Lutah25
New Member
- Jan 28, 2025
- 4
- 12
Septemba 10,2024 Mahakama Kuu ilitoa uamuzi wa kuwarudisha kazini Askari watatu kama taarifa ilivyojieleza kwenye mtandao wa Mahakama ujulikanao kama TanzLii (Home - TanzLII) ambapo majina ya askari hao na sababu ya uamuzi uliotolewa vyote vimebainishwa katika taarifa hiyo.
Baada ya uamuzi huo sijawahi kusikia popote kwamba ni hatua gani zilizochukuliwa kutokana na kwamba taarifa hii imejumuisha Mihimili miwili (Polisi na Mahakama)kati ya mitatu inayounda dola ya nchi yetu.
Kinachonisukuma kuleta andiko hili hapa jamvini ni kutokana na jinsi suala hili limekaliwa kimya na linaleta maswali kadhaa kwamba:-
1. Je, askari hao wako salama tangu uamuzi ulipotolewa mwaka jana 2024 mpaka sasa?
2. Inakuwaje Jeshi la Polisi limekaa kimya bila kusema chochote kuhusiana na utekelezaji wa maamuzi ya Mahakama Kuu?
3. Ikiwa askari anapofukuzwa kazi Jeshi la Polisi kwa kawaida hujitokeza na kubainisha sababu au chanzo cha kumfukuza askari huyo, vipi pale Jeshi linapobainika kukosea katika maamuzi kwanini lisijitokeze na kutoa ufafanuzi kwa raia wake kuhusu suala kama hili?
4. Je kwa kukaa kimya hivi bila kutolea ufafanuzi masuala ya aina hii Jeshi la Polisi halioni kwamba linajenga taswira ya kudharau maamuzi ya mhimili muhimu hapa nchini (Mahakama) na kupelekea hata wananchi kufuata mkumbo wa aina hii?
Wito wangu ni kwamba Jeshi lijitokeze hadharani na kueleza kuhusiana na suala hili ili wananchi tujue kama askari hawa waliopewa tuzo ya kurudishwa kazini ikiwa wapo hai, wapo nchini Tanzania, au wako nje ya Tanzania na utekelezaji wa maamuzi ya Mahakama kuu umefikia wapi?
Wajibu wa Jeshi la Polisi ni pamoja na “Kulinda Raia na Mali zao” hivyo ili tuwe na imani na Jeshi letu ni pamoja na kutolea ufafanuzi masuala kadhaa hasa pale inapobainika kwamba Jeshi hilo liliamua au kutenda tofauti na matakwa ya kisheria.
Ramadhan Kareem✍️✍️