scam. Google adesense ndiyo walipaji wakubwa wa kutazama matangazo wanajulikana dunia nzima kuwa ndiyo gwiji wa kulipa kwa views lakini wao wanalipa kati ya $3-5$ kwa 1000 views ila LBL wao wanakula 18000 kwa kutazama video 5 ambazo ni kama $5.
Watanzania tunatapeliwa kwa ujinga na kutokufanya background check. Tafuta hiyo kampuni mahali popote utaona haipo na wala haipo uingereza.
Uzuri watu wanaoingiza watu wanajua kuwa ni utapeli wanaingia mapema wanakula pesa wanabaki kuwachora. Mimi nilingia september na nilihisi haifiki december, ilipofika november na akaunti nikaigawa. Kua kabinti nilikambia usiwekeze pesa ya muda mrefu hii ponze scheme. Baadaye kakaja kuniambia kameweka pesa sijui ile ya meizi 3. Nikaona huyu hajaniamini. Mpaka sasa anaamini kuwa watarudi ila ndo wamesepa.