Jeshi la Polisi: Ukipewa dhamana polisi kutoka ni bure usitoe pesa

Jeshi la Polisi: Ukipewa dhamana polisi kutoka ni bure usitoe pesa

Mkuu wa jeshi la polisi amuhamishe huyu mama kutoka kule Geita matukio yamekuwa mengi sana inafikia hatua mpaka hao wezi wanamtishia maisha hata yeye na Kanda ya ziwa wanawadharau sana wanawake hasaakiwa Kiongozi.
 
Kwa Geita sawa ila hawa waketu huku Daslaam thubutuuu! Arooo nakwambia unarudi rumandeee shenzi type!
 
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amepiga marufuku tabia ya baadhi ya Askari kuomba rushwa pale ambapo Mtuhumiwa anapokamatwa na kupewa dhamana na Ndugu zake kwa kumtaka atoe chochote katika Vituo vya Polisi.

Akiongea na Wakazi wa Kata ya Kamoge Wilayani Bukombe Mkoani Geita Katika ziara aliyofanya Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigella, Jongo amesema ni marufuku Mwananchi kutoa kitu chochote kwa Askari endapo Mtuhumiwa atapewa dhamana na Ndugu zake kwa kutimiza Masharti.

"Jamani ehee kuingia Polisi bure kutoka hela hili jambo marufuku mbele ya Uongozi wangu Mimi Bibi yenu, ukiingia Polisi bure kutoka bure, wewe ukitoa hela umetoa rushwa na sitakubali nawaachia namba yangu ya simu mniambie huyo Askari anayedai hela kutoka ndani ya kituo cha Polisi Mimi sasa hivi nimehama kwenye Ubibi nitakuwa Shangazi”

RPC Jongo amesema baadhi ya Askari wamekuwa wakilichafua Jeshi la Polisi huku akiahidi endapo watagundulika atawachukulia hatua za Kisheria huku akiwataka Wananchi kutoa taarifa mapema kwa atakayeendelea kufanya hivyo.
Siyo POLISi wale wa stakashari
Wanakula rushwa hatari! Siyo wote lakini
 
Back
Top Bottom